bullet proof
Member
- Sep 19, 2012
- 57
- 35
Ikiwa ni takribani miaka 2 imebaki kabla ya uchaguzi mkuu nchini kufanyika, kuna baadhi ya wabunge wa CCM wenye nia ya kupeleka hoja bungeni ili kuruhusu vyama kuungana wakati wa uchaguzi kama ilivyokuwa Kenya. Wakati hali ikiwa hivi kuna kila dalili kuwa CCM kitaungana na CUF ili kusimamisha mgombea mmoja wa Urais! Je, kuna sababu ya CHADEMA kuungana na vyama au chama kingine ili kusimamisha mgombea mmoja? Na kama CHADEMA kitafanya hivi, vipi kikiungana na NCCR-Mageuzi? Na mwisho kabisa ushindani utakuwaje kati ya CCM na CUF dhidi ya CHADEMA na NCCR-Mageuzi?