Uchaguzi Igunga: Ni lini Upinzani utajifunza?

Natumia neno upinzani nikimaanisha kuwa upinzani unatarajiwa au walau unapashwa kuwa na united front...after all wanapingana na timu moja-chama tawala.

Swali kuwa lini upinzani utajifunza linatokana na matokeo ya uchaguzi wa Igunga hii leo. Ukweli ni kwamba CCM watashida (kihalali au kiwizi) kwa kupata 20% ya kura wakati Upinzani collectively watagawana 80% (vyama 7).

Ushindi wa CCM Igunga God forbid...uwe wa kihalali au kwa wizi kutatokana na exposure kwa wapinzani kwa kukosa umoja miongoni mwao. Watch this space

Hivyo vyama vingine viweke upande wa ccm, kwa hiyo ni kwamba vyama ni viwili tu ccm na cdm.
 
Kwanza Chama kama Chadema waungane na chama gani ?
Kuna vyama vilikuwa igunga muda wote nimevisikia leo navyo vya kuungana na Chadema .KUna vyama kama Bakwata, KAFU na CCM wao wameungana kwa maslahi ya matumbo yao si taifa .
mkuu Bakwata siyo chama ch Siasa
 
Achana naye huyo, kichenchede huyo.
Hata ww haujajifunza bado,SWALI KWAKO;kama upinzani hauwezi kushinda ilikuwaje asilimia 80% ya CCM ikashuka hadi 61%,na (b),ilikuwaje CDM kikashinda majimbo 21 kwa kishindo na (c),kama CDM haikushinda ilikuwaje CCM wakachakachua mpaka leo hii Makame anastaafu NEC haijawahi kutoa data za matokeo kama taharifa rasmi?

NB: Majibu yako ni muhimu mkuu.
 
utaungana na nani nimpinzani kama udp na wengine wa wanapata o ccm jike cuf vituo vingi hata kura 19 hawana?
 
Sioni ni wapi MoTown amekosea, yuko sahii kwa wazo alilokuja nalo: ushirikiano kwa vyama upinzani ili kuin'goa CCM ni muhimu sasa, hivi vyama vyetu vya upinzani unakuta vinapingana vyenyewe kwa vyenyewe ni hatari na itatuchukua muda kufanya kama watu wa Zambia.

we just imagine endapo CCM kule Igunga ikipata 20% ya kula zote na zikabaki 80% zikagawanywa kwa vyama 7 ina maana kila chama kitapata 11.4% ambazo ni ndogo sana huyo ni mfano.

Inabidi tufikilie kwa makini kama tunania ya kuachana na haya magamba kwa ujumla

Asante Mkuu kwa kuona concept iliyo wazi kabisa...ni bahati mbaya sana tunakuwa mashabiki kiasi tunasahau kuwa kila jambo lina technical aspect.

Swala la vyama vya upinzani kuwa na sauti moja (siyo itikadi) muhimu kuliko kuwa na mashabiki wasiotaka maendeleo ya upinzani.
 
Mara ya kwanza wapinzani waliposhinda uchaguzi Zambia, kilichowasaidia ni kuungana na wote wakiwa na nia moja tu, ya kumwondosha Banda madarakani. Na hivi juzi ndio hivyo hivyo. Kwa nini vyama vya upinzani TZ vinashindwa kuunganisha nguvu. Vyama vya upinzani vikunganisha nguvu, vinawaunganisha Watanzania, vikigawanyika kama ilivyo sasa, vinawagawa Watanzania na matokeo yake tunawapa mwanya mkubwa wa kufanya wanavyotaka. Angalia hizi hesabu za chapchap ingawa sijui kama haya ndio matokeo rasmi:

CDM:23620
CUF: 2104
JUMLA:25724

CCM: 26484-
CDM+CUF:25724
Jumla: 760
Hii ni kusema kwamba iwapo vyama upinzani vingeungana visingeshindwa na kura 761 kuwaondosha CCM pale. Watanzania tuamke, UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU.
 
@ mammamia
mimi naona maamuzi yako yanaweza kuinufaisha CUF peke yake maana ktk madaraka/uongozi itabidi waweke uwiano sawa lakini vipi kuhusu uwiano wa kura uoni kuwa ni mzigo kwa chadema? Maana hawa jamaa hawakubaliki sana huku bara, yani ni bora kama wangekuwa na nguvu sawa
 
mkuu Bakwata siyo chama ch Siasa

Wanatumika vibaya na ccm ili kuuwa vyama vya upinzani hasa Chadema au umesahau tamko Lao la hivi majuzi kuwahimiza wafuasi wao(waislam)wasikipigie Chadema kura!!?
 
Mara ya kwanza wapinzani waliposhinda uchaguzi Zambia, kilichowasaidia ni kuungana na wote wakiwa na nia moja tu, ya kumwondosha Banda madarakani. Na hivi juzi ndio hivyo hivyo. Kwa nini vyama vya upinzani TZ vinashindwa kuunganisha nguvu. Vyama vya upinzani vikunganisha nguvu, vinawaunganisha Watanzania, vikigawanyika kama ilivyo sasa, vinawagawa Watanzania na matokeo yake tunawapa mwanya mkubwa wa kufanya wanavyotaka. Angalia hizi hesabu za chapchap ingawa sijui kama haya ndio matokeo rasmi:

CDM:
23620
CUF:
2104
JUMLA:
25724

CCM:
26484-
CDM+CUF:
25724
Jumla:
760

Hii ni kusema kwamba iwapo vyama upinzani vingeungana visingeshindwa na kura 761 kuwaondosha CCM pale. Watanzania tuamke, UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU.

Mkuu hapa Tanzania huwezi kuunganisha vyama kirahisi kama unavyofikiria zambia na kwingineko.

Hapa kwetu ccm imepandikiza watu wake ndani ya vyama vya siasa kwahiyo hamuwezi kuungana mkafanikisha chochote. Mipango na siri zote zitakuwa zinawafikia ccm kabla hata hamjamaliza kikao. Kwahiyo njia pekee iliyopo kwa sasa ni kila chama kisimame chenyewe, watanzania watapima ni nani wa kweli na ni nani wa uongo na kisha watafanya maamuzi.

Pamoja na hujuma wanazofanya ccm dhidi ya wapinzani wa ukweli kwa kutumia vyombo vya dola na serikali kwa ujumla lakini lazima tukubaliane kwamba tunakoelekea ni kuzuri mno kuliko tulikotoka, tutashinda tu muda si mrefu, hawa polisi tushaanza kuwazoea na siku watu wote wakichoka kuibiwa kura na kuonewa, safari ya ccm itakuwa imetimia.
 
Natumia neno upinzani nikimaanisha kuwa upinzani unatarajiwa au walau unapashwa kuwa na united front...after all wanapingana na timu moja-chama tawala.

Swali kuwa lini upinzani utajifunza linatokana na matokeo ya uchaguzi wa Igunga hii leo. Ukweli ni kwamba CCM watashida (kihalali au kiwizi) kwa kupata 20% ya kura wakati Upinzani collectively watagawana 80% (vyama 7).

Ushindi wa CCM Igunga God forbid...uwe wa kihalali au kwa wizi kutatokana na exposure kwa wapinzani kwa kukosa umoja miongoni mwao. Watch this space

Dogo elewa vyama vinaunganishwa na sera sio kuungana tu kwa madhumuni ya kuiondoa CCM. Ikiwa sera zenu zinatofautiana mnaungana kutafuta nini???
 
Back
Top Bottom