Ubovu wa daraja la Yombo Dovya ni simanzi

Ubovu wa daraja la Yombo Dovya ni simanzi

Atukuzwaye

Senior Member
Joined
Oct 5, 2026
Posts
137
Reaction score
158
Unaweza kudhani wanaotembea kwa mwendo huu ni watu wenye ulemavu, lakini hapana. Hawa Ni wananchi wazima kabisa wanaolazimika kutembea kwa tahadhari kutokana na ubovu wa Daraja la Kwa Muki, lililopo Yombo Dovya, Temeke, jijini Dar es Salaam.

Kwa zaidi ya miaka mitano tangu daraja hilo lianguke, wananchi wameendelea kukabiliwa na changamoto ya kuvuka, huku hofu ikiongezeka kuelekea kipindi cha mvua.

Mwenyekiti wa Mtaa huo, Rashid Mbanga, amesema changamoto hiyo ni ya muda mrefu na amekuwa akifanya jitihada kuhakikisha daraja hilo linarekebishwa. “Ninapata mashaka kwa sababu tunaelekea kwenye kipindi cha El Niño, na hali ya pale ni mbaya,” amesema Mbanga.

Wananchi sasa wanasubiri hatua za kudumu kutoka kwa mamlaka husika ili kurekebisha daraja hilo na kuondoa adha wanayopitia. Hii hali ni hatarishi kwa jamii aisee kwasababu mtaani kuwa watoto, wazee na walemavu pia, na kwa jinsi daraja hili linavyoonekana, hii ni hatari kubwa sana.

 
Ukiliangalia hilo daraja vizuri,linaonekana wazi kabisa kua katika ujenzi wake,hazikufuatwa Engineering requirement katika ujenzi wake,inaweza kua ni kwenye technical design au construction procedure katika ujenzi wake toka mwanzo.
 
Back
Top Bottom