Elections 2010 Kampeni za CCM Moshi Mjini na picha za kuchakachua

Kizimkazimkuu

JF-Expert Member
Nov 8, 2007
337
234
Nimeelezwa na jamaa aliyekuwapo uwanja wa mashujaa Moshi katika kampeni za JK Moshi kuwa hali haikuwa kama picha zilizoonyeshwa TBC1 ktk taarifa za habari. Ukweli ni Kuwa CCM walitangaza kuwa mkutanno ungeanza saa 8 lakini BURUDANI ZITAANZA KUANZIA SAA TANO ASUBUHI. Umati ulijaa kuona burudani na ze Comedy na Mkuu aliingia saa 11 jioni badala ya saa 8. Alipoanza tu hotuba, watu wengi wakaanza kutawanyika. Jamaa akaniambia kama nilikuwa makini ningeangalia picha, ni obvious ile picha ilikuwa edited. Ilikuwa ikimuonyesha Kikwete kutokea mbele na then crowd bila kuewa na picha iliyoweka view ya Kikwete na crowd yote similarly kama wanavyofanya kwa SLAA (siku wakipenda) wanamuonyesha pekee yake then wanachagua angle yenye watu wachache na watoto.Lakini hali ya kisiasa CCM wana hali mbaya HAI (Mh.Fuya Kimbita), SIHA (Agrey Mwanri) na Moshi mjini (Justin Salakana). Hapa Ndesamburo kaahidiwa na vijana kuwa kura watampa but awaache tu wapeperushe bendera na mabango ya CCM, Wanahasira mno na kukatwa jina la mfanyabiiashara ''mtoto wa mjini'' Athumani Ramole (Buni).
 
Iringa wanasema hawadanganyiki na Zecomedy. walimtaka mwakalebela. wamemkosa sasa watampa msigwa wa chadema. Hapa kweli ccm walijikaanga!
 
Hooooray!
Ukombozi uko jirani!
Sasa hv aukiangalia TBC muda mwingi wanamweka Amiri Jeshi Mkuu(jk) akiongelea habari za jeshi, kumbe ndo wanamuuza kiaina kwa watu!(what a shame)!
Lakini ndo huyo hauziki, wala hanunuliki!
 
Mtaaibika!Najua mtakimbia katika hili jukwaa mara baada ya matokeo kutangazwa!
 
du mwaka huu kazi ipo km kweli ccm walitekeleza ilani yao kwa nn wanatumia pesa nyingi hivi kwenye kampeni! shiit!
 
Mtaaibika!Najua mtakimbia katika hili jukwaa mara baada ya matokeo kutangazwa!

Mkuu Pengo, hakuna wa kukimbia ndugu yangu.
Suala zima la wizi wa kura twalijua even before 31/10!!!

Ukweli ni kuwa hali ya upepo wa kisiasa CCM ni mbya sana; taka usitake...
 
du mwaka huu kazi ipo km kweli ccm walitekeleza ilani yao kwa nn wanatumia pesa nyingi hivi kwenye kampeni! shiit!

Wamurubhere hata kuitaja wanaiogopa waliahidi maisha bora kwa kila mtu. Sasa wanajisifu na mambo ambayo ni wajibu wa serekali kufanya(kotokana na kodi zinazotozwa) kujenga shule,barabara,hospitali ingawaje nazo sio katika viwango stahiki.
 
Nimeelezwa na jamaa aliyekuwapo uwanja wa mashujaa Moshi katika kampeni za JK Moshi kuwa hali haikuwa kama picha zilizoonyeshwa TBC1 ktk taarifa za habari. Ukweli ni Kuwa CCM walitangaza kuwa mkutanno ungeanza saa 8 lakini BURUDANI ZITAANZA KUANZIA SAA TANO ASUBUHI. Umati ulijaa kuona burudani na ze Comedy na Mkuu aliingia saa 11 jioni badala ya saa 8. Alipoanza tu hotuba, watu wengi wakaanza kutawanyika. Jamaa akaniambia kama nilikuwa makini ningeangalia picha, ni obvious ile picha ilikuwa edited. Ilikuwa ikimuonyesha Kikwete kutokea mbele na then crowd bila kuewa na picha iliyoweka view ya Kikwete na crowd yote similarly kama wanavyofanya kwa SLAA (siku wakipenda) wanamuonyesha pekee yake then wanachagua angle yenye watu wachache na watoto.Lakini hali ya kisiasa CCM wana hali mbaya HAI (Mh.Fuya Kimbita), SIHA (Agrey Mwanri) na Moshi mjini (Justin Salakana). Hapa Ndesamburo kaahidiwa na vijana kuwa kura watampa but awaache tu wapeperushe bendera na mabango ya CCM, Wanahasira mno na kukatwa jina la mfanyabiiashara ''mtoto wa mjini'' Athumani Ramole (Buni).

Dah kwa kweli inatia moyo sana kuona wananchi wako makini sana mwaka huu na wanahasira na mabadiliko. Kama kweli watu wako makini namna hii kufuatilia hadi picha kujua ipi ni photoshop na ipi ni halisi, inamaana hata kufuatilia na kudhibiti wizi wa kura tutaweza safari hii. Go Dr. Slaa Gooooooo
 
Mtaaibika!Najua mtakimbia katika hili jukwaa mara baada ya matokeo kutangazwa!

Ninaamini kwamba CCM mtaiba kura maana hiyo ndiyo tabia yenu. Ila nina amini pia kwamba mwaka huu tunaweza kuzipiga Tanzania. Nina wasiwasi mkubwa sana kwamba yaliyotokea Kenya mwaka 2007 yanakuja Tanzania iwapo CCM haitataka kuridhika na matokeo na ikaamua kuiba kura. Kwa bahati mbaya sana hao mnaowaita usalama wa taifa ambao daima huwa wanaipigia magoti CCM, mwaka huu wapo upande wa Slaa. Physically wanamuunga mkono JK, spiritually wapo na Slaa bega kwa bega. Kumbuka kuna yale makombora 20 ambayo Dr Slaa bado hajayavurumusha. Tunasubiri angalau wiki mbili kabla ya uchaguzi ndipo tuyarushe. Mtakula jeuri yenu mwaka huu.
 
Hooooray!
Ukombozi uko jirani!
Sasa hv aukiangalia TBC muda mwingi wanamweka Amiri Jeshi Mkuu(jk) akiongelea habari za jeshi, kumbe ndo wanamuuza kiaina kwa watu!(what a shame)!
Lakini ndo huyo hauziki, wala hanunuliki!

Hhahaha kaka bidhaa imeshaexpire haiuziki kaka. ccm mwaka huu hawana chao anguko kubwa lawasubiri october na wakianguka hawainuki tena milele.
 
Katika hali ya kuonyesha kukata tamaa na kuamua kujaribu mbinu chafu, lilikuwepo jaribio la kuwapa kadi za Chadema wanafunzi wa vyuo (kwa hakika mwanafunzi wa chuo cha ushirika amenithibitishia hili) ili wazirudishe siku ya JK na itangazwe wasomi wa vyuo vikuu wamehama CHADEMA...... nadhani hili lilifanikiwa. Pia ikumbukwe kuwa ziara ya JK Moshi iliahirishwa was supposed to be there earlier, nadhani kutoa nafasi ya kutayarisha mazingira ya kufunika fedheha. Umati mkubwa unamfuata huyu jamaa sababau ya Zecomedy, walipomaliza tu wachaga wakarudi kwenye shughuli zao....SASA TUSUBIRI UMATI WA UKWELI SIKU YA TAREHE 22 SEPTEMBER atakopoingia SLAA katika venue ile ile aliyoitumia JK, Mashujaa Ground.
 
Wanaochakachua picha kwa kuonyesha kwamba J.K. amepata umati mkubwa ktk mikutano yake ambapo ukweli sivyo, hawamsaidii mgombea wa CCM. Aidha wanaoleta washangiliaji kwa malori ya fuzo na mabasi kushangilia hawamsaidii J.K. Kama J.K. hatambui umati na washangiliaji ktk T.V. ni wa kughushi, ataendelea kudhani kwamba umma unampenda kumbe ni vinginevyo. Waacheni ccm waendelee kujidanganya.

Nawashauri wanaChadema na Dr. Slaa waendelee na kampeni zao za kuwaambia WaTz. ukweli bila kujali picha za kuchakachua zinazoonekana ktk TV au ktk magazeti. Wachambue kwa umakini sababu za matatizo ya nchi na kupendekeza majawabu ya kisayansi. Chadema hatuwezi kukumbatia nguvu za giza na za kishirikina. Tujue kwamba wapiga kura ni wale watu halisi wanaosikiliza hotuba. Tuwaheshimu. Tuwaridhishe kwa mantiki.

Hakuna kulala, Mpaka kieleweke.
 
Wazo zuri sana hili mzee Mtei,
Juzi nimeongea na mzee mmoja aliyehudhuria moja ya mikutano ya Dr Slaa kanda ya ziwa. Huyo mzee ambaye amekuwa mwanachama wa ccm kwa miaka mingi sana (toka enzi za TANU) aliniambia kuwa, kuhudhuria mkutano wa Dr Slaa ni kati ya maamuzi bora kabisa aliyowahi kufanya maisha yake.

Issue iliyomgusa sana kuliko zote, ni ile ya kuwa na magari ya kifahari ya thamani ya milioni mia mbili wakati hospitali karibu zote nchini hazina dawa za kutosha.

CHADEMA endelezeni kuwafumbua wananchi macho. Hii ndiyo inaitwa elimu ya uraia. Hakuna mtu (esp ccm na corrupt media ya Tanzania) atakayefanya kwa niaba yetu.

MUNGU awabariki na kuwalinda kwa kazi nzuri sana mnayoifanya kwa ajili ya nchi yetu.
 
Back
Top Bottom