Ubovu wa mihimili yote mitatu ya serikali

Ubovu wa mihimili yote mitatu ya serikali

rhoda ryoba

Member
Joined
Apr 19, 2016
Posts
88
Reaction score
168
Hapo mwanzo nilidhani mhimili wa bunge ndio mbovu kutokana na kushindwa kuisimamia serikali kama asemavyo CAG mstaafu kuwa bunge letu ni dhaifu, taarifa za CAG kila mwaka zinathibitisha kuwa hatuna bunge makini ndio maana mambo yanaenda hovyo hovyo,

Bunge hili limeshindwa kutunga sheria makini za kulinda rasilimali za nchi ,kazi kubwa ya bunge imekuwa ni kumsifia Rais kwa kila kitu ili wabunge wapate upendeleo rejea kauli ya rais wakati akimuapisha mkuu wa mkoa wa mbeya alimwambia ahakikishe Tullia anarudi Kwa kuwa ndio amekuwa chawa pro max wa Rais.

Mhimili wa serikali kuu(mawizara na Taasis zake) hali ni mbaya sana kwenye kuhudumia wananchi na kutekeleza mipango ya nchi na bajeti huku pesa za umma zikitafunwa bila huduma.

Nilidhani mihimili hiyo ni mibovu, lakini nilipoanza kufatilia mhimili wa mahakama nimegundua ndio haufai kuliko yote, mfumo mzima wa hakijinai umeoza na unaongozwa kwa maelekezo, urasimu uliopo mahakama ni wa hali ya juu, kimsingi ni ngumu sana kupata haki kwenye mahakama za Tanzania.

Nadhani kesi kubwa za nchi inapaswa zisiendeshwe na WaTanzania maana wameoza wananuka hawafai, kama unaweza kumaliza jambo nje ya mfumo wa haki jinai bora ulimalize tu, mfano mimi kesi zangu huwa sipeleki polisi wala mahakamani, ninao mfumo binafsi wa haki jinai. Poleni wote ambao mihimili hii inawatesa kimsingi tupo kwenye nchi ya mfalme juha
 
Back
Top Bottom