ubingwa wa enyimba champions league 2003, na mamelodi 2016 kama naiona kwa simba vile . Babra na Mo wananitisha mimi Mwanayanga

Enyimba iko wapi siku hizi ama tajiri alijitoa vp pia timu za waarabu mbona hazichukui sana caf champions na hela wako vzr
Timu za uarabuni zinaongoza kuchukua makombe ya caf champions.

Caf champions ilianza mwaka 1965, mpaka sasa ni miaka 55 tangu ianza.

Timu kutoka misri, tunisia, algeria na moroko zimetwaa kombe hili mara 31. Tangu miaka ya 90 africa kaskazini inatawala kwenye michuano ya vilabu afrika.
 
Mamodel wa humu huwa wanamihemko ya ajabu,sasa Uzi kama huu unafutwa kwa tatzo lipi
 
Simba jifunzeni kwanza kushinda away games Tena wakiwa na mafans wao ndo muanze kuongelea habar za ubingwa wa caf
 
Mamelodi pia waliamua kumpa timu mzee Motsepe.

Hii Mamelodi Sundown almaarufu "Masandawana" ima "The Brazilians" ni project ya Motsepe mwenyewe. Hakupewa na watu wengine.

Model yake ni kama Azam FC.

Sio kweli... mamelodi sundowns imeanzishwa 1970, yaani miaka 51 iliyopita.. ni timu ya wanachama..

Motsepe aliuziwa share 51% mwaka 2004.. ila akawa anaiendesha bila kuwekeza sana... mwaka 2013 ndipo alipoamua kusajili watu wa gharama na kubadili managememt ya timu.. tangu hapo mamelodi ikaanza kutawala soka kuwapita wakongwe kina orlando pirates na kaizer chiefs.. na miaka mitatu mbele yaani mwaka 2016 ndipo mamelodi akatwaa caf champions league kwa mara ya kwanza.. na hiyo siku mzee motsepe alivua shati na kubaki tumbo wazi kwa furaha...

Mzee motsepe aliuziwa share na wanachama mwaka 2004 .. yeye ni mmiliki wa asilimia 51.. sio model ya azam.. mamelodi ina miaka zaidi ya 50 tangu ilipoanzishwa..
 
Habari wadau..

Nimeona documentary ya enyimba success timu ya kwanza nigeria ku win caf champions league.. nimeiangalia kwa umakini nikajua ilikuwaje?

Kwa nilichokiona kwa enyimba kama nakiona kwa Mo na simba yake ya zama hizi.

Enyimba ilikuwa timu ya kawaida sana nigeria haijawai kuifikia enugu rangers wala haijawai kuifikia heartland kwa mashabiki .. ila ndio timu pekee iliyotwaa ubingwa wa africa kutoka nigeria na tena sio mara moja. Safari ya enyimba naiona kama simba maana kuna mtu anaitwa mzee Kalu.. mu Igbo mwenye hela zake mzaliwa wa enyimba village, aliamua kuweka hela kama Mo anavyofanya simba.. kama mo alivyompeleka babra simba. Kalu na yeye alimpeleka binti yake enyimba ndio akawa mlipaji wa kila kitu cha timu.. kalu aliogopa kuibiwa

Pia hata Mamelodi sundowns safari yao ya ubingwa wa caf champions legue 2016.. ina story kama ya simba.. maana south africa mamelodi imezidiwa kiasi kikubwa na vigogo kaizer chiefs na orlando pirates.. ila ndio timu pekee mamelodi inasumbua caf.. maana kuna mtu kama mo aliamua kuweka hela anaitwa mzee motsepe.

Mimi mwanayanga ila naona kabisa simba atatwaa caf champions league mapema kuliko yanga yangu kwa staili yetu ya kuwapa vyeo kina msolla...

Wazee kama Msolla kwa mfano ukweli kabisa mabadiliko hayataki ila anazuga anayataka kwa mbinu ya kuyachelewesha ili ale pesa za yanga mpaka anazeeka na kustaafu.. msolla sio mjinga kuchelewesha mabadiliko.. anajua yakija haraka cheo chake kitafutwa na yeye atakosa ajira.

Enyimba wa igbo waliamua kumpa timu mzee kalu.. na akaifanya timu iwe kigogo africa..

Mamelodi pia waliamua kumpa timu mzee Motsepe..

Yanga gsm hawezi kuweka hela za kutosha sababu hajapewa timu kama Mo alivyopewa simba.

Huu uzi mods usiufute.. ili uwe kumbu kumbu pale simba watavyotwaa Caf champions league kama utani vile.. huku yanga tunabaki na msemo timu ya wananchiii na kulilia penaly ligi ya wendawazimu bongo.

Kwa mnaotaka kujua story ya enyimba na kalu someni hapa .. mtajua Mo ni kalu wa simba.

Na nina wasiwasi Mo kaangalia izo documentary za enyimba na mamelodi nayeye kaamua kupita humohumo........
 
Nimeikumbuka Yanga ya Manji, ilifika hatua Yanga ikawa inawatambia Simba kwa kujiita wakimataifa, maana walishiriki kila mwaka kombe mojawapo la Afrika huku Simba ikiishia hapa nchini.

Baada ya kufulia, wakaachana na jina wakimataifa na kujiita timu ya wananchi maana walianza kutoza sadaka katika kila mechi.
 
Wako watu yanga wanatakiwa kuondoka haraka sana pia as YOUNG funny hatujapata mdhamini wa kikweli kweli tulionao ni wapigaji tu
 
MO anamiliki hisa 49%, wanachama 51%. bado timu ni ya wanachama
Kumbuka kwenye hizo hamsini na moja share na yeye yupo kama mwanachama!! Ndugu zake wote ni wanachama!! Wahindi wameweka mtego, siku Simba itakapo anza kuuza share rasmi!!, Mtego ndio utateguka na timu kuwa ya kanjibahi and co.
 
Back
Top Bottom