Ubunifu wa hali ya juu; Ng'ombe aibwa na kuwekwa kwenye Noah

Msigazi Mkulu

JF-Expert Member
Dec 22, 2013
4,137
3,323
Afande Mkoa wa Njombe ni salama kwa saa 12 zilizopita hakuna tishio kubwa kiusalama lililobainika. Aidha, kuna tukio la wizi wa mifugo limeripotiwa ktk wilaya ya Makambako.

Kilichovuta hisia ni mbinu waliyotumia wezi hao kumsafirisha ng'ombe aliyeibiwa toka zizini kwa kutumia gari aina ya Noah. Hapo ndipo umuhimu wa doria na askari wetu kuwa wadadisi unapofanya kazi. Askari waliokuwa doria walishuku gari hiyo na kuisimamisha, lakini dereva hakusimama na akaongeza mwendo. Askari walilifukuza na hatimaye, dereva na watu wengine watatu walilitelekeza na kutokomea porini.

Intel tunajifunza kupitia tukio hili kuwa wahalifu kila uchao wanabuni mbinu mpya kufanikisha uhalifu.

7fb02b4bee634fc94a77b71b7043e6a6.jpg
 
Unashangaa nini?? Daladala la Gongo la Mboto ilivyogongana na lori la ng'ombe pale Tabata kuna ng'ombe alipandishwa bajaji kichwa na mapembe yake kilitokezwa nje na kiwiliwili na mkia wake kimetokeza nje upande wa pili tumbo na kifua ndio ziko kwenye bajaji.

Watu wakawa wanaitafuta Kigogo hiyo.
 
Naona hao watu wa kwenye noah walikimbia tu kuogopa kosa la kubeba ng'ombe ndan ya gari na sio kwamba walikuwa wameba
 
Dah sasa huyo ng'ombe si wangemweka upande wa passenger Sit ? Hapo akipandisha midadi huyo dereva si anawaua
 
Hakuna hata mmoja wa kupongeza askari ila wasingepatika hao wezi lawama zote ni kwa askari
 
Back
Top Bottom