Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,778
Choroko ni zao tunalolitumia sehemu nyingi, wengi tunakula choroko kama kitweo. Kupata ubora wa ziada katika choroko ni kula na kimelea, katika halii hii unapata protein kwa ubora wake. Hii pia ni nzuri kwa wale waliopumzika kula nyama au kuamua kuwa walaji wa mboga mboga.
Chukua kikombe cha choroko, zioshe tu usiziloweke, zitoe kwenye maji, taarisha ungo weka tea towel au paper towel kwenye ungo kuepusha mchuruziko wa maji. Weka choroko zako humo na uziache sehemu kavu kama juu ya kabati. Zirudie baada ya siku mbili utaona zimeota vimelea. Hizi ziko tayari kuliwa. Una weza kuzichanganya kwenye kachumbari au bakuli la salad.