Uchaguzi Chadema

Uchaguzi Chadema

Emmanuel Luoga

Senior Member
Joined
Oct 26, 2012
Posts
111
Reaction score
29
Tumekuwa wanachama wa CHADEMA kwa miaka
mingi mbona hatukuvaa kombati mpaka wakati wa
Mbowe? Tumekuwa wanachama wa CHADEMA kwa
miaka mingi mbona hatukuitwa makamanda
mpaka wakati wa Mbowe? Tumekuwa wanachama
wa CHADEMA kwa miaka mingi mbona
hatukuitumia nguvu ya umma mpaka wakati wa
Mbowe? Tumekuwa wanachama wa CHADEMA kwa
miaka mingi mbona hatukuwa kitisho kwa utawala
wa mafisadi mpaka wakati wa Mbowe? Tumekuwa
wanachama wa CHADEMA kwa miaka mingi mbona
hatukuwa chama kikuu cha upinzani mpaka wakati
wa Mbowe? Ukiyajua hayo utakubaliana nami
kwamba, Mbowe ni kiongozi makini na mwenye
weledi. Hilo ndilo linalowanyima usingizi mafisadi.
Wanakosa raha sababu ya umakini wake.
Wameendesha propaganda nyingi zikaangukia pua.
Swali tunalopaswa kujiuliza wana CHADEMA, hivi
wapinzani wetu ccm wanaweza kutuelekeza
kiongozi bora wa kuiongoza CHADEMA? Hivi huyo
wanaetumia muda wao mwingi kumpamba na
kumpa sifa zisizo zake haimaanishi wamegundua ni
uchochoro kwao? Bila shaka chaguo lao ni dhaifu
kama wao. Hana uwezo wa kufanya harakati za
ujenzi wa chama, uwezo wake ni kujenga makundi
ya kubomoa chama. Uwezo wake ni kujenga
mitandao kama mafisadi. Wanaamini kupitia yeye
watakuwa wameiondolea CHADEMA upinzani halisi
na kuwa na upinzani wa kishikaji kama vyama
vingine. MUNGU ibariki CHADEMA maana ndilo
tumaini la watanzania.
 
Hakuna anayebisha kwamba amefanya kazi nzuri sana ya kuijenga CHADEMA na anapaswa kushukuriwa kwa hilo lakini kusema kwamba ndio iwe sababu ya Mh Mbowe kuendelea kuiongoza CHADEMA nadhani hapo umeteleza mkuu.Kumbuka ni juzi Mwenyekiti wetu tunayempenda akiwa Denmark katika Mkutano wa ndani na Chama cha Conservative moja ya mambo aliyokuwa anayapigia upatu katika mkutano huo ni kujenga hali ya kuthamini Democratic values & principles ndani ya Nchi yetu.Na kwa kuitishwa Uchaguzi ndani ya Chama ambapo Wanachama wote watakaoona wana sifa nzuri na zinazofaa kulingana na maelekezo ya Katiba ya Chama basi na waachiwe wagombee kwa kufanya hivi CHADEMA kama Chama tutakuwa tumeudhihirishia Ulimwengu kwamba tumedhamiria kujenga Tanzania mpya yenye kujali na kuheshimu misingi ya Kidemokrasia na zaidi itamjenga zaidi Mbowe kiheshima kama mtu mwenye kuheshimu Demokrasia kivitendo.Lakini kuitishwa kwa Uchaguzi na hatimaye kupatikana kwa Uongozi mpya utaweza kuuwa hoja kwamba CHADEMA haina hazina ya kutosha ya Uongozi.Thanks
 
Mkuu na kubaliana na wewe pia naishi nikiamini kuwa mabadikliko ni lazima, muhimu kufanyika mahali popote pale. Ni kweli chadema inaitaji kufanya uchaguzi wao kwa mujibu wa katiba ya Chadema, na nimuimu wakafuata katiba yao. Ila mabadiliko ni muimu yafanyike ndani ya muda muafaka na sio kufanya mabadiliko eti kisa mwaka jana tulifanya mabadiliko kipindi kama hiki. Ila timu bora inayocheza vizuri na jinsi dakika zinavyoenda inaonyesha kuna kila dalili ya kupata goli la ushindi huwa haiwapumzishi mastar wake bali huwaongezea nguvu. Na hili ndilo tunaloliona ndani ya Chadema kwamba Uongozi wa Kamanda Mbowe na katibu wa W.P. Slaa unakaribia kuleta ushindi kwa watanzania wote dhidi ya adui yetu mkubwa CCM.

NB: Kosa kubwa litakalowagarimu Chadema kwa miaka mingi ijayo ni kuiaribu au kuweka sura mpya katika uongozi wa juu ya chama. Na hii nikutokana kuwa mwenyekiti wa chadema ni mtu alieandaliwa kwa muda mrefu na amefanya maandalizi mengi na amepitia magumu mengi mpaka kupanga kikosi chake na sasa ndio muda muafaka wa kutumia kikosi chake.
Pia katibu wao Dr. P. Slaa ni moja kati ya tunu za taifa hili iliyoandaliwa kwa gharama kubwa na chama cha Chadema ili aje kuliongoza taifa hili na kulifikisha linapostaili.

Na shetani CCM anasubuiria Adam (Chadema) ale tunda ili apate kutawala ulimwengu (Tanzania)
 
Aaaaghrrrrr!!!!!! mimi nilijua unatangaza tarehe ya uchaguzi kumbe simulizi za sungura na fisi?
mleta mada hana hoja ya msingi, matarajio yangu ni kuona tarehe ya uchaguzi kumbe anatuletea hadithi za pwagu na pwaguzi? kweli unamtindio wa ubongo, si kosa lako, ni uwezo mdogo wa uwelewa ndo unakusumbua.
 
Mie nilidhani makamanda tunafanya uchaguzi hivi karibuni?maana inabidi tubadilishe mtu kwenye nafasi ya Katibu Mkuu,huyu tuliyenaye ni full majanga,nasikia kampachika mimba house girl wake.
 
Huo ni uropokaji kama wa nape huwezi kujiita na Wewe great thinker naomba urudi facebook, huku hakukufai..
 
Mie nilidhani makamanda tunafanya uchaguzi hivi karibuni?maana inabidi tubadilishe mtu kwenye nafasi ya Katibu Mkuu,huyu tuliyenaye ni full majanga,nasikia kampachika mimba house girl wake.

Embu naomba nieleze jinsia yako kwanza, maana naongopa kukulaumu kwa ulichokiandika hapo na huku kumbe jinsia yako inaruhusu kufanya hivyo
 
Unazidi kutuaminisha kuwa CHADEMA ni chama cha kifalme kisicho na uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa kipo kwa manufaa ya watu wa kaskazini tu
 
Kalenda ya uchaguzi ni 2014 sasa tuzungumzie katiba, mambo ya uchaguzi wa chadema yatatangazwa wakati ukifika na wananchama wake wataamua nani awaongoze,
 
CCM ni wajanja sana wanatakakuifundisha CHADEMA ili ifuate matakwa yao kwa kisingizio cha demokrasia.Isije ikawa magamba wamemwandaa mamuluki ambae wanataka kumupenyeza kwenye safu ya uongozi wa CHADEMA ili wapate kaunafuu fulani baada ya kubanwa kisawa sawa na uongozi uliyopo.Hii huruma ya magamba kwa CHADEMA wanaitoa wapi?Tangu lini magamba wakawa na demokrasia ya kweli kiasi cha kutaka kuifundisha CHADEMA demokrasia?.Mbona Mwenyekiti wao wa kwanza Jk Nyerere alikaa kwenye uongozi wa TANU bila kuitisha uchaguzi mpaka akaipeleka kwenye uhuru mwaka1961 hata baada ya nchi kupata uhuru aliendelea kuwa mwenyekiti.Ikazaliwa CCM akaendelea kuwa mwenyekiti hivyo hivyo huku akiendelea kuwa Rais wa Tz hata alipoacha urais kwa kipindi cha zaidi ya miaka 30 alikataa kukabidhi nafasi ya mwenyekiti wa chama alikuja kukabidhi baada ya kujiridhisha kuwa sasa ni wakati muafaka wa kukabidhi nafasi hiyo.tangu wakati huo nafasi ya Urais na kwenye chama wagombea walikuwa ni mwenyekiti na kivuli mtindo ambao unaendelea mpaka sasa kwenye nafasi ya uwenyekiti wa chama ambapo ni maruku mwenyekiti wao kupingwa mpaka baada ya muda fulani kupita.Ukija upande wa CHADEMA hakuna hata kiongozi mmoja aliekaa zaidi ya miaka 30 wawe waasisi wa chama au awe nani.Ukiangalia kwenye safu ya uongozi wote ni viongozi wapya humukuti kiongozi wa mwaka 47.CHADEMA wanafaa kuwa walimu wa demokrasia.
 
Hivi neno democrasia lina maana gani? na huwezi ukatoa mifano ya TANU na CHADEMA kwani kila kimoja na wakati wake na mazingira halisi kama uongozi mbowe sio wakwanza kukiongoza CHADEMA
 
Mbowe amepokea urithi wa uenyekiti wa NGO ya mkwe wake. Hadi apatikane mwana ukoo mwingine ndio uchaguzi utafanyika
 
CCM ni wajanja sana wanatakakuifundisha CHADEMA ili ifuate matakwa yao kwa kisingizio cha demokrasia.Isije ikawa magamba wamemwandaa mamuluki ambae wanataka kumupenyeza kwenye safu ya uongozi wa CHADEMA ili wapate kaunafuu fulani baada ya kubanwa kisawa sawa na uongozi uliyopo.Hii huruma ya magamba kwa CHADEMA wanaitoa wapi?Tangu lini magamba wakawa na demokrasia ya kweli kiasi cha kutaka kuifundisha CHADEMA demokrasia?.Mbona Mwenyekiti wao wa kwanza Jk Nyerere alikaa kwenye uongozi wa TANU bila kuitisha uchaguzi mpaka akaipeleka kwenye uhuru mwaka1961 hata baada ya nchi kupata uhuru aliendelea kuwa mwenyekiti.Ikazaliwa CCM akaendelea kuwa mwenyekiti hivyo hivyo huku akiendelea kuwa Rais wa Tz hata alipoacha urais kwa kipindi cha zaidi ya miaka 30 alikataa kukabidhi nafasi ya mwenyekiti wa chama alikuja kukabidhi baada ya kujiridhisha kuwa sasa ni wakati muafaka wa kukabidhi nafasi hiyo.tangu wakati huo nafasi ya Urais na kwenye chama wagombea walikuwa ni mwenyekiti na kivuli mtindo ambao unaendelea mpaka sasa kwenye nafasi ya uwenyekiti wa chama ambapo ni maruku mwenyekiti wao kupingwa mpaka baada ya muda fulani kupita.Ukija upande wa CHADEMA hakuna hata kiongozi mmoja aliekaa zaidi ya miaka 30 wawe waasisi wa chama au awe nani.Ukiangalia kwenye safu ya uongozi wote ni viongozi wapya humukuti kiongozi wa mwaka 47.CHADEMA wanafaa kuwa walimu wa demokrasia.
Demokrasia ya kuwa mwenyekiti wa kudum??
 
Kalenda ya uchaguzi ni 2014 sasa tuzungumzie katiba, mambo ya uchaguzi wa chadema yatatangazwa wakati ukifika na wananchama wake wataamua nani awaongoze,
Mada inahusu uchaguzi wa SACCOS ya chadema. Suala la katiba tunasubiri juice siku ya jumanne
 
Kalenda ya uchaguzi ni 2014 sasa tuzungumzie katiba, mambo ya uchaguzi wa chadema yatatangazwa wakati ukifika na wananchama wake wataamua nani awaongoze,
Vipi kuhusu yule diwani wa chadema moshi aliyepiga fedha ya mradi wa wananchi akaswekwa lupango. Lissu ataenda kumtetea?
 
Magamba mbona imawauma sana hili la uchaguzi wa CHADEMA.....?nashawishika kuamini kwamba mnampango mbaya wa kuingiza mamruki kipitia uchaguzi.....kwa Taarifa yenu mbinu hii tumeshaigundua,hatufanyo kama mnavyotaka nyinyi.....
 
Back
Top Bottom