Uchafu kutumbua vigogo Dar

Uchafu kutumbua vigogo Dar

mamayoyo1

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2018
Posts
1,011
Reaction score
1,019
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ametangaza ziara ya kukagua usafi katika jiji hilo na kuwaonya watendaji wa Serikali za Mitaa ambao maeneo yao yatakutwa machafu watapata tabu sana.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa, Makonda aliwaagiza wenyeviti wa serikali za mitaa na kata kuhakikisha wanasimamia usafi katika maeneo yao na yeyote atakayeshindwa atapoteza ajira yake.

“Kuanzia wiki hii na inayokuja nitaanza kutembelea kata zote na mitaa inayokithiri kwa uchafu na kiongozi wa eneo husika kama ameshindwa kusimamia atakuwa hana ajira kwenye mkoa wangu," alisema Makonda.

Alisema jukumu la kusimamia usafi katika mitaa ni la wenyeviti hao, hivyo wanapaswa kuhakikisha taka zimeondolewa na kampuni zilizopewa zabuni za usafi zinafanya kazi yake.

Aidha, alisema jukumu la askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na mgambo wanaopita katika maeneo mbalimbali siyo kufanya usafi bali ni kusimamia makandarasi waliopewa kazi hiyo.

Alisema pia wana jukumu la kushirikiana na wenyeviti wa mitaa kusimamia usafi pamoja na kuwakamata watu wote wanaotupa taka ovyo.

Alieleza wote watakaomatwa na askari hao watafikishwa katika ofisi za serikali za mitaa kwa ajili ya kulipa faini kwa kosa la uchafuzi wa mazingira.

“Askari hawa wamepata mafunzo na wanafanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni bila kumuonea mtu na atakayekamatwa atafikishwa kwa kiongozi wa serikali za mitaa na kata na kulipa faini yake ambayo inajulikana," alisema.

Aidha, Makonda alisema aliondoa zuio la kufunga maduka kila siku ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi, lakini haikumaanisha wenye maduka wasifanye usafi bali wahakikishe maeneo yao ni safi na watakaoshindwa kufanya hivyo mgambo na JKT watawakamata.

“Wewe mfanyabiashara fungua muda wowote, lakini hakikisha eneo lako ni safi na ukishindwa kufanya usafi utakamatwa," alisisitiza Makonda.

Makonda pia aliwataka wafanyabiashara kuweka vifaa vya kuhifadhia taka nje ya maduka yao na kuziagiza manispaa zote za mkoa huo kuweka vifaa hivyo katika maeneo yote ya vituo vya basi ili kuwezesha abiria kutupa taka.

Uzalishaji taka Dar

Mkoa wa Dar es Salaam pekee huzalisha tani 4,600 za taka kila siku, huku ukiwa na uwezo wa kuzoa taka tani 2,300 pekee.

Kadhalika, mkoa huo unatumia Sh. bilioni 10 kila mwaka kwa ajili ya kuzoa taka na kusafisha maeneo yake na dampo pekee linalotumika kutupa taka hizo ni Pugu Kinyamwezi.
Jarida la Forbes liliwahi kuliorodhesha Jiji la Dar es Salaam lenye Manispaa tatu za Ilala, Kinondoni na Temeke kuwa miongoni mwa majiji 12 yanayoongoza kwa uchafu duniani.

Mwaka 2016 Makonda alizindua kampeni ya usafi jijini Dar es Salaam kwa kuwashirikisha watendaji na wenyeviti wa serikali za mitaa, huku akitangaza zawadi nono kwa mtaa utakaoongoza kwa usafi.

Chanzo: IPP Media
 
"Mkoa wangu"

Ila mtukufu raisi anataka mapato yaongezeke na sio porojo
 
Elimu,elimu,elimu, mkuu wa mkoa ana mandatory ya kumfukuza kazi mwenyekiti wa serikali ya mtaa, kwani yeye ndiye anaye wachagua, eti na wenye viti wa kata, sikuizi kuna wenye viti wa kata?
 
Kuhusu suala la uchafu, hakuna jinsi wacha atupige tuuuu faini, Maana hakuna jinsi. Amesahau na mabomba yanayomwaga maji aje atupige tuuuu faini, tumeshachoka na kuleana leana, maji yanamwagika kila kona. Yaani shida kila kona
 
Back
Top Bottom