Elections 2010 Ubunge: yupi ni sahihi?

Mkeshahoi

JF-Expert Member
Jan 4, 2009
2,469
281
Wadau, niliibabatiza hii kutoka stesheni flani ya redio flani asubuhi hii ktk mishe zangu za kuhemea..!

John Momose Cheyo(UDP): Ubunge ni wa wazee... nawashauri vijana wajenge maisha... waoe... wasomeshe watoto.. baada ya hapo ndio wagimbee ubunge kuja kufanya maamuzi kwani watakuwa wameona mengi..! Bunge likijaa vijana watachapana makonde!!

Ruhanyu(Viti maaalum)... Bunge likijaa vijana litakuwa zuri kwani watakuwa na muda mrefu wa kuongoza!

Paul Kimiti(Mbunge anayestaafu)... Ubunge haujalisi umri wa mtu wala Elimu, wala muda mrefu katika uongozi... Ubunge wamfaa yeyote mwenye uwezo wa kuongoza na bbusara ya kufanya..

Binafsi nahisi kila mmoja wao ana mantiki kwa namna flani.. muhimu mbunge atoke palepale katika jumuiya anayotaka kuiongoza(sio wa kuletewa to Uingereza).. na awe ameonesha kuwa ana uwezo wa kuunganisha nguvu na wananchi ilik kuleta maendeleo... na awe ameelimika(hata kama ni elimu ya msingi).. Umri,Elimu kubwa viwe ni nyongeza tu katika wasifu wake.....!!

Mwaionaje hiyo wadau?!
 
Mi naungana na Mh Kimiti,hatuhitaji umri,jinsi wala kiwango kikubwa cha elimu.Tunahitaji mtu mwenye uwezo wa kuwaunganisha watu ktk kujiletea maendeleo,pia awe na busara na fikra bunifu baasi!
 
Mi naungana na mh Kimiti,yuko sahihi coz hatuhitaji umri wa mtu,jinsia ama ukubwa wa elimu yake.Tunahitaji mtu mwenye uchungu na nchi hii,mzalendo wa kweli,mwenye busara,mwenye nia ya dhati ya kutumikia watanzania,mwenye uwezo wa kuwaunganisha wananchi ktk kujiletea maendeleo!pia asiwe mnafiki,ila awe jasiri.
 
cheyo amefulia yule hata sauti inaelekea kuisha na akikosa ubunge mwaka huu sio siri atakuwa na muda mfupi tu wa kuishi coz amefirisika sana now.
 
Kimiti oyeee! Mapesa ziiiiiiiiiiiiiii!

Huyu mapesa ni tapeli na nawaomba wananchi wa Bariadi wampatie kijana ili kumjibu kwa vitendo. Hafai na hatuhitaji wabunge wa aina yake
 
Back
Top Bottom