Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 14,176
- 25,919
Leo hii, kama vyama vyote vya siasa vingechukua msimamo wa kukataa kutia sahihi kanuni za uchaguzi, amini nawaambieni, sasa hivi tungekuwa tunaongea mambo mengine kabisa. Vyama vya siasa havikuiona na kutambua kuwa hiyo ilikuwa nafasi ya kuilazimisha CCM kukaa nao mezani na hata kubadili kanuni za uchaguzi.
Ingekuwa kituko cha dunia nzima CCM kuingia uchaguzi mkuu wakiwa chama pekee cha siasa kwenye uchaguzi mkuu. Dunia nzima ingewashangaa, na hata kama CCM hawana aibu, kwa hili wangeona aibu! Wasingekubali kuwa na legitimacy ya kuongoza serikali kwa ushindi ambao vyama vyote vya siasa viliususia uchaguzi. Huenda hata JWTZ wangeamua kuingilia kati.
CCM wataendelea kutumia filosofia ya divide and rule kuhakikisha wanaendelea kuwa madarakani, na divide and rule ni kuhakikisha vyama vya siasa haviungani katika kufikiri, na hasa na Chadema.
Hebu tuseme ukweli, zaidi ya ACT Wazalendo, huu utitiri wa vyama vingine 16 waliotia sahihi kanuni za uchaguzi, kweli kweli wanategemea kutoa upinzani kwa CCM na kushinda nafasi ya uraisi au hata viti vya ubunge?
Na upande wa ACT Wazalendo - ubinafsi na kujitutumua (pride) ndio imefanya mkatie sahihi ujinga huu wa kanuni za uchaguzi. Pride kwa kuwa hamtaki kuonekana mnafanya mambo chini ya kivuli cha Chadema, na ubinafsi kwa kuwa mnaona Chadema kutoshiriki uchaguzi kunawapa nafasi ya kuwa Chama Kikuu cha Upinzani nchini. Lakini ndani ya mioyo yenu mnajua it was wrong kutia sahihi. Mko tayari kutoonekana mnaishi chini yakivuli cha Chadema, lakini hamuoni ubaya kuishi chini ya huruma za CCM
Kwa namna hii ya kufikiri kwa vyama vya siasa nchini, CCM itatawala milele na nyie wengine mtaendelea kuwapo kwa huruma za CCM siku zote. Kurushiwa makombo na CCM.
Lakini it is not too late - waandikieni INEC kwamba mna-revoke sahihi zenu. La sivyo, poleni sana. Vyama vyote vya siasa vikisusia uchaguzi, amini nawaambieni, CCM watalazimika kubadili msimamo. Tikiseni kibiriti.
Ikiwa CCM wanaona ili kuilazimsha Malawi kununua mchele wa Tanzania ni kuwasusia Malawi mazao yao na kuwanyima matumizi ya bandari yetu, basi wanajua wakisusiwa uchaguzi mkuu itabadi wakubali yaishe. Simple psychology.