Ubunge wa CCM, CUF utata mtupu - Taarifa za NEC zaonyesha CHADEMA imeshinda kwa 83% | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubunge wa CCM, CUF utata mtupu - Taarifa za NEC zaonyesha CHADEMA imeshinda kwa 83%

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jan 13, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Mary Victoria - Raia Mwema


  [​IMG]


  Mwenyekiti na Mkurugenzi wa NEC uchaguzi wa 2010


  Taarifa za NEC zaonyesha CHADEMA imeshinda kwa 83%


  TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeingia katika kashfa mpya baada ya kuwapo kwa taarifa zenye utata kuhusu matokeo ya kura za ubunge katika Mkoa wa Kaskazini Pemba, ambako Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeshinda ubunge katika moja ya majimboni mkoani humo, kwa asilimia 83.17, Raia Mwema, imebaini.

  Matokeo hayo yanayokipa CHADEMA ushindi mkubwa na wa kipekee katika siasa za Zanzibar ambazo kwa miongo zaidi ya miwili zimekuwa zikitawaliwa na vyama vya CCM na CUF, yamekutwa na gazeti hili katika tovuti ya NEC.

  Kwa mujiibu wa matokeo hayo kwenye tovuti, CHADEMA inatajwa kushinda katika Jimbo lililotambulishwa kwa jina la Tumbe. Ushindi huo wa CHADEMA unafuatiwa kwa mbali na Chama cha Mapinduzi, ambacho kimeambuliwa asilimia 9.52.


  Mgombea wa CHADEMA aliyeshinda ubunge huo ambao hata hivyo, jimbo husika halionekani katika orodha ya majimbo yanayotambuliwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Hamad Omar Kombo.


  Kombo katika takwimu hizo kwenye tovuti anatajwa kushinda ubunge kwa kupata kura 5,633, ambayo ni asilimia 83.17 ya kura zote, akifuatiwa na mgombea wa CCM, Rashid Ali Abdallah, wa Chama cha Wananchi (CUF) aliyepata kura 97, sawa na asilimia 1.43.


  Mgombea wa NCCR-Mageuzi, Abdalla Yussuf Hassan, ameshika nafasi ya nne kwa kupata kura 89, ambazo ni sawa na asilimia 1.31.


  Katika Jimbo hilo linalotikisa umakini wa NEC na uhalali wa matokeo yaliyokwishatangazwa katika Uchaguzi wa Mkuu wa mwaka 2010, kura zilizoaharibika zinatajwa kuwa ni 309, ambazo ni sawa na asilimia 4.56.


  Takwimu hizo kwa mujibu wa maofisa wa NEC walioziingiza kwenye tovuti hiyo zinabainisha kuwa jumla ya kura zilizopigwa ni 6,773, sawa na asilimia100.


  Majimbo mengine kwenye orodha hiyo katika mkoa huo wa Kaskazini Pemba ni Micheweni ambalo mgombea wa CUF, Khatibu Said Haji, ameshinda kwa kupata kura 5,268, sawa na asilimia 82.2, akifuatiwa na mgombea wa CCM, Salum Nafoo Omar kwa kura 715 sawa na asilimia 11.16.


  Mgombea wa CHADEMA, Hamadi Salumu Khamisi, alipata kura 125, sawa na asilimia 1.95, wakati Sholo Ali Salum wa NCCR-Mageuzi, alipata kura 86, sawa na asilimia 1.34, huku kura zilizoharibika zikiwa 215, sawa na asilimia 3.35, na jumla ya kura zote ni 6,409, sawa na asilimia 100.


  Hata hivyo, mbali na gazeti hili kubaini kuwapo kwa utata katika Jimbo linalotajwa kuwa CHADEMA imeshinda ambalo pia halimo kwenye orodha ya majimbo yenye wabunge wanaotambuliwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pia imebainika kuwa mgombea anayeoneshwa kushinda katika Jimbo la Mtambwe, si yule aliyeapishwa bungeni, mjini Dodoma.


  Tovuti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaonesha kuwa katika Jimbo hilo la Mtambwe, Khamis Seif Ali wa Chama cha Mapinduzi ndiye mshindi kwa asilimia 84.05, lakini katika orodha ya wabunge walioapishwa bungeni, Mbunge wa CUF, Said Suleiman Saidi, ndiye aliyeapishwa na kwa sasa ndiye mbunge.


  Kwa mujibu wa tovuti, Khamis Seif Ali wa CCM alishinda kwa kupata kura 4,849, ushindi ambao kwa kuzingatia tambo za siku nyingi za CCM, ni wa kishindo ukiwa ni wa asilimia 84.05. Said Suleiman Said wa CUF, yeye anatajwa kwenye tovuti hiyo kuwa ameambulia kura 346, sawa na asilimia sita, lakini hata hivyo, huyu ndiye aliyeapishwa kuwa mbunge na hadi sasa anaendelea na wadhifa huo.


  Jumla ya kura zilizopigwa ni 5,769, ambazo ni sawa na asilimia 100 ya waliojiandikisha lakini ni kura 574, ndizo zilizoharibika ambazo ni sawa na asilimia 9.95.


  Juhudi za kumpata Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva, hazikuzaa matunda hadi tunakwenda mitamboni kwa ajili ya uchapaji.

  Juhudi hizo zinaendelea.


  Matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 yamekuwa na utata mkubwa katika baadhi ya maeneo, huku NEC ikichukua muda mrefu kuyaweka matokeo hayo ya jumla katika tovuti yake.


  Kwa upande wa matokeo ya urais yaliyompa ushindi Rais Jakaya Kikwete kuweza kuendelea na awamu ya mwisho ya kuongoza nchi, yalipingwa na aliyekuwa mgombea urais wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa, ambaye pia hakuhudhuria sherehe za kutangazwa kwa matokeo hayo.


  Katika hatua nyingine, taarifa kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, zinabainisha kuwa mpaka sasa, ukaguzi wa hesabu za vyama vya siasa kwa mujibu wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi, haujaanza rasmi.


  CAG Utouh alithibitisha kuwa bado ukaguzi huo wa hesabu za vyama hivyo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, pamoja na hesabu za uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Igunga, mkoani Tabora, haujaanza.


  "Kwa kweli siwezi kusema ni lini hasa tutakamilisha. Hili ni jambo jipya kisheria na katika mchakato wa utekezaji wake niseme tu kwamba kwa sasa tumeanza kufanya uchambuzi wa nyaraka mbalimbali kwanza," alisema Utouh.


  Lakini katika mazungumzo yake na Raia Mwema ofisini kwake mwanzoni mwa wiki hii, Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, aliweka bayana kwamba vyama vya siasa 18 vimekwishawasilisha taarifa za hesabu zao za Uchaguzi Mkuu wa 2010 ofisini kwake na kwamba ofisi yake imewasilisha taarifa hizo kwa CAG kwa ajili ya ukaguzi.


  "Vyama 18 vimekwishaleta taarifa na CAG nadhani amekwishaanza kukagua hesabu hizo, tusubiri taarifa kutoka kwake ili tujue walitumia kiasi gani cha fedha," alisema Tendwa na kuongeza:


  "Februari mwaka huu, vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi mdogo wa ubunge Igunga, vitatakiwa kuwasilisha marejesho ya matumizi ya gharama zao katika uchaguzi huo."









   
 2. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mmh! CDM ishinde pemba? si zani!
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,485
  Likes Received: 19,879
  Trophy Points: 280
  mbona sijaelew kitu?
   
 4. Kibona

  Kibona JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 1,021
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Hudhani nini! wakati hayo ndo matokeo ya NEC?
   
 5. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #5
  Jan 13, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Matokeo ya uchakachuaji; hadi unapitiliza ama unajisahau!
   
 6. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Pamoja na kuwa mimi ni muumini wa CDM lakini kwa hili la kushinda pemba mmh!
  Nahisi computer za NEC zimekosea jawabu....atlist wangesema unguja kidogo ningeamini lakini si pemba
   
 7. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2012
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Raia mwema wanautani na wapemba nini?
   
 8. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #8
  Jan 13, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Si kweli
   
 9. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hizi ni error ndogo ndogo katika swala zima la uchakachuaji, msi-mind sana wananchi
   
 10. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #10
  Jan 13, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  yaaani mijitu mijizi mpaka inakosea kuandika minamba ya wizi.....
   
Loading...