Uchaguzi 2015: Tujadili Aina ya Wapiga Kura

Uchaguzi 2015: Tujadili Aina ya Wapiga Kura

Siasa za Udini ziko kwenye Pragmatic Voters zitakuwa na role kubwa kwenye uchaguzi ujao! Ndio maana kuna uzi hapa unaonesha wataka urais wa CCM wamejikita kwenye nyumba za Ibada na CUF nayo imeshaanza rasmi...

Naunga mkono hoja, hili linachangiwa sana na ombwe la itikadi miongoni mwa vyama vya siasa;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mchambuzi nashukuru sana kwa uchambuzi wako mzuri na unajitahidi sana kutokuwa na upande. Hata hivyo, kuna kitu hujakiona ambacho ni muhimu sana. Kwanza nakubaliana na wewe kuhusu aina 3 za wapiga kura. Hata hivyo, natofautiana na wewe kuhusu uwezekana wa pregmatic na common sence kuisaidia ccm 2015. Sijashawishika, kimantiki (am very objective hapa) kwamba kwenye ngazi ya urais chadema itategemea rational votes peke yake. Kwa nini nasema hivyo?
Mosi, pregmatic votes inaangalia masuala ya dini ya mgombea, kabila, ukanda, jinsia, uswahiba, urafiki nk. Ni mambo ambayo siyo ya msingi na yasiyofaa kabisa. Sasa basi, kama hivyo ndivyo, kura za pregmatics zitategemea mgombea aliyesimamishwa na ccm na anaingia ktk kundi gani la pregmatic vile vile Mgombea wa Chadema ni yupi anaingia ktk kundi gani la pregmatic. Kwa hiyo, pregmatic inaweza kuisaidia chadema au ccm ila tu inategemea mgombea aliyesimamishwa na vyama hivyo.
Tatu, kuna waziri moja wa ccm alisema shule za kata ndizo zitakazoiua ccm, nakubaliana naye 100%. Common sence group iko vijijini na hawa siyo vijana ni wazee. Kwa hiyo, kundi ni kweli ndio msaada wa ccm, hata hivyo kundi linakumbwa na changamoto kadhaa.
Mosi, kwa kuwa ni wazee, hili ni kundi linalopungua na vijana wanaongezeka.
Pili, vijana wa shule za kata wanawabadilisha kimtazamo wazee hawa wachache waliobaki.
Rational votes kama ulivyosema mwenyewe ni kura za chadema kutokana hali ya kisiasa ilivyo, kwa hiyo, nashawishika kuamini kwamba, kama uchaguzi wa 2015 utakuwa huru,Chadema itashinda kwa kishindo.
 
Michael P Aweda,

Karibu sana kwenye mjadala Kamanda, una hoja za msingi sana, ngoja nitulie nitazijadili;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
nimesoma bandikolako namba 1,ila naanza kwa kupinga kwamba si Rational choice pekee kama kundi la wapiga kura ndio chadema hutegemea,kwa sababu kwa sifa la kundi la 2. The Pragmatic Choice kama ambavyo limejieleza

"Kundi la pili kwa mujibu wa Shivji ni ‘Pragmatic' na anajadili kwamba kundi hili halipigi kura kufuatana na ‘instinct', ‘principle' au ‘reason'; Badala yake, Shivji anasema kundi hili linaendeshwa na 'self interest' – bribes and favours, regional, racial, religious or gender prejudice and bias. Vile vile anasema kwamba kundi hili ndio kubwa kuliko makundi yote ya wapiga kura yaliyopo nchini."

Sasa sehemu hizo nilizobold naona sifa za aina hiyo ya wapiga kura zinangukia kwa chadema ukiacha hiyo ya bribes and favours.
Kwa upande wangu naona watu wanaonufaika na favours si wengi kwa idadi sababu aidha ni wanafamalia wa watawala(watoto,mjomba,binamu nk ),rafiki wanaopewa vyeo vya kisiasa na wengine wafanya biashara wachache wachache ambao katika biashara zao wanapohusiana na wanasiasa biashara zao zisikwame.
kwa upande wa bribe sio lazima ikamfanya yule alipewa bribe abadilishe maamuzi ya kura yake,mtu anaweza pewa rushwa ya wali,nguo hela nk lakini bado kura yake ikawa siri yake,kwa hiyo point hii haimpi asimia mia mtoaji anufaike na yule aliyempa.
Self interest, naangukia kwenye sifa hii ikiwa nimeelewa kwamba ni mapenzi binafsi ya kunifanya nikipigie chama gani,kwa kutumia tabia hii mimi napigia chadema na wewe waweza pigia CCM au CUF

regional ,hii pia huwagawa wapiga kura wa pande zote za vyama vitatu ikiwa tu mpiga kura atapiga kura yake kwa kuzingatia hili na hivyo sifa hii pekee haiwezi kuwa kwa CCM pekee.mf mgombea wa CCM akatokea Zanziba na CDM akatokea Tanzania bara

religious hii inaweza kuathili chama chochote kile kwa idadi ya watu watakao pigia kura CCM,CUF ama Chadema.Kwa kutegemeana ni mtu wa dini gani ama simama kama mgombea

Narudi kwenye paragraph yako ya kwanza juu ya hatari ambayo umeiona juu ya kundi linalojiaminisha kwamba mgombea wao wanaamini ni lazima atashinda na ikiwa tofauti na hivyo hofu yako ni kwamba watazusha vurugu,bila shaka kundi hili unamaanisha upinzani na hasa chadema.
Lakini swalli linakuja je chama tawala(CCM) ambacho kinayo dola kitaweka mazingira ya uchaguzi yawe huru na haki ikiwa nao wanaapa kwamba kushinda kwao suala la lazima?na wanaona chama chochote kinachotaka madaraka ni adui wao mkubwa. Mimi naamini kama vurugu zitatokea kwa kundi linalojiaminisha kushinda basi vurugu hizo zitachangiwa na kutokuwepoka mazingira ya huru na haki katika mchakato mzima wa uchaguzi.

Mwisho nimalizie kwa msemo utaokinzana na common sense choice ambao ni bandu bandu humaliza gogo(nikimaanisha ufisadi wamuda mrefu hata kama unafanyika kidogokidogo,utamaliza rasilimali zote za nchi),VS Zimwi likujualo halikuli likakumaliza hii ikimaanisha kwa lile zimwi kuendelea kula mwisho atamaliza kila kitu hivyo ni bora kumkimbia ama kumkataa.Kwa common sense hii pia CUF ama Chadema wanachukua pia baadhi ya wapiga kura katika kundi hili,common sense pia huja baada ya kuwa more informed na naamini watu wanzidi kuwa informed kupitia different channels of influence ikiwamo mitandao ya kijamii.
 
Back
Top Bottom