Ubaguzi wa CCM unaivuruga nchi!

Allen Kilewella

Verified Member
Sep 30, 2011
13,509
2,000
Ubaguzi ni kitendo au hali ya kumnyima mtu haki yake anayoistaili na kumpa mtu mwingine kwa kigezo cha jinsi alivyo kwa rangi yake, jinsia yake,kabila lake,asili yake, ama maumbile yake. Hali ya ubaguzi katika maisha ya Mwanadamu ni jambo ambalo lipo lakini lisilokubalika na jamii zilizostaarabika zimeweka sheria na Kanuni kuzuia watu kubaguana na kuona ni jambo la kawaida!

Kwa mwenendo wa mambo hapa nchini tangu miaka ya nyuma, CCM imekuwa inaendesha Ubaguzi wa kila namna ili mradi tu wanaofanyiwa ubaguzi huo si wana CCM kwa lengo la kuwatisha ama kuwakatisha tamaa watu hao ili kukifanya chama hicho kiendelee kubaki madarakani hata kama hakina sifa ya kuendelea kuongoza nchi yetu tuipendayo sote!

Fredrick Sumaye akiwa mjini Moshi zama hizo bado ni mwana CCM, aliwahi kusema kwamba kama mtu anataka mambo yake ya kibiashara yanyooke basi ni lazima awe CCM. Ukiiangalia kauli hii kijuu juu unaweza ukaona ni ya kawaida lakini maana yake ni kwamba usipokuwa CCM mambo yako hayatakunyookea na Ghadhabu ya kutokuwa CCM itakuangukia!

Leo hii kauli ambayo Sumaye aliitoa wakati akiwa CCM ndiyo ameiona kiuhalisia. Kitendo cha Sumaye kunyang'anywa shamba lake kwa nderemo zilizokuwa zinapigiwa chapuo na aliyekuwa Kada mwenzake wa CCM zama hizo, William Lukuvi, ni kielelezo cha kutimia kwa kauli hiyo ya kibaguzi aliyoitoa Sumaye akiwa CCM. CCM ilimfanya Sumaye kutengeneza Sumu ambayo amekuja kuinywa yeye mwenyewe.

Waislamu wanalalamika kwamba Magufuli hachagui waislamu kwenye teuzi anazofanya, lakini Jakaya Kikwete alipokuwa madarakani naye alilaumiwa na wana CCM wenzie wakristo kwamba kwenye kila teuzi anazofanya lazima idadi ya waislamu inakuwa kubwa kuliko wakristo. Kuteuana kwa kuzingatia dini kabila ama mtu atokako ni kansa ya ubaguzi iliyomo kwenye CCM ambayo kwa bahati mbaya sana wanaisambaza hadi kwenye jamii nzima ya watanzania.

Wakati CCM walisema CUF ni chama cha Waislamu hivyo wasichaguliwe kwa kuwa wataendesha nchi kwa kufuata "sharia", wenyewe kwenye Ilani yao ya Mwaka 2005 waliwaahidi waislamu kuwapa mahakama ya Kadhi. CCM inaposema CHADEMA ni ya watu wa Kaskazini hivyo kina ubaguzi, Magufuli kateua watu wengi toka kanda ya Ziwa lakini CCM haioni kama huo ni Ukanda.

Tanzania jambo lolote la kibaguzi huzaliwa CCM, hulelewa huko, hukuzwa na kudekezwa na wao, hukomaziwa kwenye jando na Unyago la ubaguzi la chama hicho, hulindwa na kisha hufanywa ni jambo la KAWAIDA. Lazima tupingane na ubaguzi wa CCM ama tukubali nchi yetu ivurugwe na ubaguzi unaopandikizwa na CCM!
 

Allen Kilewella

Verified Member
Sep 30, 2011
13,509
2,000
Nani anayedai kwanini ni kudai wewe unaona raha sana kuitangazia dunia kuwa tuna zika unajua athar zake
Hajasema kwamba kuna ugonjwa wa ZIKA bali kuna watu wana Virusi vya ZIKA. Waambie wenzako hapo "Ofisini" hasa wale wazoefu kwamba kuna utofatuti kati ya kuwa na Virusi vya Ugonjwa na mtu kuwa ni Mgonjwa!!
 

sembela

Member
Aug 8, 2013
67
95
Hamna ubaguzi ndani ya ccm hata siku moja...watu wote wanafulsa sawa ndyo maana chama kinazid kuimarika siku hadi siku. Na nyumbu kawaida yenu kusema hovyo so tushawazoea. Na dhambi yenu ya ubaguzi ndyo inayotafuna chama chenu siku zote.
 

sembela

Member
Aug 8, 2013
67
95
Hakuna ubaguzi wa jinsia wala kidin ndani ya CCM haya ni mawazo mgando tu ya wana ufipa. Chama chenu kimekosa mwelekeo wowote mmebaki kukeje tu kila linalofanywa na serikal ya ccm. Mmejaa uroho wa madaraka tu hamna lolote. Jpm hajawahi kuteua mtu eti kisa ni wa kanda ya ziwa, anateua mtu kutokana na utartibu uliopo na weledi wa mtu husika katika kitengo husika...ts better mkamuacha afanye kazi kwa umakini ili atatue kero za wananchi kama ilani ya ccm inavyosema. So badiliken bana....alaaah.
 

Allen Kilewella

Verified Member
Sep 30, 2011
13,509
2,000
Jpm hajawahi kuteua mtu eti kisa ni wa kanda ya ziwa, anateua mtu kutokana na utartibu uliopo na weledi wa mtu husika katika kitengo husika...ts better mkamuacha afanye kazi kwa umakini ili atatue kero za wananchi kama ilani ya ccm inavyosema. So badiliken bana....alaaah.
Waislamu ndiyo wanalalamika na wameshampelekea majina ya Waislamu wasomi awateue!
 

habari ya hapa

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
12,800
2,000
Hakuna ubaguzi wa jinsia wala kidin ndani ya CCM haya ni mawazo mgando tu ya wana ufipa. Chama chenu kimekosa mwelekeo wowote mmebaki kukeje tu kila linalofanywa na serikal ya ccm. Mmejaa uroho wa madaraka tu hamna lolote. Jpm hajawahi kuteua mtu eti kisa ni wa kanda ya ziwa, anateua mtu kutokana na utartibu uliopo na weledi wa mtu husika katika kitengo husika...ts better mkamuacha afanye kazi kwa umakini ili atatue kero za wananchi kama ilani ya ccm inavyosema. So badiliken bana....alaaah.
jitetee wewe na nafsi yako, kwanini kutumia nguvu nyingi kutetea mwingine
 

Allen Kilewella

Verified Member
Sep 30, 2011
13,509
2,000
CCM ni kiboko kwa ubaguzi. Walipoona hawamtaki Mzee Marehemu Samuel Sitta wakasema ilikuwa ni " zamu" ya Mwanamke kuwa Spika. Sijui walitaka mzee wa watu akabadili jinsia(Transgender) ili awe mwanamke?
 

sembela

Member
Aug 8, 2013
67
95
Sio kweli...hizo ni propaganda za watu tu ambao hawaitakii mema ccm. By z way jpm hawez kuteua wasomi wote sasa eti ili tu kubalance upande flani. Na huwa aangaliii dini ya mtu wala kabila au anatoka wapi maana hawaendi kufanya kazi za kidini/ wala za kimila serikalin...yy anamteua mtu kutokana na sifa na vigezo linganinshi na kazi ambayo anaenda kuifnya...tuache kuwa watu wa kupayuka tu bila kuwa na ufahamu mzur wa mambo.
 

Bishweko

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
2,562
2,000
Kinana bhana eti tunawateua makada tu kwenye nafasi za
RAS
DAS
D.C.
M.D.
RC
WOE
VEO
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom