Ubatizo wa Mwita25

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
61,365
Reaction score
100,406
Wanajamvi,

Wahenga walisema "Kweli itatuweka huru" na kwamba "Kitu anachoweza mtu mzima akiwa amekaa, kijana hawezi kukiona hata akiwa amesimama" hayo ndio maono na busara za wazee wetu, leo hii nimeguswa sana na michango madhubuti ya kina mwenzetu (sijui kama ni Me au Fe - hilo sio muhimu kwa sasa).

Umadhubuti wa michango yake hautokani na ukweli kwamba alijitoa kuisadia CCM la hasha bali ukweli kwamba, amyeafungua macho yake, akajitakasa, akaiona kweli na sasa yuko huru, hachangii kwa ushabiki, ni mwelewa lakini pia amejitahidi sana kuwepo hapa jamvini hata usiku wa manane (angali thread aliyoanzisha leo hadi asubuhi hii bado yupo na anaendelea kuchangia).

Huu ndio ninaouita ubatizo wa kweli, wa kujivua uongo, unafiki na uzandiki na kuamua kuwa mkweli (sizingumzii itikadi yake ya chama chochote).

Ningefurahi sana kuona na wale wengine, ambao najua wanafahamika kwa majina au hata kwa tabia waikiri ile kweli ili iwaweka huru, Mwita25 alisema ukweli kwamba alikuwa kama Sauli aliyelipwa ili kuikomoa na kuharibu mijadala ya maana kwa mustakabli wa Taifa (lengo lake na nia yake vinabaki sirini) ila sasa ameuona ukweli, nakutakia maisha yenye mafanikiona kamwe usirudi nyuma tena.

Ila nina tatizo moja kwako, kwanini hua thread nyingi unaanzisha usiku sana, maana hata ile ya kujivua gamba ilianzi ndotoni, naikumbuka vyema sana...
 
vigezo.
Aweke akaunti zake zote hapa hadharani,ili mods wazifungie.
 
Hivi haya mambo ya kutafuta umaarufu kupitia mgongo wangu yataisha lini?
 
mimi nilimpngeza ila ile id yake nyingine vipi?
 
anakaribia kuagana na wakuu hivyo anajiandalia njia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…