EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,483
- 15,308
Kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Arumeru zinaelekea kuwachanganya wawekezaji hasa wa biashara ya maua jimboni humo kutokana na vyama vya CCM and Chadema kudai kwenye kampeni zao kuwa kama mgombea wao atachaguliwa watafanya mabadiliko makubwa kwenye umiliki wa ardhi jimboni humo.
Wawekezaji hao wakubwa wanaogopa kuwa watanyang'anywa ardhi wanayoimiki na kupewa wazawa wa kipato cha chini. Wakati wa ufunguzi wa kampeni za CCM, Rais mstaafu, Mh. Benjamini Mkapa aliwahaidi wananchi wa Arumeru kuwa atamshauri Rais Kikwete afanye mabadiliko ya umiliki wa ardhi jimboni humo.
Mkapa alisema land reform itawezesha kubadili umiliki wa ardhi kutoka mikononi mwa matajiri wachache kwenda kwa wananchi maskini ambao hawana hata ardhi ya kulima. Mgombea wa Chadema Joshua Nasar nae amehaidi kama akichaguliwa atahakikisha kuwa umiliki wa ardhi Arumeru unarudishwa kwa wananchi wa Arumeru.
Ripoti zinadai kuwa kilimo cha maua (horticulture) kimeingizia Tanzania fedha za kigeni karibu $990 million kwa miaka mitatu iliyopita. Karibia asilimia 80 ya kilimo cha maua Tanzania kinafanyika maeneo ya mlima Meru na wanaondesha kilimo hicho ni wawekezaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Muungano wa Horticulture Tanzania, Jacqueline Mkindi anapinga vikali mapendekezo ya kubadili umiliki wa ardhi Arumeru. Anadai kuwa wanachama wake wako kisheria Arumeru na jitihada zozote za kujaribu kuwaondoa zitaigharimu nchi. Bi Mkindi pia amedai wanafuatilia kwa karibu kampeni za uchaguzi Arumeru.
Dean wa Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu cha Tumaini Elifuraha Laltaika, amedai kuwa mapendekezo ya land reform Arumeru yako kimyume na Sheria ya Uwekezaji Tanzania ya mwaka 1997 and pia Katiba ya Tanzania. Anadai kwa vile makampuni ya maua yalifanya maombi kupitia ya Sheria ya Uwekezaji ya mwaka 1997, wana-enjoy "investment guarantees" ikiwa ni pamoja na "predictable investment climate."
Bw. Laltaika amezungumzia kifungu cha 22 cha sheria ya uwekezaji ambacho kinasema kuwa "no person who owns, whether wholly or in part, the capital of any business enterprise, shall be compelled by law to cede his interest in the capital to any other person." Pia amedai Ibara ya 13(2) ya Katiba inasema kuwa "No law enacted by any authority in the United Republic shall make any provision that is discriminatory either of itself or in its effect."