ukweli mhimili
Member
- May 31, 2014
- 11
- 4
Ubinafsi wa kiakili ni ile hali ya kuamini fikra zako tu binafsi.Tunapofikri kwa mtindo huu,hatutaweza kufahamu mawazo,hisia na mihemko ya wengine.
Huu ni mtazamo wa kiasili ambapo tunaguswa zaidi na maumivu yetu pamoja na matamanio yetu,na matumaini yetu ndio tunayoyapa nafasi kwanza kuliko ya wengine.Mahitaji ya wengine hayana umuhimu kabla ya kutimiza mahitaji na matamanio yetu kwanza.
Hatuwezi kutilia maanani masuala,matatizo na maswali kutoka kwa wengine yanayotofautiana nasi, kwani tunapoamua kuyatilia maanani yatatulazimisha kubadili mitazamo yetu.
Tunawezaje kutenda haki kwa wengine kama hatujajifunza jinsi ya kujishusha na kufikiri kama wao?
Kama hatutajifunza namna ya kua upande wa wengine na kwa umakini kufikiri kama wanavyofikiri,hatutaweza kuhukumu kwa haki mawazo na imani zao.
Kwa mfano, ukishindwa kufikiri kwa mtazamo wa msimamizi wako,utapata ugumu wa kufanikiwa katika kazi yako na mwishowe utavunjika moyo.Ukishindwa kufikiri kwa mtazamo wa wafanyakazi wako utashindwa kuwaelewa kwa nini wanafanya hivyo wafanyavyo.Ukishindwa kufikiri kwa mtazamo wa mke wako ubora wa ndoa yako utaathirika.Ukishindwa kufikiri kwa mtazamo wa watoto wako,watahisi huwaelewi na watajiweka mbali na wewe.