Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam watoa tahadhari ya kiusalama kwa raia wake kufuatia matishio ya Iran

Sasa ulitaka wahamishie ugomvi wao kwenye nchi yetu, waache wapiganie huko huko, huku watatuua na sisi tusiohusika
Wa Iran wao hawajali hilo, watamlenga Mmarekani mmoja katikati ya Watanzania mia moja, alafu watashangilia kumuua huyo Mmarekani hata kama ataangamia yeye na Wabongo 50.
 
Dunia nzima wanajua Iran inapotishia kulipiza kisasi sio kwamba wataenda kushambulia Marekani, hata al shababu watapiga kazi Mzee baba.
 
Ajabu kabisa kuna mtu yuko Jf na hajui hili tangazo linatuathiri vp, yaan anashindwa kuelewa kua hata kwenye sector ya Utalii tu kutaathirika maana hakuna mgeni anataka aende mahala ambako kuna waswas wa kiusalama? Yaani fikiria namna Wamarekani tu waliokua wamepanga kuja Tz siku za karibuni watakavyo cancel booking zao kutokana na hili tangazo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kimsingi hii tahadhari imetolewa sehemu nyingi nasiyo Tanzania tu. Kenya ndiyo kabisaa... vikosi vya wana usalama vimeongezeka mara dufu mtaani. Hili la Tanzania ni cha mtoto tu.
 
Tahadhari siyo Bongo pekee. Nchi nyingi sehemu zenye maslahi ya mmarekani zimeimarishwa ulinzi. Hata zile nchi za Ulaya ambazo hazina chokochoko nyingi wameimarisha ulinzi na kuna tahadhari.
 
Natamani balozi zetu zingekuwa zinafuatilia usalama wa raia wake kiasi hiki.
 
Actually, they will be safer in Tanzania than the US!
Acha kupotosha watu. Hilo tangazo ni standard procedure. Limetolewa nchi zote zenye Ubalozi wa Marekani. Unataka kusema watalii na wafanyabiashara wataacha kwenda kwenye nchi zote hizo kwa sababu ya hilo tangazo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…