Elice Elly
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 1,268
- 1,593
Najiuliza Swali hilo hapo juu Lakini nakosa jibu. Mwl Nyerere alitufundisha kuwa Binadamu wote ni sawa. Cha ajabu Leo hii uthamani wa Mwafrika aliyeko Marekani na Mwafrika aliyeko Bongo ni tofauti.
Wabongo wanalaani vitendo viovu vinavyo tendwa na wazungu dhidi ya Waafrika lakini hawalaani vitendo viovu vinavyotendwa na Waafrika dhidi ya Waafrika wenzao. Tunashuhudia watu wanauawa, wanapigwa risasi, wanatekwa, wanafunguliwa kesi za kubumbabumba. Lakini hayo kwavile yanatendwa na Waafrika dhidi ya Waafrika wenzao kila mmoja anaona sawa. Ile kauli ya Mwalimu Nyerere ina maana gani?
Matendo yanayotendwa Leo na watawala ni yaleyale waliyo tenda makaburu nasi tukawa mstari wa Mbele kupiga kelele, leo kipo wapi? Tunayatenda tena kwa Uhuru bila kificho na baadhi ya wabunge wakiyashabikia tena wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge. Waafrika Tuache unafiki, tukemee kwanza ya hapa nyumbani kwani yanatisha zaidi kiasi kwamba watu wameogopeshwa na wanaogopa kufungua vinywa vyao.