Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,305
- 33,924
Ubaguzi ni kitendo au hali ya kumnyima mtu haki yake anayoistaili na kumpa mtu mwingine kwa kigezo cha jinsi alivyo kwa rangi yake, jinsia yake,kabila lake,asili yake, ama maumbile yake. Hali ya ubaguzi katika maisha ya Mwanadamu ni jambo ambalo lipo lakini lisilokubalika na jamii zilizostaarabika zimeweka sheria na Kanuni kuzuia watu kubaguana na kuona ni jambo la kawaida!
Kwa mwenendo wa mambo hapa nchini tangu miaka ya nyuma, CCM imekuwa inaendesha Ubaguzi wa kila namna ili mradi tu wanaofanyiwa ubaguzi huo si wana CCM kwa lengo la kuwatisha ama kuwakatisha tamaa watu hao ili kukifanya chama hicho kiendelee kubaki madarakani hata kama hakina sifa ya kuendelea kuongoza nchi yetu tuipendayo sote!
Fredrick Sumaye akiwa mjini Moshi zama hizo bado ni mwana CCM, aliwahi kusema kwamba kama mtu anataka mambo yake ya kibiashara yanyooke basi ni lazima awe CCM. Ukiiangalia kauli hii kijuu juu unaweza ukaona ni ya kawaida lakini maana yake ni kwamba usipokuwa CCM mambo yako hayatakunyookea na Ghadhabu ya kutokuwa CCM itakuangukia!
Leo hii kauli ambayo Sumaye aliitoa wakati akiwa CCM ndiyo ameiona kiuhalisia. Kitendo cha Sumaye kunyang'anywa shamba lake kwa nderemo zilizokuwa zinapigiwa chapuo na aliyekuwa Kada mwenzake wa CCM zama hizo, William Lukuvi, ni kielelezo cha kutimia kwa kauli hiyo ya kibaguzi aliyoitoa Sumaye akiwa CCM. CCM ilimfanya Sumaye kutengeneza Sumu ambayo amekuja kuinywa yeye mwenyewe.
Waislamu wanalalamika kwamba Magufuli hachagui waislamu kwenye teuzi anazofanya, lakini Jakaya Kikwete alipokuwa madarakani naye alilaumiwa na wana CCM wenzie wakristo kwamba kwenye kila teuzi anazofanya lazima idadi ya waislamu inakuwa kubwa kuliko wakristo. Kuteuana kwa kuzingatia dini kabila ama mtu atokako ni kansa ya ubaguzi iliyomo kwenye CCM ambayo kwa bahati mbaya sana wanaisambaza hadi kwenye jamii nzima ya watanzania.
Wakati CCM walisema CUF ni chama cha Waislamu hivyo wasichaguliwe kwa kuwa wataendesha nchi kwa kufuata "sharia", wenyewe kwenye Ilani yao ya Mwaka 2005 waliwaahidi waislamu kuwapa mahakama ya Kadhi. CCM inaposema CHADEMA ni ya watu wa Kaskazini hivyo kina ubaguzi, Magufuli kateua watu wengi toka kanda ya Ziwa lakini CCM haioni kama huo ni Ukanda.
Tanzania jambo lolote la kibaguzi huzaliwa CCM, hulelewa huko, hukuzwa na kudekezwa na wao, hukomaziwa kwenye jando na Unyago la ubaguzi la chama hicho, hulindwa na kisha hufanywa ni jambo la KAWAIDA. Lazima tupingane na ubaguzi wa CCM ama tukubali nchi yetu ivurugwe na ubaguzi unaopandikizwa na CCM!