Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi



Duu? Ufisadi hadi muuza gazeti? ama kweli mafisadi wana mizizi mirefu, sasa hiyo ni sehemu ya gazeti ama wasifu ulikuwa umechomekwa tu? kama ni sehemu ya gazeti ni rahisi kumshughulikia! kwanza hata kwa wateja wenyewe manake kurasa zitakuwa hazijatimia!
 

Kama ndivyo hivyo basi inaonyesha bado wanaupeo mdogo wa siasa. Mpinzani wako mshinde kwa hoja sio kumyima ruksa ya kujitangaza.
 
Huu ni ushahidi kwamba bado CCM inatumia sana jeshi la polisi, tume ya uchaguzi na viongozi wa serikali katika kujihakikishia ushindi.

Nilishasema hapa hapa jukwaani kwamba CCM ikijaribu kufanya uchaguzi wa haki na huru na ikajidanganya kutaka siku moja kuingia uwanjani kutaka ushindi wa haki, itabamizwa kipigo cha mbwa koko.

Silaha za CCM katika ushindi katika uchaguzi hasa hasa katika chaguzi ndogo ni
  1. Ununuzi wa shahada za wapiga kura
  2. Kugawa rushwa, zawadi km nguo vyakula na vinywaji
  3. Matumizi ya Jeshi la polisi
  4. Kubebwa na Tume ya Uchaguzi
  5. Viongozi wa serikali kutumika kuibeba CCM na kuvibana vyama makini vya upinzani.
  6. Wizi wa kura
  7. Kulazimisha kutangazwa mshindi
Wakinyang'anywa silaha hizi hawawezi kushinda uchaguzi popotre hata pale Chalinze kwa Kikwete.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Childish... kweli wanasiasa wetu bado wanacheza mchezo huu kwa level ya mtoto wa miaka 3!
 

Yani umemwaga pointi tupu kamende, ila hUyo ibilisi aliye kuingia kwa hapo nilipo pigilia mstari ashindwe na alegee,

ama basi tuseme ni typo error, ulitaka andika

KISIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Rwagubiri

Kama kuna neno linaniudhi ni hili KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI. Nina uhakika neno hili linawaudhi watanzania wengine wengi. Ndani ya hili neno kuna kila hila. Umasikini wa Tanzania unatokana na hili neno pia. Ufisadi tunaoulalamikia na kuhangaika nao unatokana na hili neno.

Orodhesha mengi.............. utakuta kuwa yanatokana na hili neno
 
Kwani wapiga kura wangapi wana uwezo kununua hayo magazeti? Pia literace Tz ni 69% na huenda Geita iko chini ya hapo!

Watumie radio au mikutano au njia zingine!
 
Samahani pia wakuu, mbona hatupati update za kinyanganyiro uko, mlio 'richabo' tafadhali muwe mna tumegea ado ado.
 
Wadau mlioko Geita tupeni hizo updates za kinyang'anyiro kinachoendelea, Huyo katibu bado yuko mikononi mwa Polisi??
 

Sidhani kama ni sahihi, ndugu Kamende, kuhamishia madhambi ya muuza magazeti mkereketwa wa CCM kwa chama kizima cha CCM. Wapinzani CHADEMA na tusiopenda CCM kwa ujumla tumtangaze mgombea wenyewe.

 
Hii inaonyesa ni jinsi gani CCM walivyo waoga maana wnajijua hawana sera zaidi ya mabavu.

Ushauri wabure ccm mjipange upya tafuteni sera za kupingana sio mabavu, demokrasia ya kweli ccm haipo na hawajui nini maana ya DEMOKRASIA.
 
ni kwamba
kwakuwa mkuu wa majeshi mstaafu aliwahi kutaka kugombea mojawapo ya chaguzi ndogo basi ni dhahiri kwamba bado makada wa sisiemu wapo kwenye vyombo vya ulinzi na usalama hivyo lazma wawapendelee tu. pia ukichukulia kwamba katiba ya sisiemu imerekebishwa kmwamba makatibu wa kuu wa jumuiya za chama watoke ktk wakuu wa wilaya je unasubiri ushahidi mwingine?
wizi mtupu.
na usikute huyo muuza magazeti ataachwa huru na katibu wa chadema atasulubiwa.... yote yawezekana tanzania huru
 
Huyo fisadi anaenyofoa wasifu wa mgombea hafikirii kabisa. Huyo anatakiwa kurushiwa mabomu ya mbagala akafie mbali huko, ili akome kufanya hivo
 
Kilichobaki ni Tanzania Daima wamshtaki muuza magazati kwa kuingilia 'property rights' zao. Nadhani katika sheria, unaweza ku-argue kuwa rights za gazati zinabaki kwa mchapishaji mpaka pale 'consumer' anaponunua na sio msambazaji. Consumer ndo anaweza kuamua sasa kama aliwashe moto au vipi. Msambazaji (muuza magazeti) yeye anapochana kurasa, anakuwa anawaharibia soko, jina na 'rights zao over the published material'. Pia anawabania wananchi haki yao ya kupata habari.
 
Taarifa zilizotufikia muda huu CCM wanazidua kampeni Busanda leo tusikilizie huko habari za mapapa na manyagumi zitakuwaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…