Uchafu wa Nagu Hanang | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchafu wa Nagu Hanang

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mtanzania1989, Sep 11, 2012.

 1. m

  mtanzania1989 JF-Expert Member

  #1
  Sep 11, 2012
  Joined: May 20, 2010
  Messages: 2,143
  Likes Received: 1,711
  Trophy Points: 280
  Wadau , hii nimeikuta http://www.shaffihdauda.com/ , najaribu kuwasiliana na mhusika ili akubali kuja kushusha ushahidi wake humu

  "
  MICHEZO, MISITU NA VYANZO VYA MAJI VINAPOHUJUMIWA KWA WAKATI MOJA NA VIONGOZI WALIOCHAGULIWA AMA KUTEULIWA ILI KUVILINDA!


  1). Inawezekana vipi mbunge mzima wa wilaya ya Hanang awakingie kifua wajomba zake waliovamia viwanya vya michezo na vyanzo vya maji kwa wakati mmoja na wasichukuliwe hatua za kisheria hadi leo?

  2). Kama hiyo haitoshi wananchi wa kitongoji cha Endamanang kijiji cha Nangwa walipofanya jitihada za kumweleza DC-Hanang na kufanikiwa kuwekwa ILANI YA SERIKALI lakini wajomba hao wa Mary Nagu wanaoitwa NINO YAHHI na SIKUKU AXWESSO wakavunja na kutupa ilani hiyo July19, 2011 na kuendelea kukingiwa kifua hadi leo huku wakiendelea kulima
  eneo lililokatazwa kisheria hawajafunguliwa mashtaka hadi leo?

  3). Je uvamizi wa viwanja vilivyoachwa na serikali yetu kwa manufaa ya watoto wetu, na uvamizi wa vyanzo vyetu vya maji ndiyo ilani ya CCM?
  Kama siyo ilani ya CCM basi haraka sana kabla ya uchaguzi wa CCM Mary Nagu awe wa kwanza kuwasihi wajomba zake kuirudisha ILANI YA SERIKALI pale palipowekwa na serikali ya wilaya March 13,2011, na pia yeye awe wa kwanza kama mbunge na mwana CCM wa kweli kuwatimua wajomba zake katika BONDE LA ENDAMANANG AMBALO NI VYANZO VYA MAJI VILIVYOPO KTK HIFADHI YA MLIMA HANANG, AMBAYO PIA ILIKUWA "RECREATIONAL AREA YA
  MAPUMZIKO YA WATOTO WA KIJIJI CHA NANGWA
  ; Siyo shamba la wajomba zake.

  Mary Nagu!!. Kama CCM inataka kuendelea kutawala nchi hii basi
  waonyeshe kwamba wanajali michezo, vyanzo vya maji na misitu yetu ambayo ndiyo rasilimali pekee ambazo tunamiliki.

  4). Pia inawezekana vipi mbunge/Waziri kuagiza Diwani wa kata ya Nangwa akamatwe sambamba na mimi mwanaharakati (Wilhelm Gidabuday), kwa kupigania viwanja vya watoto wetu na vyanzo vya maji ya watanzania?
  Polisi hawakuanza leo mauaji ya wazalendo; Tarehe 1 October, 2011, mimi Gidabuday nilisakwa usiku na mchana ili nipigwe risasi kwa ushirikiano wa Polisi wa Katesh kwa maagizo ya Mbunge, OCD na OCCID.
  Nilisaidiwa na ofisa moja wa Polisi kwa yeye kunipa habari za kiintelejensia kuwa, “order imeshatolewa kuwa Diwani atakamatwa na wewe utapigwa risasi halafu wangesema walinifananisha na jambazi waliyekwa wakimtafuta siku nyingi”
  !!. Mimi nikatoroka lakini Laptop yangu ilichukuliwa ili
  ushahidi wa picha za bonde hilo lipotezwe; mimi kwa hisia zangu
  binafsi nlikuwa nimehifadhi kumbukumbu yangu katika flash.
  HIVYO USHAHIDI WOTE NINAO NA NILISHAWAHI KUFIKISHA KTK VYOMBO FULANI VYA HABARI
  LAKINI SIJUI NI KWA NINI HAWAKUWA WAZALENDO WA KUUELEZA UMMA UNYAMA HUO!!.


  5). Ushahidi wa Video Clips, picha ya kawaida na documents ninao na ikihitajika sasa yoyote nitatoa, ila leo napenda kutoa USHAHIDI WA UHARIBIFU ULIOKINGIWA KIFUA NA MBUNGE WA HANANG (Ilani iliyoharibiwa na kutupwa ).


  Matukio muhimu yalitokea kuhusiana na ubabe huo ndani ya hifadhi ya vyanzo vya maji
  :

  - TAREHE 28/12/2010 DC WA HANANG ALIPOKEA BARUA YANGU ILIYOKUWA NA DETAILS ZOTE (nakala ipo).

  - TAREHE 06/01/2011 DC HANANG ALIKUJA KUJIONEA UHARIBIFU NA KUONYESHA MASIKITIKO MAKUBWA.

  - TAREHE 04/02/2011 DC HANANG ALIHUDHURIA MKUTANO BONDENI NA KUTOA AMRI YA KILIMO KUKOMA MARA MOJA.

  - TAREHE 13/03/2011 ILANI YA SEREKALI ILIWEKWA BONDENI NA HIFADHI (W) WAKIWEMO POLISI KATESH.

  - TAREHE 12/04/2011 AFISA MISITU MKOA ALIKUJA AKIONGOZANA NA WAVAMIZ.

  - TAREHE 14/07/2011 MKUU WA MISITU KANDA ALITEMBELEA BONDE NAKUSHAURI VIKALI KILIMO KIKOME PALE.

  - TAREHE 19/07/2011 WAVAMIZI WALIN'GOA ILANI MBILI ZA SEREKALI NA KUZITUPA

  - TAREHE 20/07/2011 WAVAMIZI WALIKAMATWA KWA MSAADA WA AFISA HIFADHI HANANG (Waliachiwa hadi leo).

  - TAREHE 01/10/2011 NILIFANYIWA "ASSASSINATION ATTEMPT" SABABU NDIYE MSEMAJI MKUBWA WA JAMII YANGU. HATA HIVYO SIKU HIYO M/KITI WA KIJIJI
  ALIKAMATWA KWA SHINIKIZO LA KUNDI HILO LA WAVAMIZI NA WAFAIDIKA WA HONGO ILI KUSHINIKIZA UOGA WATU TUSIENDELEE KUPIGANIA VYANZO HIVYO VYA MAJI. KINACHOSIKITISHA ZAIDI NI MAOFISA HUSIKA KUTOJALI WAKATI WAMEAJIRIWA KUTETEA MASLAHI YA TAIFA!!. (tunaahidi kupambana zaidi
  hadi kieleweke).

  NB: Mary Nagu ni ndugu na rafiki muhimu sana wa wazazi wangu wapendwa, ndiye aliyemsaidia mama yangu wakati mimi na wadogo zangu tunazaliwa; lakini kwa hili sintaacha kusema ukweli kwani tukioneana aibu
  hatutafika!!.

  "
   
 2. Deus F Mallya

  Deus F Mallya Verified User

  #2
  Sep 11, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 707
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Binafsi nazikubali sana harakati za huyu kamanda! Huyu ni Mwana JF popote alipo (We dare to talk Openly)
   
 3. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #3
  Sep 11, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Safi mkuu mwaga mboga na ugali vyote tule. Huyu mama alipata ubunge 2010 kwa tabu sana. Nina hakika 2015 hana kitu Hanang. Namuonea huruma kwa resources anazohangaika kupeleka kule. Mama Nagu hifadhi hizo kwa miaka yako iliyosalia maana 2015 kapa. Anapenda mabavu sana!!! Musculinity!!!!!
   
 4. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #4
  Sep 11, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,723
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160
  acha longo longo kama CCM...if you really dare to talk openly....weka hizo nondo hapa tuone na kujadili.

  we picha/video zote unazo halafu umezibania...wakiku-mwangosi, utaenda kumuonesha nani huko ahera madukani???!!!
   
 5. Deus F Mallya

  Deus F Mallya Verified User

  #5
  Sep 11, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 707
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ahera Madukani???
  You are not Serious Comrade!
   
 6. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #6
  Sep 11, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,593
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Je hii ndiyo taswira halisi ya wabunge wa mawaziri wa JK? Na ni sera ya ccm au aina ya watu walioko ccm.
   
 7. kinya

  kinya JF-Expert Member

  #7
  Sep 11, 2012
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 483
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Huyu kamanda alikomaa na bayi sasa anakomaa na mama yake HAKIKA HAKI HAINA UNDUGU WA RANGI SAFI WILHELM G
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Sep 12, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  hili ni jambo zito sana...
   
 9. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #9
  Sep 12, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Hiyo anaharibu katika Kata na Wilaya yake! Nimeona uzi humu kuwa ana ndoto za URAHISI.....
   
 10. BASHADA

  BASHADA JF-Expert Member

  #10
  Sep 12, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 487
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kwa haraka naona mambo mawili na huenda moja au yote yakawa kweli. Moja ni kwamba vita kati ya sumaye na huyu mama ndo inapamba moto. Pili yawezekana kinachosemwa ndo ukweli.
   
 11. L

  Lamusumo JF-Expert Member

  #11
  Sep 12, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaa huwa hatafuni maneno,he talks openly kwa kweli ila aende mbele zaid kuweka ushahidi mwingine aloweka kapuni mpaka sasa
   
 12. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #12
  Sep 12, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Ni kweli. Mimi nashauri mods wamtafute huyo jamaa awapatie hizo docs maana alipeleka kwenye media wakazikalia. Waweke hapa ndio mahala pake!
   
Loading...