johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 94,160
- 164,598
Tuliambiwa na mwenezi wa CCM kuwa chama chao kilikuwa na waombaji zaidi ya 400 na baada ya mchujo mkali wameteua wagombea 12. Sasa kama wale tuliowashuhudia ndio the best kwenye chama chenye zaidi ya wanachama milioni 8 basi kuna shida kubwa.
Na niwashauri tu CCM wakati mwingine malizeni kazi hukohuko kwenye chama msilitegemee sana bunge.Teueni kabisa majina yenu 6 kwa kufata utamaduni wa chama unavyotaka mfano jinsia, muungano na hata uwiano wa kidini na uwakilishi wa walemavu.
Katika ushindani wa kifalsafa Makongoro Nyerere ni kete muhimu sana Eala hasa tunapolilia utengamano wa kibiashara na Uganda plus Rwanda, usitegemee mtu kama kibaji, Jah people au msukuma kulielewa hili kwa haraka.Matokeo yake ndio haya tunayoshuhudia kila uchaguzi ccm inashuka viwango kiuteuzi na kiukweli tusitegemee sana mapya kwenye hii team.
Bora Chadema na CUF ya maalim Seif, walau hawa walikuwa na maono na kwa kuitakia mema nchi hii waliteua na kuchagua kabisa kwa idadi ileile inayotakiwa na kuliachia bunge kazi ya kuwapitisha.Angalia wasifu wa Taslima na Masha lakini pia Wenje ambae kwa miaka 5 amekuwa waziri kivuli wa ushirikiano wa kimataifa.
Cha kushangaza bunge limewakataa lakini limemkataa hata Makongoro aliyewaambia alipambana usiku na mchana kuhakikisha bomba la mafuta la Uganda lililokuwa lipite Kenya linapita Tanzania. Baraka nyingine tunazifukuza wenyewe.
Ahsante!