Ubora wa "Open University of Tanzania"

namanyele

JF-Expert Member
Oct 19, 2012
1,852
608
Habari wana "Great Thinkers",huwa naskia maneno mengi sana kuhusu Open University,actually mengi huwa si mazuri sana na leo nimeona nilete humu Jf nina uhakika nitafahamu ukweli kuhusu hiki chuo,ningependa nifahamishwe yafuatayo:
1.Ubora wa hiki chuo na ubora wa degree zao kulinganisha na vyuo vingine
2.ubora na uwezo wa wanafunzi wao waliohitumu hiki chuo hasa wakiwa kazini na maeneo mengine

Ni hayo tu wakuu nilipokosea mnirekebise
 
Kama huwezi kujitafutia walimu na in mvivu wa kujisomea mwenyewe open utatoka huna kitu kichwani, kitu wanafunzi wengi wanapata tatizo nalo, lakini mitaala yao ni mizuri kama kawaida na wana manuals nzuri,ukitaka kusoma hapo lazima ujipange kutumia muda wako vizuri. Hakuna mtu atakukumbusha leo kuna kipindi njoo darasani, Mfano kuna wanafunzi wa sheria ambao walienda law school na walifanya vizuri kupita wale wa vyuo vingine. Pia wana library Ina vitabu vizuri sana. Wanafunzi wanaoona pagumu ni wale wanaoshindwa kuwatumia walimu wa pale vizuri. Ukitaka tatizo eneo Fulani wanakusaidia kukufafanulia.

Wako wengi makazini na wanafanya vizuri tu. Ila mpaka umuulize ulipata wapi degree yako kitu ambacho si rahisi.
 
Kwa rank ya sasa hivi SUA inaongoza kwa ubora ikifuatiwa na OPEN UN.kuna vitu vingi vinaangaliwa kama walimu, product inayotolewa n.k UD wapo nyuma
 
Kwa rank ya sasa hivi SUA inaongoza kwa ubora ikifuatiwa na OPEN UN.kuna vitu vingi vinaangaliwa kama walimu, product inayotolewa n.k UD wapo nyuma

mkuu hiyo rank walitoa lini? maana ya mara ya mwisho niliyopata UDSM ilikuwa inaongoza
 
Kwa rank ya sasa hivi SUA inaongoza kwa ubora ikifuatiwa na OPEN UN.kuna vitu vingi vinaangaliwa kama walimu, product inayotolewa n.k UD wapo nyuma
kuna watu wengi wamesoma pale UDSM ambao sekondari walikuwa weupe sana. Lakini kwasababu wana pesa walienda pale kujilipia na wamesoma wamemaliza. Nashindwa kuelewa wanawezaje? naona hii hoja ni upuuzi sana,la msingi ni kuangalia JE WAHITIMU KWENYE VYUO VYETU WANA VIWANGO? Mwanafunzi asiye na uvumilivu na jitihada hawezi kusoma open akamaliza. LAZIMA aache mwenyewe
 
Kama huwezi kujitafutia walimu na in mvivu wa kujisomea mwenyewe open utatoka huna kitu kichwani, kitu wanafunzi wengi wanapata tatizo nalo, lakini mitaala yao ni mizuri kama kawaida na wana manuals nzuri,ukitaka kusoma hapo lazima ujipange kutumia muda wako vizuri. Hakuna mtu atakukumbusha leo kuna kipindi njoo darasani, Mfano kuna wanafunzi wa sheria ambao walienda law school na walifanya vizuri kupita wa "thanx mkuu 4 gud information"
 
  • Thanks
Reactions: Izc
Kama huwezi kujitafutia walimu na in mvivu wa kujisomea mwenyewe open utatoka huna kitu kichwani, kitu wanafunzi wengi wanapata tatizo nalo, lakini mitaala yao ni mizuri kama kawaida na wana manuals nzuri,ukitaka kusoma hapo lazima ujipange kutumia muda wako vizuri. Hakuna mtu atakukumbusha leo kuna kipindi njoo darasani, Mfano kuna wanafunzi wa sheria ambao walienda law school na walifanya vizuri kupita wale wa vyuo vingine. Pia wana library Ina vitabu vizuri sana. Wanafunzi wanaoona pagumu ni wale wanaoshindwa kuwatumia walimu wa pale vizuri. Ukitaka tatizo eneo Fulani wanakusaidia kukufafanulia.

Wako wengi makazini na wanafanya vizuri tu. Ila mpaka umuulize ulipata wapi degree yako kitu ambacho si rahisi.

unaongelea Dar wewe. Nje ya Dar ni hoovyo
 
1. Huwa nalinganisha wanafunzi wa OUT na kuku wa kienyeji (wanaojitafutia chakula wenyewe) kuliko kuku wa kigeni - wanaofugwa - (wanaopewa chakula muda ukifika).
2. Ukisoma OUT nilichojifunza ni kwamba hakuna kulala - yaani, kama huna culture ya kujisomea na kutawala vizuri muda wako huwezi kufaulu maana kila kitu kinategemea bidii yako ya kukitafuta.
3. Mimi pia nasoma OUT na ninachokifanya ni kupata 'course outlines' ya masomo ninayoyachukua na kuona ni vitabu gani nihitaji na natafuta fedha na kuvnunua vitabu na materials mengine (sheria nyingi au case laws nazipata kwenye mtandao). Kutokana na 'workload' yangu sipati muda wa kwenda 'tuition'.
4. Actually, niliacha kwenda tuition kwa maana siku moja jamaa mmoja alikuwa akitushawishi tumhonge mwalimu hela eti atufanyie assignments akidai "kusoma kwa siku hizi ni tofauti na zamani. Siku hizi tunasoma ili kupande cheo na kupata mshahara mzuri na siyo kuelewa. Huyo njemba aliwashaiwshi karibu asilimia kubwa ya darasa na siku waliyopanga kupeleka hizo fedha nikaona nikienda wanaweza kudhani nawachimba mkwara maana sikuwa tayari kuoneshwa assignment bali nilitaka nijipime mwenyewe kuliko kupata maksi ambazo sistahili.
5. Hii ilinifanya niwe negative kuhusu tuitions na tangu siku hiyo siendi tena na wala sidhani kama nitaenda hata siku moja.
6. Wapo na wanafunzi wengine waliosusia na huwa tukikutana tunajikumbusha "eti hata assignement watu wanataka waoneshwe na test au mtihani itakuwaje?"
7. Mimi nimejiwekea utaratibu wa kusoma kila siku nikiwa kazini (muda ambao sina kazi ya kufanya) na nyumbani. Nimejipangia ratiba yangu kuwa baada ya masaa ya kazi nafika nyumbani, napumzika na kisha nalala masaa 6. Yakiisha naamka na kuanza kusoma hadi muda wa kwenda kazini tena siku inayofuata. Nina muda wa kupumzika (kwa maana ya ku'relax' pia na kufanya mazoezi nisije nikawa 'anti-social'). Huenda ratiba yangu ni tofauti na ratiba za watu wengine. Naingia ofisini mara nyingi saa 4:30 (asubuhi) na kutoka saa 2:00 au 3:00 (usiku). Kama ningekuwa natoka nyumbani saa 12:00 au 1:00 asubuhi na kurudi saa 11 jioni ningepanga ratiba yangu pia inipe muda wa kupumzika na masaa 6 ya kulala usingizi. Hii ni nzuri kwa afya.

8. Kwa hiyo, achana kabisa na watu wanaodhani kiwango cha elimu OUT kiko chini maana inategemea mtu mwenyewe na jinsi anavyo'manage' muda wake. Hata kama ukiwa kwenye chuo bora kiasi gani kama wewe mwenyewe hujitumi haikusaidii kitu. Inabidi kufanya 'sacrifices' otherwise itakuwa vigumu kufaulu. Kitu kingine ni kwamba ukisoma kwa kuwategemea sana walimu unaweza kuwa 'disappointed'. Inabidi uwe kweli na 'discipline' ya kupanga na kutekeleza mipango yako mwenyewe kwa asilimia kubwa kama unataka kufaulu OUT.
9. I really like kuwa kama kuku wa kienyeji kwa maana katika kujitafutia chakula mwenyewe nagundua vitu vingi, ambavyo kama ningekuwa kwenye conventional unviversity nisingeweza kupata. Lakini mimi tangu zamani ni mtu ninayependa kujisomea peke yangu. Huwa ninatumia kanuni kwamba kama mwalimu amesoma kitu fualni na kukielewa na kisha kutufundisha kwa nini mimi nishindwe kukielewa nikikisoma peke yangu? What's wrong with me? Hii inanifanya nisikate tamaa niendelee kutafuta "chakula" hadi nipate!
10.OUT inafunza bidijii ya kujituma na kuwajibika maana bila ya kufanya hivi hakuna kufaulu!
 
du! nimekuelewa mkuu Magobe napenda sana nisome OUT ili niwe creative zaidi,binasfi nimefanya paper ya form 6 combination HGE nilipata div.III ya 13 mwaka 2006 ukweli sikuwa kuingia darasani wala tuition aina yoyote,mpaka leo napenda sana kujisome coz najihisi kama naelewa sio kukalili na pia huwa sipendi kusoma kupitia past papers,sasa chuo nimepangiwa Mount meru ila course sijaipenda nataka niombe OUT ndo mana nikaomba huo ushauri kuhusu hiki chuo,university sio kama sekondari
 
Poa! Kama una nidhamu ya kupanga na kutekeleza ulichokipanga basi OUT itakupa fursa ya kuwa "kuku wa kienyeji" na siyo "kuku wa kisasa au wa kufugwa". Lazima utambue kuwa OUT ni "student oriented learning" na siyo "teacher oriented learning."
 
Sawa kabisa!!! Misingi ya familia zetu nyingi ni kuangalia movie nyingi na si kusoma vitabu vingi!!! na ndiyo maana OUT inatushinda na kuiona ngumu sana!!! Ila ni elimu moja tamu sana kama utajua namna ya kwenda na muda na bidii ya kujisomea tu basi!!
 
Nimesoma BACHELOR yangu OUT, sasa namalizia masters yangu hapo hapo! nimepapenda kiukweli, hakuna kuigiza kusoma, bidii yako na kujitegemea hujenga mafanikio yako, isitoshe you learn to be an independent in the job market, mtu akimaliza open nadhani atakuwa na uwezo mkubwa hata wa kustahimili changamoto za ajira! ila kweli kama wewe kusoma kwako hadi usukumwe OPEN hapakufai tafuta vyuo vingine! zamani chuo kilikimbiliwa na vijana, kwasasa vijana wamefahamu siri ya OPEN kwamba kusoma si lazima muda wote wa miaka 3 upoteze kwa kusoma pekeyake, wakati uraiani maisha yanasonga, UNAKOSA Uzoefu wa kimaisha! Hii ni kwa wale wenye kupenda elimu huria! bachelor yangu ina nguvu tu kwenye michongo ya kazi na kujiendeleza zaidi.
 
bro hapo nimekupata mimi shida yangu ni oss 101 social work na oss 108 kama vinapatikana nijurishe bro gharama
 
Mimi naona kizunguzungu 2. Wsh I cudnt join that thng! its rly hectic.
Ila uzuri ni unasoma pepas zikianza. Othwz unakula bata. Mi nna kauli mbiu yangu ever since 'HUWEZI KUSOMA SOMA BILA SABABU'

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Ubora wa chuo upo kichwani mwako na sio title ya chuo unachotoka.

Waajiri walio makini (ikiwemo serikali) wanaangalia kichwani mwako kuna nini na sio umesoma chuo gani. issue ya chuo inaweza kujitokeza pale ambapo itaonekana kuna shaka ya recognition ya chuo ulichosoma (hasa vyuo vya nje ya nchi).
jenga kichwa chako kiwe vizuri kwenye fani yako utapiga dili nyingi kuliko ukawa mburula na kutegemea kubebwa na jina chuo
 
MULUGO ni wa hapo, in short OUT ni wazuri Dar tu kwani wana madarasa Kinondoni na Temeke. Kwingine siasa

INawezekana kweli, hivi mtu yuko NAMANYELE Hana kitabu, msaada wa mwl., ataweza vipi kulinganishwa na wa DAR, MWANZA AU ARUSHA? Hata ktk graduation list majority ni wa miji mikubwa. kuhusu ubora wa elimu ni wa hali ya juu. Lecturers ni qualified.
 
Back
Top Bottom