Ubungo yafurika wengi wasitisha safari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubungo yafurika wengi wasitisha safari

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 11, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  NIFAHAMISHE ilishuhudia jana watu wakiwa wamefurika katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani wakihangaika na usafiri wa kurudi mikoani baada ya stendi hiyo kufurika kupita kiasi na kusababisha usafiri kuwa mgumu.
  Ilibainika kuwa jana watu wengi walikuwa wakihitaji usafiri wa kurudi mikoani kutokana na kuwa muda wa likizo kwa wanafunzi ulikuwa umeisha na wafanyakazi wengi walimaliza likizo zao za mwishoni mwa mwaka.

  Hali hiyo iliacha wasafiri hao wakihaha kusaka usafiri wa kuwarudisha mikoani kwa kuwa mabasi yote yalikuwa yamejaa.

  Mabasi mengi yamekuwa yakionekana kupata tenda maalumu za mashule kurudisha wanafunzi mikoani na kusababisha ukosefu wa usafiri na abiria walioweza kusafiri walidai kuwa waliweka oda maalumu wiki moja kabla.

  Baadhi ya abiria walioweza kuzungumza na Nifahamishe.com walisema “usafiri ni shida mno kama unavyoona, tumekuja hapa toka saa 12 asubuhi na sasa inaenda saa 7 hatujapata usafiri, inabidi tuahirishe maana hamna dalili ya usafiri”.

  Huyo alikuwa ni mmoja wa watu waliokuwa wakihitaji usafiri wa kuelekea mkoani Mbeya.
   
 2. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  ni kawaida kipindi hiki ambacho wanafunzi wanarudi mashuleni
   
 3. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  Poleni ubungo. Halafu ile stand kuwa pale inakera. Bora wangeisogeza huko kibaha au kibamba.
   
Loading...