BABA TUPAC
JF-Expert Member
- Sep 30, 2015
- 1,527
- 3,811
Habari zenu wakuu,
Kuanzia Ubungo mataa mpaka Ubungo darajani kumekuwa na watu ambao wao wanajiita tembo.
Watu hawa wamejimilikisha eneo lote lile la Ubungo hivyo wafanyabiashara wote wa Ubungo wanalipia kodi ya lile eneo kwa watu hao wanaojiita tembo.
Na ili upate eneo la kufanyia biashara pale Ubungo basi ni lazima uwalipe tembo pesa si chini ya elfu hamsini, hao tembo wenyewe ni vijana wasio na kazi wala makazi ila wameamua kujichukulia kodi eneo la Ubungo kwakuwa wameona serikali imelala.
Serikali iamke ikawashughulikie tembo wa Ubungo.