Ubaguzi wa serikali juu watumishi wa Afya walioko TAMISEMI

Redpanther

JF-Expert Member
Feb 23, 2019
2,813
3,767
Habari za Asubuhi ndugu na wanajambi wenzangu. Ni muda sana sijaweka bandiko hapa JF. Majukumu na kazi za watu zinabana sana kusema ukweli. Naomba niende kwenye mada moja kwa Moja.

Mimi ni mtumishi katika moja ya Taasis za serikali katika Manispaa "X" mkoa mmoja maarufu kama Kanda Maalum. Nimeajiriwa huu mwaka wa Tatu sasa nipo napiga kazi. Katika miaka miwili iliyopita nikiwa kama mtumishi wa serikali chini ya wizara ya OR-TAMISEMI nimeshuhudia watu wakilalamikia na Wizara hii kuwabagua watumishi wa Afya walioko chini ya wizara hii. Mambo machache naweza taja ambayo toka nimeingia kazini sijawahi kulipwa na sijui ni lini nitalipwa ni pamoja na;
  • Extra-duty
  • On call
  • Posho za likizo
  • Fedha za Kujikimu (Hizi zilichelewa sana)
Nilijaribu kuwafuata Viongozi wakadai frdha hazitumwa na serikali. Changamoto hizi nilizozitaja huwezi sikia kwa mtumishi wa Afya aliyeko chini ya Wizara ya Afya. Mpaka inafika muda najilaumu kwanini nisijgekaa tu mtaani huenda labda ningepata kitu cha Kufanya. Hi inasababisha kukosa motisha ya kazi. Hebu waza unaingia kazini usiku unakesha na wagonjwa lakini bado linapokuja suala la stahiki kama On call haziji kwa wakati.

Kuna wale walionitangulia wanasema wamekua wakiomba kwenda kusoma vibali ni shida kupata. Na hata ukipata bado recategorization inacheleweshea sijui shida iko wapi? Juzi kazi Waziri mwenye dhamana alitoa maagizo juu ya kucheleweshwa kwa Malipo ya fedha za Kujikimu za Ajira Mpya. Wakati huo huo, Watumishi wapya waliopata Ajira chini ya Wizara ya Afya walipata mapema sana.

Je, shida iko wapi? Kama hili la watumishi kupata stahiki zao basi Watumishi hawa warudishwe MoH. Watumishi wa Afya walioko TAMISEMI wanafamilia majukumu sawa tu hao walioko MoH. Waziri mwenye dhamana anapambana ila bado hizi changamoto haziishi. Hebu ifike mahali watumishi hawa wawe chini ya Wizara ya Afya tu.

Mambo haya yanapunguza morali ya kazi na hata wakati mwingine kupelekea kupungua kwa ufanisi na hata kupelekea Wananchi kupata huduma Mbovu na kutukana watumishi hao.

Kuna wakati nawaelewa wale waliokua wanakataa kuripoti vituoni. Kituo upamgiwe huko ndani ndani Mawe matatu kwenye Zahanati. Unafika kituoni unakuka hakuna nyumba, eneo lina shida ya maji wakati mwingine ukakaa wiki nzima bila maji lakini unavumilia. Kwenda kujiendeleza napo shida. Wakubwa mnataka watu wabaki na elimu zao zile na waangamie huko wafe wakiwa masikini na watoto wao wafe kwa utapia mlo?

Hebu hili liwafikie wahusika. Lakini pia ningeepeweshwa kwanini hospitali za Mikoa Wilaya, Vituo vya Afya na Zahanati ziko OR-TAMISEMI na sio MoH. Na huku ndio kumejaa wale wazee wa Unanijua mi nani?

20231012_114943.jpg

Screenshot_2023-10-12-11-57-37-076_com.twitter.android-edit.jpg

Screenshot_2023-10-12-11-45-33-315_com.twitter.android-edit.jpg
Screenshot_2023-10-12-11-49-26-667_com.twitter.android-edit.jpg
Screenshot_2023-10-12-11-45-04-325_com.twitter.android-edit.jpg
Screenshot_2023-10-12-08-35-15-724_com.twitter.android-edit.jpg
Screenshot_2023-10-12-08-36-10-829_com.twitter.android-edit.jpg
Screenshot_2023-10-12-11-56-41-348_com.twitter.android-edit.jpg
 
Back
Top Bottom