Peter Stephano 809
Senior Member
- Feb 29, 2020
- 120
- 162
Kuna wakati niliamini kila mtu aliyekaribu na mimi basi ananipenda na anaweza kuwa mtu mwema sana kwangu.
Lakini baadae nikaja kugundua kuwa ukaribu na upendo ni mambo ambayo inawezekana hayana ufanano ingawaje yanakaribiana.
Umenielewa? ndio ipo hivi, Unaweza ukawa na watu wengi unaoishi nao nyumba moja, mtaa mmoja pengine hata kula nao pamoja lakini usijue wanakuwazia nini jema ua baya.
Tumesikia mara ngapi "Mke amuua mume wake, Mume amuua mke wake" ni mara nyingi tu.
Je bado tukae tuamini kuwa upendo wetu hutokana na ukaribu au urafiki tunao upata kwenye familia au jamii zetu?
Si ajabu kukuta mtu unatetwa kwa maneno ya uzushi ambayo ni kashfa juu yako lakini usipate kumbiwa na mtu yeyote juu ya huo uzushi mpaka pale utakaposafiri kwenda Sehemu fulani ndio ukaambiwa ilifanya haya na haya ulikotoka ukabaki unashangaa mbona hata jirani yangu hajaniambia nakuja kuambiwa huku?
Ubinadamu ni fumbo kweli kweli, ndio maana tunaoishi nao wanashangilia matatizo yetu na kuchukia mafanikio yetu kwa sababu zisizojulikana.
Ubinadamu ni kukosa msaada kwa watu ulioamini watakusaidia na kupata msaada kwa watu ambao hawana ukaribu wala Urafiki na wewe tena haukuwahi kuwafahamu hapo kabla.
Mungu alituumba binadamu na tabia ya unafki ili tusiache Kuchukua tahadhari.
Kikulacho kinaweza kuwa nguoni mwako jitathmini kila wakati na watazame watu wanaokuzunguka kwa jicho la tatu lisilo na upendeleo.
Kwa kufanya hivyo Mungu atakupa uwezo wa kuwa na upendo kwa kila mmoja kwakua unataka kujenga hazina yako iliyonjema hapa duniani.
Ubinadamu ni fumbo kweli kweli jitahidi kutenda wema kwa watu wote hata wale usiowafahamu kwakua hujui nani mwenye kutenda wema kwako kwa wakati ujao.
Fumbo hili linataka kufumbuliwa kwa kuelewa kuwa haijulikani ni Nani mwenye hatma ya msaada wako na upendo wa kweli kwako.
Kiburi, dharau, majivuno na jeuri si tabia nzuri katika ujenzi wa Ubinadamu wenye matokeo chanya.
Asikwambie mtu Ubinadamu ni fumbo kweli kweli.