'Ubunge' wa Heche Tarime waingia doa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Ubunge' wa Heche Tarime waingia doa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sir.JAPHET, Aug 18, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  [h=2][/h] Ijumaa, Agosti 17, 2012 07:21 Na Mwandishi Wetu, Tarime

  SIKU chache tu baada ya Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema Taifa (BAVICHA), John Heche kutangaza nia ya kugombea ubunge jimboni Tarime katika uchaguzi mkuu 2015, nia hiyo imepokelewa kwa hisia tofauti na wananchi wa jimbo hilo.

  Baadhi wameunga mkono hatua hiyo, huku wengine wakipinga, wakidai huu si muda muafaka kwa kiongozi huyo kutangaza nia hiyo, kwa sababu anaweza kukigawa chama.

  Baadhi ya wananchi hao, ambao wamejitambulisha kuwa ni wanachama wa Chadema, waliliambia MTANZANIA kuwa, Heche ndiyo chimbuko la makundi ambayo yalisababisha Chadema kupoteza jimbo hilo mwaka 2010.

  Walidai kuwa, badala yake kiongozi huyo wa BAVICHA, angetumia nafasi aliyo nayo ya kitaifa kuwatumikia wakazi wa jimbo hilo katika kutatu kero mbalimbali, badala ya kufikiria ubunge kwanza.

  “Bado miaka mitatu kufikia uchaguzi mkuu 2015, haikupaswa kwa mwanachama yeyote kuvuka na kuanza kufikiria kushinda uchaguzi akiwa peke yake bila msaada na kuungwa mkono na zaidi ya theluthi mbili ya wananchama wote jimboni.

  “Sasa leo tunaweza kuhamisha mawazo yetu katika kupambana na umasikini tukaanza kufikiria ubunge,” alisema Samwel Chacha.

  Naye mkazi mmoja wa mji mdogo wa Sirari, Julius Makima, alisema Heche ndiye pekee anayeweza kutetea maslahi ya jimbo hilo na wilaya nzima, kwa kuwa alishathibitisha hilo wakati akiwa diwani wa Kata ya Tarime Mjini kupitia Chadema, katika uchaguzi uliopita.

  Alisema kwa muda mrefu, mwenyekiti huyo wa BAVICHA ameonyesha ukomavu wa kisiasa ambapo mara kadhaa ameonyesha uwezo wa kuunganisha koo zote za kabila la Wakurya na kusaidia kuepusha mapigano ya mara kwa mara ya koo hizo.

  Akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Sokoni katika mji mdogo wa Sirari, mapema wiki hii, Heche aliweka bayana msimamo wake huo wa kugombea ubunge Jimbo la Tarime katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015, endapo chama chake kitampitisha.
   
 2. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Waandishi wetu wa habari na wahariri wap wengi ni makanjanja
   
 3. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #3
  Aug 18, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  huyu c ndiye aliyemlaani shibuda huyu.
   
 4. peri

  peri JF-Expert Member

  #4
  Aug 18, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  yaleyale ya ccm, hakuna jipya.
  Na bado, kadri cdm inavyokuwa, ndio migogoro itaongezeka
  kwasababu migongano ya maslahi itakuwa mingi.
  Hio ndio siasa ilivyo.
   
 5. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #5
  Aug 18, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Kwani cdm kuna mgogoro!? Kuna ubaya gani kutangaza nia ya kugombea uongozi?
   
 6. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #6
  Aug 18, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Heche anakubalika sana ila wakina Benard sanane na kundi lake la wakina Juliana shonza wenye siasa uchwara ndio wanaompiga majungu huyu jamaa tangu kawashinda kwenye uchaguzi wa BAVICHA.
   
 7. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #7
  Aug 18, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,480
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  Mbona hoja yako haina mshiko, kutangaza nia ni hatua muhimu kujua utakubalika au la, mbona Lowasa anafanya kampeni za urais makanisani ulisemi hilo? we kama ni GAMBA achana na CDM kwa hoja zako za kijinga
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Aug 18, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kumbe gazeti lenyewe MTANZANIA?
   
 9. ugolo wa bibi

  ugolo wa bibi JF-Expert Member

  #9
  Aug 18, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 1,231
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  au gazeti la uhuru nini?
   
 10. m

  mharakati JF-Expert Member

  #10
  Aug 18, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  tatizo siyo migogoro ni jinsi wana CDM mnavyotaka kujijichukulia kama chama kisicho na kasoro, chenye umoja wa hali juu unaongozwa na uzalendo uliotukuka n.k haya yanafanya hata vitu vidogo kuchukulia kama ni vikubwa na walio nje ya chama au wapinzani wenu ccm.
   
 11. y

  yaya JF-Expert Member

  #11
  Aug 18, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu mharakati, nimeshindwa kukuelewa, mimi siko kokote kiitikadi na nisingependa kueleza kwa nini. Lakini, kwani si kweli kwamba CDM wana umoja na ni wazalendo?
  Ni nani aliyewataja mafisadi wa TZ kule Mwembeyanga?
  Ni nani aliyeuweka wazi wizi wa EPA?
  Ni nani anayetaka kufichua waliojilimbikizia mabilioni ya pesa huko Uswisi iwapo serikali ya TZ haitawataja?
  Huko kutokufumbia macho maovu yanayoiumiza nchi yako TZ, na kutokulindana ndio uzalendo wenyewe.

  Suala la mtu kutaka kugombea au kutangaza nia ya kugombea ubunge ni kitu kidogo sana na wala hakiwezi kugawa wanachama.
  Na ndiyo maana wagombea huwa wengi kabla ya kupitishwa na vyama vyao kulingana na vigezo walivyojiwekea.
   
 12. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #12
  Aug 18, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Mkuu, sio kwamba cdm ni malaika. Kwakuwa sisi kama wananchi tunapewa nafasi ya kuchagua, basi tunaangalia afadhali! Kwa sasa afadhali cdm kuliko vyama vingine. Ndio maana waliochagua cdm wanajaribu kuelezea uafadhali wake ukilinganisha na vyama vingine. Wale waliochagua vingine nao wanajaribu kufanya hivyohivyo. Tofauti yetu ni kwamba, pale wanapoonesha kwamba cdm ni afadhali, wengine wanaona kama ni kuwalinganisha na malaika! Lakini ukweli unabaki palepale, kwamba kwa sasa cdm ni afadhali sana kuliko vyama vingine vyote hapa nchini!
   
 13. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #13
  Aug 18, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  umekosa cha kuandika mbona hiyo stori imekaa poa ....endapo chama chake kitampitisha.......cdm sio malaika kwamba hawatafanya makosa lakini ccm wameshaonesha wazi hawana dhamira ya kuwaongoza watz mabaya ni mengi mno kwao
   
 14. m

  mharakati JF-Expert Member

  #14
  Aug 18, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145

  nashukuru kaka uafadhali lakini siyo umalaika..wewe unaelewa wenzako wengine ni shida tupu kuelewa ili au ni maksudi tu nashindwa kuelewa.
   
 15. a

  afwe JF-Expert Member

  #15
  Aug 18, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 4,087
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Kwa nini ulitegemea akubalike na kila mkazi wa Tarime? Ni lazima wapo watakao kubaliana na yeye na pia watakaompinga. Huu sio wakati wa ku-assume tu kuwa akitangaza nia basi ataungwa mkono na kila mtu. Kwa kuwa mara nyingi kwenye siasa ni muhimu usome alama za nyakati, huenda ni kweli kwamba haikuwa sahihi kwake kungaza sasa hivi ni yake.
   
 16. t

  thatha JF-Expert Member

  #16
  Aug 18, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  kwa heche sawa lakini kwa zitto ni dhambi kubwa
   
 17. t

  thatha JF-Expert Member

  #17
  Aug 18, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Vipi kuhusu kamanda mwita mwikabe ambaye aligombea mwaka 2010,nadhani angeachiwa arudie tena
   
 18. t

  thatha JF-Expert Member

  #18
  Aug 18, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  hapa tunamjadili heche na ubunge,kama unataka kuongelea mabaya ya ccm anzisha thred yake.
   
 19. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #19
  Aug 18, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Mambo ya kutangaza nia kwa kiongozi wa kitaifa kwa sasa si busara hata kidogo!
  Huu ni muda wa kujenga chama kwa kutumikia wananchi.
   
 20. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #20
  Aug 18, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Kilaza kamuuuilize Mbowe kwanini alikemea kutangaza nia za kugombea urais na ubunge siku walipokuwa wanafanya usanii wa kusafisha fedha yao chafu..?
   
Loading...