Muda nikafanya tafiti ndogo hapa mtaani kwangu. nikagundua mtaa una 'Bar' na 'Grocery' kumi na saba. ni eneo la mraba si zaidi ya 900. Huko Mbeya rafiki yangu mwingine alifanya tafiti ndogo akagundua kata moja ina kanisa 67. Watu wengine wanawekeza kwenye klabu za mpira fedha nyingi tu. Vile vile nishuhudia mtu anageuza seburi ya nyumba yake kuwa "Nursery School' na sasa anamiliki shule kubwa!!!.Dhamira hushinda kheri.
Wachangiaji wengine watakuja na takwimi rasmi. Hapa nina mambo matatu ambayo ningependa kuchangiana na wengine. Moja, Je? tunapotaka kuendeleza elimu, Ujuzi au Ufundi na Taaluma, tunafikiri kuanzia na vyuo vilivyojitosheleza katika kila hali kwa hali yetu ya uchumi walionayo watu wetu?. Mbili, Hivi? Serikali inapokuwa inafanya ukaguzi inakuwa na lengo la kuboresha au kwenda kutafuta makosa ili ifungie uwekezaji wa watu wetu katika maeneo niliyotaja hapo.Tatu na mwisho, hawa watu wanaojitoa kuwekeza katika maeneo haya ya Elimu, Ujuzi au Ufundi na Taaluma kuna tahadhari yoyote tanazopasa kuwachukulia tofauti na uwekezaji mwingine?