Uchaguzi 2015: Tujadili Aina ya Wapiga Kura

Uchaguzi 2015: Tujadili Aina ya Wapiga Kura

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Posts
4,850
Reaction score
9,434
Sehemu kubwa ya mijadala kuhusiana na uchaguzi mkuu 2015 inatawaliwa na hoja zinazohusiana na personalities – ‘choices' za baadhi ya wanachama lakini hasa viongozi wakuu wa vyama vya siasa na wapambe wao; Chini kwa chini makundi mbalimbali kutoka vyama vyote vikuu vya siasa pia yamekuwa yakiendela kuimarisha hoja zao kuhusiana na nani wanadhani ndio chaguo bora la watanzania kumpokea kijiti Rais Jakaya Kikwete October 2015; Katika makundi haya, wapo watu ambao tayari wameshajiridhisha kwamba chaguo lao/mgombea wao (sio chaguo la wananchi walio wengi) tayari ameshapita, na kinachosubiriwa ni muda tu wa kuapishwa; Mtazamo wa watu hawa unalipeleka taifa letu katika hatari kubwa kwani iwapo matokeo ya uchaguzi wa Rais 2015 yatakuwa ni kinyume na matarajio yao, hata kama uchaguzi mkuu utathibitika kufanyika katika hali ya Wazi na Haki, bila ya uangalifu, makundi haya ndio yatakuwa ni chanzo cha vurugu nchini kwani watachochea wananchi kukataa matokeo ya uchaguzi wa Urais; Hili ni jambo la hatari, hasa ikizingatiwa kwamba logic na vigezo vinavyotumika na wahusika kujiaminisha juu ya ushindi wa wagombea wao vinapwaya, hasa kutokana na kutozingatia hali halisi iliyopo kwenye electorate ;

Nia ya mada yangu ya leo ni kuziba ombwe lililopo katika mijadala ya urais kuelekea 2015, hasa kupanua zaidi mjadala kuhusiana na ‘choices' walizonazo watanzania 2015, badala ya choices walizonazo viongozi wa vyama vya siasa pamoja na wapambe wao;

Miaka 27 iliyopita (1985), Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alitamka maneno yafuatayo (Gazeti la Citizen, 19 Februari 2005):

"So my prayer to the socialists God is to get to have the American one party system in Tanzania...So my hope is that you can have another party; You can have two parties in Tanzania, both believing in the essentials of the Arusha Declaration. Then try to see which is going to be more efficient in implementing it. But one Socialist party, One Capitalist party, theoretically Yes, but i don't know how it can Work"

Maneno haya ya Baba wa Taifa yalikuja miaka michache kabla ya kuanza kwa mjadala wa vyama vingi Tanzania, hasa kufuatia uteuzi wa Tume ya Nyalali iliyozunguka nchi nzima kuchukua maoni ya wananchi kuhusiana na mfumo wa siasa unaowafaa. Mwalimu alienda mbali zaidi na kutumia tamthili/ufanani (analogy) ya mfumo wa taifa la Marekani ambapo alisema ingawa Marekani ina vyama viwili vya siasa:

"...But they are really one party. Both Parties agree on the basic national objectives. Internally, both of them are highly capitalist. Externally, both of them are imperialist".

Mwalimu nyerere pia akaelezea matumaini yake kwamba siku moja CCM itameguka na kuzaa Vyama Viwili vikubwa na vyenye nguvu - both Socialist and Both Nationalist;

Kwa bahati mbaya au nzuri kutegemeana na mtazamo wa mtu, Mungu wa Ujamaa hakujibu sala za Mwalimu Nyerere kwani - badala ya CCM kumeguka na kuwa vyama viwili vikuu vyenye nguvu, CCM ikaamua kulizika azimio la Arusha, lakini pia kuzika Nationalism (Utaifa) na Socialism (Ujamaa); Lakini muhimu zaidi ni kwamba vyama vyenye nguvu ya kupambana na CCM ni chama tofauti na vile alivyotabiri Mwalimu kwa kutumia analogy yake ya mfumo wa kisiasa wa marekani kwani Chadema na CUF vytoe sio Socialist na bado vina safari ndefu ya kuwa true nationalists; Vinginevyo nje ya hapo, ni vyama vitatu tu nchini kati ya karibia vyama ishirini ambavyo vina sifa ya kuitwa vyama vya siasa. Vyama hivyo ni CCM, Chadema na CUF kwani tofauti na vyama vingine, ni hivi vitatu tu ndio kwa zaidi ya miaka kumi vimeonyesha 'consistency', 'organisation na 'institutionalization';

Lakini pamoja na haya, vyama hivi vitatu kimsingi vinakabiliwa na tatizo moja kubwa – havina utofauti wowote wa maana in terms of Vision, Outlook & Major Policies; Hata CCM ambayo inajisifia kuwa na sera bora, sera zake zimeshindwa kuleta manufaa ya maana kwa wananchi walio wengi (vijijini). Mbaya zaidi, vyama vyote hivi vitatu vinategemea wahisani (donor – dependent); Pili, vyama vyote hivi vina abudu sera za uliberali mamboleo - liberalisation, privatization, marketization bila ya mchujo na matokeo yake ni ‘Maisha Bora Kwa Walio Wachache' kwani huo ndio msingi wa ‘Washington Consensus'; Wasiwasi unakuwa mkubwa zzaidi pale mtu unapobaini kwamba hakuna hata chama kimoja kinachoweka wazi jinsi gani kinajenga dira mbadala ya taifa ambayo ni home - driven (badala ya donor - driven), na havina mikakati ‘elaborate' ya kujenga ‘a democratic economy'; Katika suala la kujenga mfumo wa utawala ambao utakuwa na manufaa ya watanzania walio wengi i.e. wanavijiji, pengine Chadema kidogo imeonyesha nia kupitia sera yake ya majimbo na pia uasisi wa mabadiliko ya katiba mpya;

Swali linalofuatia ni - Je, katika mazingira ya namna hii, tunapoelekea Uchaguzi mkuu wa 2015, wapiga kura wa Tanzania wanaenda kupigia kura kitu gani hasa/kuchagua kitu gani hasa?

Mwaka 2005, Profesa Issa Shivji alichapisha makala moja ambayo ililenga kuchambua choices walizokuwa nazo watanzania kuelekea uchaguzi mkuu wa 2005; Katika uchambuzi wake, aligawanya ‘choices' za watanzania katika makundi makuu matatu. Nina amini kwamba uchambuzi huu wa Profesa Shivji bado ni relevant kwa uchaguzi mkuu ujao (2015). Shivji alijadili choices za watanzania katika makundi yafuatayo:

1. The Common Sense Choice
2. The Pragmatic Choice
3. The Rational Choice

Huku akisema kwamba kuna jingine – ‘The principled Choice', lipo kinadharia zaidi kuliko kivitendo. Kwa mujibu wa Shivji, mvuto kwa kundi hili ni ‘unique principles and policies' za vyama husika na anajadili kwamba ‘principled choice' kwa bahati mbaya bado haipo Tanzania na hoja ya msingi katika hili ni kwamba kimsingi hauwezi kutofautisha sera za vyama vyote vikuu vya siasa Tanzania vya - CCM, Chadema na CUF (rejea mjadala hapo juu kuhusu vyama vya siasa kuwa donor – driven). Kwa muktadha huu, Shivji anajadili choice kuu tatu zilizopo Tanzania ni kama ifuatavyo:

  1. The Common Sense Choice

Hili ni kundi la kwanza kwa mujibu wa Shivji. Njia rahisi inayowekwa na Shivji kutusaidia kuelewa nature ya kundi hili ni kulifikiria katika muktadha wa dhana maarufu isemayo kwamba:

"Better the devil you know than the devil you do not know";

Lakini haraka haraka, Shivji anasema kwamba – 'Common Sense, however is not always Good Sense', na kuzidi kufafanua kwamba:

"If you continue to strengthen the devil you know, there is a likelihood that he may be further emboldened to become even more devilish. These overwhelming electoral victories or what are called ‘ushindi wa kishindo', or with an even more ominous connotation ‘ushindi wa tsunami', have their consequences. Few parties and still fewer individuals who have got into the political seats with 70 – 80 percent of the vote can resist the arrogance of power. Self control in the exercise of power is a rare phenomenon."

2. The Pragmatic Choice

Kundi la pili kwa mujibu wa Shivji ni ‘Pragmatic' na anajadili kwamba kundi hili halipigi kura kufuatana na ‘instinct', ‘principle' au ‘reason'; Badala yake, Shivji anasema kundi hili linaendeshwa na ‘self interest' – bribes and favours, regional, racial, religious or gender prejudice and bias. Vile vile anasema kwamba kundi hili ndio kubwa kuliko makundi yote ya wapiga kura yaliyopo nchini, huku akisisitiza:

"We have already seen it in the internal nomination processes of the parties and should prepare ourselves to see more of it during the elections. Supposedly, there are watchdogs like the electoral commissions who are supposed to check such parties. But who watches the watchdogs"?

3. Rational Choice

Kwa mujibu wa Shivji, hili ni kundi la tatu na analijadili kwamba:

‘In absence of availability of principled choice, the most rational choice would be for a political configuration that assures stability, security, basic freedoms and checks on gross misuse of power. In our situation, theoretically speaking, it means a Union Parliament which would have a strong presence of the opposition; say 40% of the seats. As for the presidency, ideally, the winning candidate should end up with a slightly over 50% of the votes. In other words, ‘ushindi wa kishindo' should disappear from our political scene"

Lakini Shivji anajenga hoja kwamba watanzania kuwa na ‘rational choice' haina maana kwamba its a principled choice (rejea maana ya principled choice huko juu); Conclusion tunayoweza kuipata kwa shivji katika hili ni kwamba kwa vile Tanzania haina principled choice, watanzania wenye nia ya kutumia haki yao ya kujiletea mabadiliko watapigia kura Mgombea Urais kwa mtindo wa ‘rational choice', na wpiga kura wa namna hii hawatakuwa wengi sana ikifananishwa na wa makundi mengine – yani the ‘common sense and/or pragmatic';

Swali la kufungua mjadala: Je, madhara ya hali hii kwa CCM na Chadema kuelekea 2015 ni Yepi?

  • Kwa upande mmoja - kuhusiana na CCM na ni kwamba iwapo CCM itarudi Ikulu 2015, basi itakuwa kupitia kura za aina mbili tulizojadili yani – The Common Sense & Pragmatic Choices;

  • Kwa upande mwingine - kuhusiana na Chadema ni kwamba iwapo Chadema itafanikiwa kuingia ikulu 2015, basi itakuwa kupitia aina moja tu ya kura - the Rational Choice;

Hitimisho

Nikianza na Chadema - ni rahisi kubaini kwanini uchaguzi ujao (2015) Chadema haitapata kura za kutosha kuingia ikulu kwani mtaji mkubwa wa Chadema ni ‘rational votes' ambazo kwa bahati mbaya au nzuri kutegemea mtu upo upande upi wa hoja, kwa ngazi ya urais, ‘rational votes' hazitakuwa nyingi uchaguzi wa 2015 ikifananishwa na ‘common sense' and ‘pragmatic votes'; Lakini huko mbeleni (beyond 2015), kuna uwezekano mkubwa wa rational votes kuongezeka hasa kutegemeana na Umoja, Mshikamano, Uvumilivu na Ukomavu wa Chadema Kisiasa; Huu ndio mtaji mkubwa wa Chadema huko mbeleni, hasa iwapo wataweza kuepuka mtego wa kukataa matokeo 2015, kwani kitendo cha kupinga matokeo 2015 kitaleta vurugu na kuzidi kutengeneza ‘common sense' and ‘pragmatic voters' (hasa vijijini)ambao ndio imekuwa ni nguzo kuu ya CCM; Kwa maana hii, iwapo Chadema itashindwa ngazi ya Urais 2015, itakuwa muhimu sana waepuke kuitwa chama cha vurugu kwa kukataa matokeo na kuifanya nchi isitawalike; Pamoja na uchache wa Rational votes ngazi ya Urais Tanzania ya leo, hili ndio tanuri la vyama makini kuzalisha principled voters, hasa iwapo vitafanikiwa kuja na sera mbadala za uliberali mamboleo ambao hauna msaada wowote kwa watanzania walio wengi;

Nikimalizia na CCM, ni muhimu CCM ibadilike sasa, vinginevyo iwapo CCM itaendelea kukataa kubadilika, basi itambue kwamba ingawa uwezekano wake kushinda Urais 2015 ni mkubwa kupitia kwa common sense & pragmatic votes, suala la kutegemea such votes is a short lived strategy and it is more of a POLITICAL LIABILITY kuliko POLITICAL ASSET; Baada ya uchaguzi wa 2015, ni dhahiri kwamba Rais yoyote wa kupitia CCM Chini ya CCM iliyokataa mabadiliko hatoweza kuleta mabadiliko yoyote ya maana kwa watanzania walio wengi (vijijini), hivyo the real value katika siasa za nchi will continue to be on rational voters na hawa watazidi kuongezeka na vyama makini vitakuwa na fursa ya kuwatumia vyema kuwabadilisha kuwa principled voters, huku sala za Mwalimu Nyerere to the Socialist God zikizidi kujibiwa;
 
Mkuu Mchambuzi, unategemea CCM ipi ibadilike? toka mwalim Nyerere kwenye kitabu chake "TUJISAHIHISHE" kila siku unawashauri, "wabadilike", nadhani na wao wanakujibu "wameshabadilika" sas hivi umeenda mbali hata kuwaza aina ya wapiga kuwa, wao bado" wamelala" mie nakushauri achana nao, na 2015 ni CHADEMA-mark this
 
Last edited by a moderator:
Pompo, sina uhakika kama umeelewa mantiki ya mada yangu;Mada hii haijalishi sana iwapo inajengwa na mwana ccm au mwana chadem, badala yake it's a fact in the electoral college mkuu;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Nadharia yako haina mantiki kwa siasa za Tz, hebu angalia takwimu za sensa ujue ni aina gani ya wapiga kura itakayokuwepo 2015 kwa takwimu sio nadharia .

aidha, jua kwamba kizazi kilichozaliwa ndani ya mfumo wa vyama vingi yaani 1992 na kukulia kwenye mfumo huo ndio wanaenda kupiga kura kwa mara ya kwanza unajua hao ni wangapi ? Then nadharia zako ndio zifuate.
 
Umeanza vizuri ku falsify hoja yangu lakini umeshindwa kuifunga vizuri kwa kutoa hoja mbadala au nikiazima neno lako - yenye mantiki; Kwa mtazamo wako, je wapiga kura wa leo ni wa aina gani? Natumaini hautawaweka wote katika kapu moja na badala yake utawajadili kimakundi; Wananchi wengi ni kweli wameichoka ccm, lakini katika kuwachambua wananchi hao, ni kosa kuwaweka wote katika kundi moja linapokuja suala la upigaji kura, bila ya kujalisha ni kizazi gani;

Ningependa kuona hoja yako mbadala, hasa maoni yako juu ya kwanini haukubaliani na uchambuzi wa profesa Shivji ambao mimi binafsi ni subscriber na nadhani sipo peke yangu katika subscription hiyo;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Ni nadharia nzuri na ya kweli lakini ni ngumu kueleweka, kukubalika au kufanyakazi.
Why?In every principle there is an exception.

Nadharia moja tu itakuwepo 2015 nayo ni; Wapiga kura wengi ni Vijana na wataka mabadiliko.
Mshindi ni yule atakayeweza kuifanyia kazi nadharia hiyo.
 
Nina sababu zifuatazo,
1. Ni kuwa kizazi kipya hakitakuwa kwenye kundi lile la common sense voters, kwani wao wameishi na kukulia kwenye mfumo wa vyama vingi hivyo ni kundi kubwa ambalo halina kumbukumbu zozote kuhusiana na maisha yalivyokuwa wakati wa Mwalimu NYerere... The old good days of communism.
2. Itategemea vyama vitakuwa na mikakati ya kulenga kundi gani hasa , ikizingatiwa kuwa hapa namaanisha makundi ya vijana wa kike na kiume, wanawake na wazee, atakayefanikiwa kupata kundi kubwa la vijana na wanawake atashinda.

3. Itategemea wagombea wa vyama viwili Cdm na Ccm , watakuwa na mvuto kwa kundi lipi zaidi old or new generation , nimesema new na sio young generation.

4. Itategemea vyama vitakuwa na ajenda gani ambazo zitawavutia wapiga kura wa makundi yote kujitokeza na kwenda kupiga kura.....yaani get out to vote .........kwani inawezekana ukaungwa sana mkono na kundi mojawapo lakini ukashindwa kuwashawishi wajiandikishe na hatimaye siku ya uchaguzi waende wakakupigie kura .

Takwimu za sensa zinaonyesha kuwa kundi la new generation , from 18-35 yrs ni wengi sana kuzidi hao wengine wenye uwezo wa kupiga kura , hii maana yake ni kuwa kuna wapiga kura wapya wengi kuliko wale waliowahi kupiga kura mara nyingi .
 
Haki Sawa, sasa nimekusoma, una hoja za msingi kwenye bandiko lako namba saba, nitakurudia muda sio mrefu for counter arguments; Pia nime click 'report abuse' by accident kwani natumia simu, lakini nawasiliana na mods kurekebisha kosa langu hilo;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mkuu Mchambuzi heshima mbele na naona mada yako imetulia.

Sasa nianze hoja yangu na suala la wadhamini na wahisani wanaosaidia vyama vyetu vikuu vya siasa ambavyo umevitaja.

Mdhamini mkuu wa vyama hivyo ni serikali ya CCM ambayo inawasaidia kuwapa ruzuku ambayo inafuatwa na sheria kwamba vyama vya siasa vinavyotambulika chini ya sheria ya msajili wa vyama vinastahili kupata ruzuku ili kujiendesha.

Sasa vilipoanzishwa vyama vya siasa wakati wa ukoloni hakukuwepo suala hili la ruzuku bali kulikuwepo wafadhili na watu mbalimbali binafsi kama Mzee Iddi Chaurembo, John Rupia na wengine ambao walishiriki kwa hali na mali kutoa michango yao kwa chama cha TANU na hadi wakati Mwalimu Nyerere anakwenda UN alilipiwa tiketi ya ndege na watu hawa.

Kwahio mkwamo (handbrake) yoyote kwa CHADEMA na CUF itaendelea kuwepo kwenye suala la kukualika kiasi cha kuaminika na electorate kupewa ufunguo wa kuingia IKULU.

Vyama vya siasa mahala popote duniani kwenye demokrasia inayoeleweka vizuri, vyama vya siasa vinasaidiwa na wafadhili, wahisani na kuimarishwa kuanzia mashinani (grassroots) hadi kwenye ngazi ya juu ya uongozi wake na kwa hali hii ni CCM pake yake ndio mshindi.

Wafadhili na wahisani wanaweza kuwa ni watu wa aina yoyote bila kuwashirikisha wageni ambao kisheria hawapaswi kushiriki siasa za nadni ya nchi iliyowakaribisha.

Kwahio kwenye masuala ya Vision, Outlook na Major Policies CHADEMA kwa mfano wanashindwa na CCM kwasababu CCM bado inaimba na neno Ilani ya uchaguzi na kwa kuonyesha vigezo kama mabarabara na madaraja lakini imefeli kweye maeneo kama sera ya ELIMU na AFYA kiasi cha kuwaachia watu kama VODAFONE na AIR TELL washughulikie masuala ya shughuli mbalimbali za kijamii.

Tunaona VODAFONE wanashughulika na hata kugawa misaada ya madawa au vifaa vinavyohusiana na utoaji wa huduma mahospitalini na AIR TELL wanavyoshughulika na miechezo mbalimbali ya bahati nasibu katika kupoza nyoyo za wananchi maskini.

Kimantiki ni kwamba makampuni haya hayalipi kodi vile inavyotakiwa ambayo ndio ingesaidia kuboresha huduma za ELIMU na AFYA lakini kwa kuwa CCM imesimamia sera za ubepari ambao siku zote unajali zaidi faida basi kila kitu kinasahaulika.

Nikija kwenye suala la voters ni kwamba CHADEMA au CUF bado wana kazi kubwa ya kuepuka madhara ya kushindwa uchaguzi wa 2015 kwani bado The Common Sense and Pragmatic Choices electorate ndio majority na ndio wanaohodhi majukwaa au platforms nyingi kama kwenye Radio, Mitandaoni na kwenye magazeti.

Kukua kwa technology ya mawasiliano kumekuwa ni katika maeneo fulanifulani ya nchi yetu ingawa bado kule remote areas kuna matatizo ya The Common Sense and Pragmatic Choices kuamua kwamba kama hawa wasio CCM hawana mvuto basi hawafai na wanapigwa chini.

Hivyo basi, nikihitimisha naona kwamba madhara kwa CCM yanaweza kuwa ni kupoteza majimbo mengi kwenye maeneo fulani ya nchi kutokana na baadhi ya sehemu kuwepo na ongezeko kuwa la Principled au Rational choice. Kwa hali hiyo kusababisha kuwepo na Bunge ambalo labda kidogo linaweza kuwa "neutralised".

Kwa CHADEMA sidhani kama wanaweza kupata kura nyingi kwenye uraisi kwa kuzingatia uwingi wa The Common Sense and Pragmatic Choices electorate, ila wanaweza kuzoa kura nyingi sana kwenye viti vya ubunge.

Ahsante.
 
Richard, do you have the numbers in place ? Au unaandika kimazoea tu!
 
Mkuu Mchambuzi, unategemea CCM ipi ibadilike? toka mwalim Nyerere kwenye kitabu chake "TUJISAHIHISHE" kila siku unawashauri, "wabadilike", nadhani na wao wanakujibu "wameshabadilika" sas hivi umeenda mbali hata kuwaza aina ya wapiga kuwa, wao bado" wamelala" mie nakushauri achana nao, na 2015 ni CHADEMA-mark this

kamanda hupo? Vipi rabikira yupo?nazani umenisoma kamanda,
 
Last edited by a moderator:
A very good analysis that for any patriot politician will have to put in consideration but too bad I don't see it happening that way come 2015 am not so sure if TZ is going to be the very same TZ we have always known cause like you said most literate(rational voters) will not be ready to accept the choice of majority of tanzanians

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Nina sababu zifuatazo,
1. Ni kuwa kizazi kipya hakitakuwa kwenye kundi lile la common sense voters, kwani wao wameishi na kukulia kwenye mfumo wa vyama vingi hivyo ni kundi kubwa ambalo halina kumbukumbu zozote kuhusiana na maisha yalivyokuwa wakati wa Mwalimu NYerere... The old good days of communism.
Common sense have nothing to do with ujamaa bali life as it is; many young boys and girls are common sense voters especially in rural areas; its only the youths in urban areas who risk change and their urban exodus exemplifies that; otherwise many rural youths are more conservative than liberal;

2. Itategemea vyama vitakuwa na mikakati ya kulenga kundi gani hasa , ikizingatiwa kuwa hapa namaanisha makundi ya vijana wa kike na kiume, wanawake na wazee, atakayefanikiwa kupata kundi kubwa la vijana na wanawake atashinda.
Hii ndio mantiki ya principled choice, naomba urudie nilijadili nini awali;

3. Itategemea wagombea wa vyama viwili Cdm na Ccm , watakuwa na mvuto kwa kundi lipi zaidi old or new generation , nimesema new na sio young generation.
Mvuto on issues or personality?

4. Itategemea vyama vitakuwa na ajenda gani ambazo zitawavutia wapiga kura wa makundi yote kujitokeza na kwenda kupiga kura.....yaani get out to vote .........kwani inawezekana ukaungwa sana mkono na kundi mojawapo lakini ukashindwa kuwashawishi wajiandikishe na hatimaye siku ya uchaguzi waende wakakupigie kura .
Hoja hii nimeijadili kwenye hoja yangu kuhusiana na rational choice and tranformation into principled choice, hasa jinsi gani vyama makini vinaweza kujipanga kutumia fursa hii kikamilifu;

Takwimu za sensa zinaonyesha kuwa kundi la new generation , from 18-35 yrs ni wengi sana kuzidi hao wengine wenye uwezo wa kupiga kura , hii maana yake ni kuwa kuna wapiga kura wapya wengi kuliko wale waliowahi kupiga kura mara nyingi .
Wapiga kura wa wapi hasa, rural or urban, na je unajaribu kusema kwamba hawa wote wapo uniform?bado sijakuelewa vizuri kwanini mtu wa miaka kumi na nane 2015 anaweza asiwe common sense voter lakini hasa kwanini asiwe pragmatic voter;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
A very good analysis that for any patriot politician will have to put in consideration but too bad I don't see it happening that way come 2015 am not so sure if TZ is going to be the very same TZ we have always known cause like you said most literate(rational voters) will not be ready to accept the choice of majority of tanzanians

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums

Mkuu Kaki, unaweza kufunguka kidogo ukajadili aina ya wapiga kura 2015 tofauti na mtazamo wa Shivji?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
.
Nadharia moja tu itakuwepo 2015 nayo ni; Wapiga kura wengi ni Vijana na wataka mabadiliko.
Mshindi ni yule atakayeweza kuifanyia kazi nadharia hiyo.

Kwanini umeita nadharia, je, haitakuwa vitendo? Pia kuhusiana na mabadiliko, wanataka mabadiliko kupitia nini - chama cha siasa? Personality ya mgombea? Ukijibu kama ni personality au chama, naomba ujadili kwa hoja;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mkuu Kaki, unaweza kufunguka kidogo ukajadili aina ya wapiga kura 2015 tofauti na mtazamo wa Shivji?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Kwa upande wangu naona uchambuzi wa shivji upo sahihi na ni swala amabalo nimeliona siku zote, kwa upande wa wataka mabadiliko ya utawala inabidi wafocus beyond 2015.

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Kwa upande wangu naona uchambuzi wa shivji upo sahihi na ni swala ambalo nimeliona siku zote, kwa upande wa wataka mabadiliko ya utawala inabidi wafocus beyond 2015.

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums

Unaweza funguka kidogo kuhusu ccm and beyond 2015 Strategy? Unaongelea suala la mgombea? Sera? Itikadi?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Nina sababu zifuatazo,
1. Ni kuwa kizazi kipya hakitakuwa kwenye kundi lile la common sense voters, kwani wao wameishi na kukulia kwenye mfumo wa vyama vingi hivyo ni kundi kubwa ambalo halina kumbukumbu zozote kuhusiana na maisha yalivyokuwa wakati wa Mwalimu NYerere... The old good days of communism.
2. Itategemea vyama vitakuwa na mikakati ya kulenga kundi gani hasa , ikizingatiwa kuwa hapa namaanisha makundi ya vijana wa kike na kiume, wanawake na wazee, atakayefanikiwa kupata kundi kubwa la vijana na wanawake atashinda.

3. Itategemea wagombea wa vyama viwili Cdm na Ccm , watakuwa na mvuto kwa kundi lipi zaidi old or new generation , nimesema new na sio young generation.

4. Itategemea vyama vitakuwa na ajenda gani ambazo zitawavutia wapiga kura wa makundi yote kujitokeza na kwenda kupiga kura.....yaani get out to vote .........kwani inawezekana ukaungwa sana mkono na kundi mojawapo lakini ukashindwa kuwashawishi wajiandikishe na hatimaye siku ya uchaguzi waende wakakupigie kura .

Takwimu za sensa zinaonyesha kuwa kundi la new generation , from 18-35 yrs ni wengi sana kuzidi hao wengine wenye uwezo wa kupiga kura , hii maana yake ni kuwa kuna wapiga kura wapya wengi kuliko wale waliowahi kupiga kura mara nyingi .

Siasa za Udini ziko kwenye Pragmatic Voters zitakuwa na role kubwa kwenye uchaguzi ujao! Ndio maana kuna uzi hapa unaonesha wataka urais wa CCM wamejikita kwenye nyumba za Ibada na CUF nayo imeshaanza rasmi...
 
Back
Top Bottom