UCHAGUZI 2010: ITV KUFUATA NYAYO ZA TBc1? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UCHAGUZI 2010: ITV KUFUATA NYAYO ZA TBc1?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kachanchabuseta, Sep 3, 2010.

 1. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  WanaJF tarehe 01/09/2010 Television ya CCM (CCMTV) au kwa kifupi TBC1 muda wa kuanzia saa 3 usiku warusha kipindi maalum "utendaji wa Jeshi letu" kabla ya hapo serikali ilitoa taarifa kuwa tarehe 01/09/2010 ni siku ya mshujaa(kama nimekosea utanikosoa)

  Kipindi hicho kulikuwa kinaonesha utendaji wa jeshi letu vifaa wanavyotumia lakini baadaye wajeshi wakiwa wameshikilia mitutu kwenye gwaride walikuwa wanaimba hivi "tuna imani na kikwete".........hawa waliandaliwa mana walikuwa vijana vijana wadogo wa jeshi.....

  Mwaka 2005 siku mbili kabla ya uchaguzi ITV warusha kipindi chao wakionesha MAUJI YA RWANDA.

  Hii ilileta fikra za woga kwa watanzania mana waliogopa vita


  CCM ina TABIA YA KUTUMIA JESHI IKIONA MAMBO HAYAJAKAA SAWA

  Mytake:
  1. Je ITV watarudia ya mwaka 2005?
  2.Kwanini TBC wanarusha mambo ya jeshi katika kipind hiki cha uchaguzi?
  3. Ila nawasii ITV na TBC kama wakiendelea na mchezo huu watanzania wamefunguka macho hawadanganyiki tena
   
 2. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  ITV inafahamika kwamba inawabeba ccm kwa kila mbinu, wako tayari kuonyesha kampeni za udiwani kwa wana ccm kuliko mgombea urais kwa vyama vya upinzani, na hawajaanza leo, kila mtu anakumbuka waliyoyafanya 2005 na hata miaka ya hivi karibuni wamekuwa wakinadi sera za kijani tu.
  Mmiliki wake mwenyewe alishatutangazia kwamba yeye ni ccm damu damu na kadi yake tukaonyeshwa, kwahiyo hakuna jambo jipya hapo.

  Ushauri wangu ni kwa viongozi, wapenzi na wanachama wa vyama vya upinzani kuunganisha nguvu na kuanzisha vyombo vyao habari, radio, tv na magazeti ili yaweze kukabiiana vizuri na radio, tv na magazeti ya wanazi wa ccm.
  Mfano mzuri ni hapo kwa majirani zetu kenya; NTV, CITIZEN TV n.k, n.k hadi kinaeleweka tu vinginevyo tutaendelea kulishwa propaganda za ccm kwa kulazimishwa kwakuwa hatuna vyombo vya habari huru!!
   
 3. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Mkuu JP

  Sasa kazi ndo imeanza wataanza kutisha watu na JESHI

  CCM ikishindwa SIRAH YAKE YA MWISHO NI JESHI

  LAKINI MWAKA HUU IMEKULA KWAO

   
 4. e

  emalau JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,179
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Wanajeshi wenyewe maonyesho yao ni kuvunja matofari kwa vichwa, kupigwa fimbo mpaka ikachanika ! hayo si maonyesho yanayotakiwa kufanywa na jeshi la kisasa. Wanajeshi wetu walinifurahisha sikumoja hapo makao makuu waliona mtu ameshika flopy disket wakamuuliza kwamba haitakiwi kushikwa na mtu wa kawaida isipokuwa wanajeshi tu ! yule jamaa aliwashangaa akawaambia hizi zinapatikana hata vichochoroni manzese wakabaki wameduwaa ! hawa ndo wanajeshi wetu!Hii inaonyesha jinsi jeshi letu lilivyolala usingizi wa pono, wakati technology kama GPS na GIS ndo zinatumika kwenye vita ya kisasa wenyewe wanavunja matofari kwa vichwa ! Mapigano ya sasa hivi hayatumii nguvu ya mwili, zaidi nguvu ya ubongo ndo inatakiwa.Sasa hii inaharalisha mawazo ya walo wengi kwamba jeshi sasa linahtaji commander in chief mpya atakayeweza kutoa new direction kwa jeshi, jeshi litakaloendana na wakati. having a new commander in chief is in the best interest of our military.
   
Loading...