Ubovu wa CT scanner MNH-Maoni ya mtaalamu!

meningitis

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2010
Posts
8,464
Reaction score
4,828
Ukweli usemwe na wakuwajibika na kuwajibishwa na wawajibike kwa haki!

Niseme tu sipingi na kamwe sitapinga kasi ya Magufuli katika kufanya maamuzi...maamuzi yote magumu lazima yawe na setbacks na regrets lakini yanaheshimika kuwa ni maamuzi magumu.

Kiongozi ni yule anayechukua maamuzi hata kama atakosea au kuumiza wengi.

Hii ndio kasi inayohitajika kwenye mfumo mbovu unaoficha maovu yake chini ya mwamvuli wa 'utaratibu'

Ubovu wa CT SCANNER NA MRI Muhimbili ni rflection ya tatizo kubwa na la msingi katika hospitali nyingi au zote nchini.

Kwa uelewa wangu hadi jana ni kwamba wizara ya afya iliingia mkataba na kampuni flani (sitaitaja jina) kufanya matengenezo ya vifaa tiba aina ya CT scan na X rays na Ultra sounds na vinginevyo.

mkataba huu ulifanyikia huko huko wizarani.

Mojawapo ya kipengele cha mkataba ni kwamba vifaa hivi haviruhusiwi kutengenezwa na mwingine yoyote zaidi ya yule aliyepewa tenda huko wizarani.

Yoyote au taasisi yoyote itakayokiuka kipengele hiko kwa kutengeneza vifaa hivyo na kwa bahati mbaya vikafa kabisa basi itakuwa imekula kwake.

Kipengele hiki kinaweza kuwa sababu ya uongozi wa MNH au hospitali nyingi kutozigusa vifaa hivi kwa matengenezo ya kawaida au dharura.

Tetesi zilizopo ni kuwa malipo ya huyu mzabuni hayakwenda sawa kwa muda mrefu kwa hiyo walivisusa au kuvitekekeza vifaa hivi .

Kwa hiyo kwa mkurugenzi anayeamini katika 'taratibu' angeweza kuendelea kusubiri wizara na mzabuni wamalizane ili mashine hizo zije kutengenezwa.

Ni common practise kuwa viongozi wa mahospitali wakijaribu kuwasilisha tatizo hili wizarani au kwa mzabuni kupewa majibu ya tunashughulikia...

KOSA LA DIRECTOR WA MNH!

Kama kiongozi wa 'zahanati' kuu alitakiwa kulichukulia tatizo la CT SCAN NA MRI kutokufanya kazi kuwa ni tatizo kuu na la kutisha na linalohitaji special attention

Alitakiwa kutokulala,kuumizwa na kulihangaikia toka siku ya kwanza.

Alotakiwa kulipresent kwa wadau wote ikibidi hata kulifikisha Ikulu na kulielezea umuhimu wake kama ukosefu wa umeme nchini.sidhani kama alifanya enough katika hili...pia sidhani kama wakuu wengi wa hospitali nyingi za serikali wana hulka hii ya kuyaelezea matatizo ya hospitali zao.
Hilo ndilo kosa pekee kama hukumu yake ilibase katika ukosefu wa huduma za ct scan na MRI!!

WANAOTAKIWA KUWAJIBISHWA KWENYE SAKATA HILI...ukiacha ditector wa MNH!

Kama nilivyoekeza hapo juu...mkataba huu wa maintanance uliingiwa juu kwa juu huko huko wizarani.

Kwa hiyo wapo wengi tu ambao wanaotakiwa kuwajibishwa...

Kuna Director wa Diagnostics yaani anayehusika na mambo ya vipimo hospitalini.

Kuna watu wa procurement aka wazee wa michakato na 10%...

Kuna watu wa hazina waliopeleka B3 jana na sio miezi miwili iliyopita.

Kuna wahasibu wa Muhimbili nikiamini kuwa kuna makusanyo ya fedha za kuweza kutengeneza hiyo mashine.

Kuna maafisa wa procurement hapo muhimbili na wizarani ambao mara nyingi hawajui umuhimu wa vifaa hivi kufanya kazi.

Kuna bodi ya Muhimbili kwa bahati nzuri ilikuwa imemaliza muda wake.

Wako watumishi wengine wadogo wadogo ambao sitawataja.

WAY FOWARD NI NINI?

Bado nakubali hii nginjanginja ya Magufuli ili watumishi wa umma waamke!

Viongozi waliopewa dhamana waelewe kuwa hakuna tatizo dogo au kubwa au la mazoea.

Sheria za manunuzi zilizopo zipitiwe na kuenenda kulingana na sekta mbalimbali...kuna sekta zilizo na uharaka au dharura kwa muda wote.

Rais awawajibishe watendaji wa wizara sio wa taasisi pekee.

Wanasiasa na bodi mbalimbali zifanye kazi kutikana na ushauri wa wataalamu.

Maamuzi mbalimbali yatoke kwa wataalamu walioko 'site' na sio wapigaji wa wizarani.

Wananchi waendelee kupigia kelele huduma mbovu sio tu kwa kuilenga taasisi bali hata executives kwa maana ya wizara.

MWISHO:

Tumekubaliana na Slogan ya [URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=HAPAKAZITU]#HAPAKAZITU [/URL] basi tukubaliane kuumizana sana tu mpaka pake tutakapokaa sawa kama taifa.

WASALAAM...HII SIO SIASA NI USHAURI WA [URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=HAPAKAZITU]#HAPAKAZITU [/URL]
 
Lakini kama utaona ziara ya magufuli hajatoa uamuzi pale pale hospital, na alikuwa akiuliza maswali pia, mbona hayakuja majibu kama haya? Na wao wanamjua alivyo!! Kwangu mimi naona ni utetezi tu, kuna uzembe mkubwa wizara nzima sio muhimbili tu
 
Mkuu huu sio utetezi bali ni maoni ya maboresho!
 
Pale wizarani kuna watu wanatakiwa kushughulikiwa kwa uhakika,maana kuna madudu mengi wanafanya ili kujinufaisha wao binafsi
 
Ikiwa hilo la wizara kujichukulia madaraka ni kweli basi ni tatizo la msingi. Ushauri ni wizara kuheshimu mamlaka zilizo chini yao na kuwaacha watende majukumu yao kwa uhuru kwa mujibu wa sheria zao, yaani, eyes on hands off.
 
Mkuu hilo ndio tatizo la msingi
 
Badilisha mfumo, badilisha timu inayoendesha huo mfumo kama haifanyi kazi vizuri - siyo mtu mmoja mmoja. Hiki ndicho Magufuli anapaswa kufanya. Hii kuibukia shirika moja moja, then kutimua bosi mmoja/wawili wa shrika wakati sote tunafahamu kuwa maamuzi ya serikali yamekuwa yanaenda kwa ngazi huku yakihusisha wengi na teuzi nyingi za hao 'wabovu' zikianzia hukohuko ikulu, is a political stunt to say the least and won't get us very far. Naunga mkono nia ya Magufuli lakini naona kama strategy bado ni tatizo.
 
  • Thanks
Reactions: 999
Raisi wetu ana nia nzuri na taifa hili lakini naona kwamba kuna baadhi ya watendaji serikalini watamkwamisha,
na sipati picha Wazili wa afya atakayemchagua kama ataendana na kasi ya Raisi wetu.
 
Raisi wetu ana nia nzuri na taifa hili lakini naona kwamba kuna baadhi ya watendaji serikalini watamkwamisha kama na sipati picha Wazili wa afya atakayemchagua kama ataendana na kasi ya Raisi wetu.

Waziri wa afya atakayemteua ni lazima awe na kasi na mwenye kuyafahamu matatizo katika msingi wake!

Akoenenda kisiasa tutamuumbua tu.
 
umenikumbusha 2013 wakati nipo MNH hakuna diclofenac twaambia wagonjwa wakanunue nje.. hali ile mi ilinikera sababu wagonjwa wa idara yangu wanahitaji sana dawa za maumivu.. nkamuuliza intern pharmasist mmoja akanambia ... muhimbili inatakiwa ichukue dawa kwa supplier flani nimesahahu nadhani ni MSD na si kwengineko na kama hawana ndio imekula kwetu , na pia kulikuwa na Tatizo hospitali inadaiwa... supplier amesitisha zoezi la kuleta dawa...

hii mikataba huwa watu wanaingia huku wakipewa pesa ndio maana wanaingia mikataba mibovu!!,....

mwisho wa siku tunakuja kupata lawama madactari tunabania dawa,, tuna maduka nje ..... makatili mgonjwa ana maumivu hatuwapi dawa.... et cal

kwa utawala huu wa awamu ya 5 mambo yatabadilika i hope Insha Allah
 
mkuu na mganga mkuu pia!! huyu aliyepo ni mpole sana alafu pia sidhani kama ni MD ... nadhani ni "AMO"
 
Namshukuru rais kwa maamuzi yake magumu. Ni kweli hapo ni kuokoa maisha ya watu Mungu akubariki baba. Ila ningependa sana angesikiliza Mkurugenzi huyo wa muhimbili aliyefukuzwa na wizara wanasemaje kuhusu ubovu wa hizo mashine? Kwa nini waadhibiwe kumbe tatizo lilikuwa hazina kutoa b3 ambazo zilitoka on time. Pia, nashauri huu mziki wa JPM uendelee kwa nguvu ila ashughulikiwe mfumo zaidi kuliko watu. Yaani washauri wake wamuelezee utaratibu ukoje? basi wote ambayo wapo kwenye huo utaratibu watimuliwe. Yaani kama kitu kilitakiwa kipite A, B, C, na D halafu kikakwamwa basi kila hatua wahusika watimuliwe na itangazwe ili watu wajue kuondoa mifumo mibovu. mfano kuna A-Muhimbili, B-Wizara ya afya, C-Bodi, D-Hazina ambaye hakufanya kazi yake kwenye huo mzunguko rungu limuangukie.
 
Mimi naona umeandika kama yanayojiri na unataka watu walipe ni kama unatoa habari ya ukweli na ushauri kutaka hao wawajibishwe

Kwa mimi hao wa wizarani ndio kwenye tatizo kubwa sana na huyo mkurugenzi wa muhimbili ni yeye tu aliyefaa

Hao wengine wakipata mahitaji na mshine zikilipiwa sidhani kama kutakuwa na matatizo yaliyotokea kwa sasa labda yawe nje ya uwezo wa binadamu.
 
mkuu na mganga mkuu pia!! huyu aliyepo ni mpole sana alafu pia sidhani kama ni MD ... nadhani ni "AMO"
Mganga mkuu wa sasa ni mtaalamu lakini hajakaa wodini mda mrefu.

mganga mkuu ni Dr Bakari
 
ahh professor bakari ni jembe !.... nilidhani bado yupo yule wa zamani...

Ni jembe lakini sina uhakika kama anaujua huu mfumo mbovu uliopo.

Cha msingi ni lazima awe mlalamikaji kwa mustakabali wa madaktari
 
umenikumbusha 2013 wakati nipo MNH hakuna diclofenac twaambia wagonjwa wakanunue nje.. hali ile mi ilinikera sababu wagonjwa wa idara yangu wanahitaji sana dawa za maumivu.. nkamuuliza intern pharmasist mmoja akanambia ... muhimbili inatakiwa ichukue dawa kwa supplier flani nimesahahu nadhani ni MSD na si kwengineko na kama hawana ndio imekula kwetu , na pia kulikuwa na Tatizo hospitali inadaiwa... supplier amesitisha zoezi la kuleta dawa...

hii mikataba huwa watu wanaingia huku wakipewa pesa ndio maana wanaingia mikataba mibovu!!,....

mwisho wa siku tunakuja kupata lawama madactari tunabania dawa,, tuna maduka nje ..... makatili mgonjwa ana maumivu hatuwapi dawa.... et cal

kwa utawala huu wa awamu ya 5 mambo yatabadilika i hope Insha Allah

Mkuu..huu ndio ukweli katika sekta hii ya afya ct scan na MRI ni mifano tu ya tatizo kubwa katika sekta hii.
 
Ukweli usemwe na wakuwajibika na kuwajibishwa na wawajibike kwa haki!

Niseme tu sipingi na kamwe sitapinga kasi ya Magufuli katika kufanya maamuzi...maamuzi yote magumu lazima yawe na setbacks na regrets lakini yanaheshimika kuwa ni maamuzi magumu.

Kiongozi ni yule anayechukua maamuzi hata kama atakosea au kuumiza wengi.

Hii ndio kasi inayohitajika kwenye mfumo mbovu unaoficha maovu yake chini ya mwamvuli wa 'utaratibu'

Ubovu wa CT SCANNER NA MRI Muhimbili ni rflection ya tatizo kubwa na la msingi katika hospitali nyingi au zote nchini.

Kwa uelewa wangu hadi jana ni kwamba wizara ya afya iliingia mkataba na kampuni flani (sitaitaja jina) kufanya matengenezo ya vifaa tiba aina ya CT scan na X rays na Ultra sounds na vinginevyo.

mkataba huu ulifanyikia huko huko wizarani.

Mojawapo ya kipengele cha mkataba ni kwamba vifaa hivi haviruhusiwi kutengenezwa na mwingine yoyote zaidi ya yule aliyepewa tenda huko wizarani.

Yoyote au taasisi yoyote itakayokiuka kipengele hiko kwa kutengeneza vifaa hivyo na kwa bahati mbaya vikafa kabisa basi itakuwa imekula kwake.

Kipengele hiki kinaweza kuwa sababu ya uongozi wa MNH au hospitali nyingi kutozigusa vifaa hivi kwa matengenezo ya kawaida au dharura.

Tetesi zilizopo ni kuwa malipo ya huyu mzabuni hayakwenda sawa kwa muda mrefu kwa hiyo walivisusa au kuvitekekeza vifaa hivi .

Kwa hiyo kwa mkurugenzi anayeamini katika 'taratibu' angeweza kuendelea kusubiri wizara na mzabuni wamalizane ili mashine hizo zije kutengenezwa.

Ni common practise kuwa viongozi wa mahospitali wakijaribu kuwasilisha tatizo hili wizarani au kwa mzabuni kupewa majibu ya tunashughulikia...

KOSA LA DIRECTOR WA MNH!

Kama kiongozi wa 'zahanati' kuu alitakiwa kulichukulia tatizo la CT SCAN NA MRI kutokufanya kazi kuwa ni tatizo kuu na la kutisha na linalohitaji special attention

Alitakiwa kutokulala,kuumizwa na kulihangaikia toka siku ya kwanza.

Alotakiwa kulipresent kwa wadau wote ikibidi hata kulifikisha Ikulu na kulielezea umuhimu wake kama ukosefu wa umeme nchini.sidhani kama alifanya enough katika hili...pia sidhani kama wakuu wengi wa hospitali nyingi za serikali wana hulka hii ya kuyaelezea matatizo ya hospitali zao.
Hilo ndilo kosa pekee kama hukumu yake ilibase katika ukosefu wa huduma za ct scan na MRI!!

WANAOTAKIWA KUWAJIBISHWA KWENYE SAKATA HILI...ukiacha ditector wa MNH!

Kama nilivyoekeza hapo juu...mkataba huu wa maintanance uliingiwa juu kwa juu huko huko wizarani.

Kwa hiyo wapo wengi tu ambao wanaotakiwa kuwajibishwa...

Kuna Director wa Diagnostics yaani anayehusika na mambo ya vipimo hospitalini.

Kuna watu wa procurement aka wazee wa michakato na 10%...

Kuna watu wa hazina waliopeleka B3 jana na sio miezi miwili iliyopita.

Kuna wahasibu wa Muhimbili nikiamini kuwa kuna makusanyo ya fedha za kuweza kutengeneza hiyo mashine.

Kuna maafisa wa procurement hapo muhimbili na wizarani ambao mara nyingi hawajui umuhimu wa vifaa hivi kufanya kazi.

Kuna bodi ya Muhimbili kwa bahati nzuri ilikuwa imemaliza muda wake.

Wako watumishi wengine wadogo wadogo ambao sitawataja.

WAY FOWARD NI NINI?

Bado nakubali hii nginjanginja ya Magufuli ili watumishi wa umma waamke!

Viongozi waliopewa dhamana waelewe kuwa hakuna tatizo dogo au kubwa au la mazoea.

Sheria za manunuzi zilizopo zipitiwe na kuenenda kulingana na sekta mbalimbali...kuna sekta zilizo na uharaka au dharura kwa muda wote.

Rais awawajibishe watendaji wa wizara sio wa taasisi pekee.

Wanasiasa na bodi mbalimbali zifanye kazi kutikana na ushauri wa wataalamu.

Maamuzi mbalimbali yatoke kwa wataalamu walioko 'site' na sio wapigaji wa wizarani.

Wananchi waendelee kupigia kelele huduma mbovu sio tu kwa kuilenga taasisi bali hata executives kwa maana ya wizara.

MWISHO:

Tumekubaliana na Slogan ya #HAPAKAZITU basi tukubaliane kuumizana sana tu mpaka pake tutakapokaa sawa kama taifa.

WASALAAM...HII SIO SIASA NI USHAURI WA #HAPAKAZITU

Umechelewa sana kumfundisha kazi Raisi, Mkuu Magufuli keshapita... anaendelea tu.... pitia vivuli vyote... Huyu Jamaa watu walishakuwa na habari naye ndio maana walihuzunika sana alipochaguliwa..... mwache apige kazi alisema hato waangusha.... Ile Sera ya wengi wape anaitimiza na ni bora afe mmoja wengi wapone...
 
Yah ni bora mmoja afe ili wengi wapone!

Sikatai bali huyo mmoja asiwe wa chini tu bali hata yule wa juu.
 
Mganga mkuu wa sasa ni mtaalamu lakini hajakaa wodini mda mrefu.

mganga mkuu ni Dr Bakari

Huyu mganga mkuu hata huwezi jua hata kazi yake nini unaweza kaa hata miezi sita hata kusikia kwenye media yoyote kwamba mganga mkuu wa serikali kafanya hiki na kile nafikiri wengine hawa wanafanya kazi kwa mazoea.
Hawa ndio magufuri anatakiwa kuwaondoa ili kuleta wapya watakaokuwa bize kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya.

Uongozi huu wa awamu ya tano ukifanikwa ktk kuboresha Huduma za afya,maji,elimu na kupunguza rushwa kwenye ofisi za uma na Huduma mbalimbali za jamii,
Uchaguzi wa 2020 hata wasipofanya kampeni wanashinda uchaguzi Ki rahisi sana.
 
Back
Top Bottom