Mwalimu,
Kabla sijajibu swali lako, ngoja nikudunge swali, Ujamaa umetufikisha wapi kielimu na kiafya?
Kama Kenya na Uganda waliokimbilia Ubepari uchwara misingi na mfumo wa Elimu na Afya ni bora kuliko Tanzania, tulikosea nini na dhana ya elimu na afya kwa watu wote na kwa bure?
Hata aikijibu kwamba "ujamaa haukuifikisha Tanzania kokote kielimu na kiafya" unadhani hiyo itakuwa tosha kuhitimisha kwamba "ujamaa haufai"?
Ni sawa sawa na mtu akakukumbusha kwamba uchumi wa dunia unayumba sasa hivi nakakuambia kwamba hiyo inaonyesha kwamba ubepari umeshindwa, kwa hiyo ubepari haufai.
Unatafuta majibu rahisi kwa mswali magumu. Naomba nisisitize tena hakuna magic formula. Kama huwezi kutatua matatizo yako, basi si ujamaa wala ubepari utakaokusaidia. Hakuna manual ya ujamaa au ubepari inayoelezea jinsi ya kutatua matatizo yote.
Na ukiangalia vizuri utakuta watu wanatofautiana sana kwenye definition zao za ujamaa na ubepari. Unaweza kuta mnabishana wee, kumbe kila mmoja ana uelewa wake.
Kwa mfano, muheshimiwa Mchungaji uko against kabisa na "bure" kwa sababu unaamini ni dhana ya kijamaa, na ujamaa haujaifikisha nchi yako popote, na pengine ujamaa ndio chanzo cha matatizo yako yote. Na nadhani unaamni kwamba USA, UK, Australia, e.t.c. ni nchi za kibepari. Sasa ushawahi kusikia "unemployment benefits"? (
Unemployment benefits - Wikipedia, the free encyclopedia ). Je, unafahamu kwamba USA na UK wapo watu wanalipwa fedha za "bure" kihivyo? Je, hiyo inafanya nchi hizo ziwe za kijamaa?
Lesson of the day: ukitaka kuzungumzia ideologies, jaribu kuzielewa kwanza; wengi huwa tunazikurupukia na kuzipachikia dhana ambazo si zake. Elewa kwamba Ujamaa ni nini na Ubepari ni nini.
Mkapa mwenyewe aliingia kichwa kichwa akidhani ubepari maana yake ni FDI, sasa hivi, kwa habari sisizo thibitika, tunasikia anajuta huko aliko
🙂 Wasiwasi wangu ni kwamba wewe unadhani ujamaa ni kuwa na vitu bure, na ubepari ni kila mtu kujigharimia.
Ukiniuliza mimi ntakwambia ideologies zote zikitumiwa peke yake huwa zina-fail kwa sababu unakuwa unajaribu kutoa one simple solution to all complicated problems. People cling to ideologies when they run-out of ideas. Badala ya kufikiria ni jinsi gani ya kutatua matatizo ya elimu au afya, kwa mtu mwingine ni rahisi zaidi kudandia ujamaa au ubepari ukiamini kwamba hilo ndilo litakuletea suluhisho la matatizo yake yote au ndio chanzo cha matatizo yake yote. Mwingine atalaumu ujamaa au ubeprari mpaka pamoja na kushindwa kupata mke mwema au mume mwema.
🙂