Uboreshwaji wa Bandari ya Mtwara umeleta mageuzi

Rashda Zunde

Senior Member
May 28, 2022
199
231
Uboreshwaji wa bandari ya Mtwara umefanya kuongezeka kwa biashara ya makaa ya mawe kutoka Kusini mwa Tanzania na kuipa Bandari ya Mtwara ambayo ni ya 3 kwa ukubwa nchini maisha mapya.

Uwekezaji wa kimkakati wa serikali katika uboreshaji wa Bandari ya Mtwara umegeuza bandari hiyo kuwa tegemeo la usafirishaji wa mizigo kwenda na kutoka mikoa ya Kusini mwa Tanzania na mataifa jirani.

Maana ya uwekezaji huo unaonekana katika ongezeko la shehena na mapato kama takwimu zinavyoonyesha, katika kipindi cha miezi michache shehena ya mizigo inayopita Bandari ya Mtwara, hususani makaa ya mawe, imepanda kiasi kikubwa huku makusanyo ya mapato yakipanda pia.

Ukusanyaji wa mapato uliongezeka kutoka sh bilioni 14 mwaka wa fedha 2020/21 hadi sh bilioni 23 mwaka wa fedha 2021/2022, ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 64.2.

Bandari ya Mtwara ilijengwa kati ya mwaka 1948 na 1954 ni miongoni mwa bandari kuu tatu zinazosimamiwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).
 
Kúmermayo, bandari ameipanua JPM, Mwezi march 2021 alipanga kuja kuzindua bandari na hospitali ya kanda bahati mbaya akafariki.
Umetukana bure weye. Mi nimemuambia huyu binti makusudi
 
Kúmermayo, bandari ameipanua JPM, Mwezi march 2021 alipanga kuja kuzindua bandari na hospitali ya kanda bahati mbaya akafariki.
Nani amekamilisha uboreshwaji wa bandari hyo? Kama sio Rais Samia Suluhu, apewe pongezi zake kwani ametekeleza alishoahidi tena kwa ufanisi.
 
Haya ndio maendeleo na fursa zitafunguka na kupunguza umaskini kwa watu wa kusini na nchi nzima, ni kweli JPM alianzisha hili apewe sifa zake, JPM kwangu ni mixed legacy lakini all in all kazi alikuwa mchapa kazi na alikuwa anaelekea kufanya mambo makubwa sana
 
Back
Top Bottom