Ubora wa Waziri Maghembe unatia shaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubora wa Waziri Maghembe unatia shaka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MchunguZI, Oct 18, 2010.

 1. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Mashaka yangu yanatokana na matamshi yake ambayo hayaonyeshi kama ana wajibika kwa Wizara yake. Naona kama hayana ufahamu tunaoutegemea kutokana na kisomo chake.

  Kuna wakati nilimuona akiwadhalau watumishi wa vyuo vikuu kwa kudai mabadiliko ktk mfumo wa malipo ya PPF. Badala ya kuwasaidia, akawadhalau na kusema wafanye utafiti ili wapate pesa. "Wasisubiri kulishwa midomoni....", Ohhh! (akaigiza kwa kupanua mdomo wake mbele ya kamera ya TV). Sikujuwa uhusiano wa madi yao na utafiti.

  Sasa kuna tatizo la wanafunzi wa vyuo vikuu kushindwa kupiga kura kwa likizo ya lazima waliyopewa bila sababu. Majibu yake tena yamekuwa ya aina hiyo. Anasema eti wasifanye siasa vyuoni. Yamaanisha wameondolewa kwa sababu za kisiasa, basi!

  Huyo ndo Waziri akijibu kwa kutumia akili yake yote wakati huo huo anafahamu CCM ndo wanaingiza siasa vyuoni na wamekuwa wakifungua matawi ya CCM vyuoni. Nawasikia sasa wakifungua hata nje ya nchi sijui kwa faida ipi!

  Nadhani ni waziri asiyekuwa na faida kwa wadau wa Wizara husika. Huko Maliasili ndo hatuna haja ya kusema ubora wake pamoja na kwamba yeye ni bwana miti.
   
 2. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Huyu ni msomi aliyechanganyikiwa!ukiingia kwenye siasa na hasa siasa za Tanzania,hata ukiwa msomi mzuri,ambaye unaweza kutolea ufafanunuzi matatizo yanayowakabili wananchi,utalazimika ujibu majibu ya hovyo hovyo ili uweze kukidhi matakwa yako au ya chama chako kisiasa!huu ni ujinga mkubwa!
   
 3. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Kuna watu walisema siku nyingi kuwa watu wa usalama wa taifa huwa wanatakiwa kumsaidia Rais kuteua baraza la mawaziri, na mtu anayeteuliwa kuwa waziri anatakiwa kuwa makini na anachoongea, sasa sijui kama uslama wa taifa walifanya kazi yao, au ndio kuna watu waliteuliwa tu bila kufuata itifaki zinazotakiwa kufuatwa. Si yeye tu kuna wengine wanaongea ovyo hata zaidi ya huyo, so it shows that somemthing is wrong somewhere.
   
 4. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Huyu ni profesa wa miti shamba, kwani maji marefu haitwi Prof???

  Kwa ujumla kuna magogo mafu mengi kwenye balaza la JMK na hawastahili kabisa marupurupu wanayopata kama mawaziri. Sofia Simba, Maghembe, Mwangunga, Mkulo, Kapuya, etc!!!!
   
Loading...