Ubaguzi unaendelea kuitafuna CHADEMA

Ubaguzi unaendelea kuitafuna CHADEMA

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2013
Posts
5,536
Reaction score
2,268
Mwl. Nyerere alishawahi kusema, "dhambi ya ubaguzi haifi, inaendelea. Dhambi ya ubaguzi ukishakuitenda inaendelea, ni sawa na kula nyama ya mtu, ukila nyama ya mtu utaendelea tu.".

Kila siku dhambi ya ubaguzi inazidi kumea na kuimarika ndani ya CHADEMA kiasi kwamba kwa sasa wamefikia hata kuanza kutesa baadhi ya watu ili kuendeleza dhambi ya ubaguzi.

Viongozi wa CHADEMA kila siku wanapanda kwenye majukwaa na kujigamba wakisema baadhi ya waajiriwa wa Usalama wa Taifa wanawapa siri za serikali na CCM lakini wanasahau kuwa, maneno yao yanachagiza Karma Law inayosema, What goes around comes around or as you sow, so shall you reap.

Viongozi wa CHADEMA walishawahi kunukuliwa kwenye mikutano katika thread hii;

CHADEMA wanafurahi sana kudai wanapewa siri za Serikali au CCM na baadhi ya waajiriwa wa Usalama wa Taifa lakini wanakuwa wa kwanza kutoa malalamiko na kudai wanahujumiwa pale siri zao zinapochukuliwa na watu hao hao wanaodai wanawapa siri za serikali au CCM. Waingereza wanasema, Don't hate the player, hate the game!

Unapopewa lazima pia ufahamu kuwa utatoa kwa njia hiyo hiyo iliyotumika katika kupewa. This is natural justice!

Baadhi ya viongozi wakuu wa CHADEMA ni ruksa kuwasiliana na baadhi ya wana usalama wa taifa (TISS) lakini mwanaCHADEMA mwingine akifanya hivyo hukumu yake ni kuteswa ndani ya ofisi za Red Brigade.

Baadhi ya viongozi wakuu wa CHADEMA ni ruksa kuwa na rafiki au ndugu ambaye anafanya kazi katika idara ya Usalama wa taifa, lakini mwanachama mwingine akionekana hata anapanda gari ya mfanyakazi wa usalama wa Taifa adhabu yake ni kuteswa na kufukuzwa uanachama.

Baadhi ya viongozi wakuu wa CHADEMA ni ruksa kuwa na namba za simu za viongozi wa CCM au serikali lakini mwanachama mwingine akiwa pia na namba hizo hizo anaitwa msaliti.

Baadhi ya viongozi wakuu wa CHADEMA huwa wanafanya mawasiliano na Mwenyekiti wa CCM Taifa, lakini hao hao viongozi wakigundua mwanachama mwingine anafanya pia mawasiliano kama hayo, watamuita msaliti ambaye adhabu yake ni kufukuzwa ndani ya chama.

Hii haitokei kwa bahati mbaya bali kinachofanyika ni
endelezo la dhambi ya ubaguzi ambayo inaendelea kuitafuna CHADEMA.

Chacha Wangwe aliishabikia hali hii lakini mwisho wake ilimtafuna.

Zitto Kabwe, Prof. Kitila na Mwigamba waliishabikia hali hii mwisho wake imewatafuna.

Khalid Kagenzi pia aliishabikia kwa kuanzisha Red Brigade, mwisho wake imemtafuna karibia apoteze maisha yake wakati anateswa ndani ya ofisi za Red Brigade kama siyo wasamalia wema kupiga kelele kuomba msaada.

CUF na NCCR-Mageuzi walishabikia ubaguzi wa CHADEMA kwa mwamvuli wa UKAWA, kwa sasa umeanza kuwatafuna kwa kuanza kubaguliwa!. Neno UKAWA kwa sasa ni bidhaa isiyouzwa au kuuzika ndani ya midomo ya wanaCHADEMA baada ya kupata kile walichokuwa wanakitaka kwenye chaguzi za serikali za mitaa.


Ifahamike tu, leo ni kwa mwingine ndani ya CHADEMA lakini kesho ni kwako unayeendeleza ubaguzi huo ndani ya CHADEMA.
 
Tatizo sio kuwasiliana bali uwasiliana kwa sababu zipi?Kumuwekea mtu sumu?Kutoa siri za vikao?

Punguza upotoshaji na unafiki
 
Kutojitambua na unafiki ni vitu vibaya sana duniani.
 
Tatizo sio kuwasiliana bali uwasiliana kwa sababu zipi?Kumuwekea mtu sumu?Kutoa siri za vikao?

Punguza upotoshaji na unafiki
Ndugu,
Hata wewe Karma Law imeishafanya kazi yake baada ya kushabikia ubaguzi.

Nilishaeleza katika thread yangu hii;
Nilisema;
Ben Saanane alikaririwa akijenga hoja za kuitetea Kamati Kuu ya CHADEMA katika misingi ya Katiba, Kanuni, Itifaki na taratibu baada ya kumuadhibu Zitto Kabwe na ''kundi lake''.

Misingi hiyo hiyo ya Katiba, Kanuni, Itifaki na taratibu aliyokuwa anaitetea kwa nguvu zote ndiyo imekuja kumtandika tena yeye mwenyewe katika safari yake ya kutaka kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa BAVICHA-taifa.
Niliendelea kusema;
Fast forward mpaka August, 2014 tunakutana tena na comment za Ben Saanane akilalamika mpaka kutaka kwenda mahakamani kupinga Katiba, Kanuni, Itifaki na taratibu ambazo siyo muda mrefu alikuwa akizipigia chapuo. Hii imetokea baada ya kupigwa nyundo ya kifitini na kuachwa barabarani katika harakati zake za kutaka tena kuwa Mwenyekiti wa BAVICHA taifa.

Ben Saanane hakufahamu au alisahau kuwa The Law of Karma is in full swing!
 
Ndugu,
Hata wewe Karma Law imeishafanya kazi yake baada ya kushabikia ubaguzi.

Nilishaeleza katika thread yangu hii;

Nilisema;

Hili ndio tatizo la watu wanafiki.Kutetea kanuni na katiba inapotumika dhidi ya mwingine inamaanisha kwamba haiwezi kutumika dhidi yangu?

Mbona una mawazo primitive kiasi hiki?

Huyu nae eti amejenga hoja hapo juu.
 
MwanaDiwani

Hakika unaipenda chadema sana unaonaje tukikupa nafasi ya uenezi? Kwenye majukwaa lazima ndio ajenda yako kwenye vikao na mitandao ya kijamii ndio ajenda yako kuitangaza cdm hongera sana na karibu cdm.
 
Last edited by a moderator:
chadema bongo lala wamesahau usalama wa taifa walimzuia mbowe kwenda kwenye mazishi ya chacha wangwe kwa usalama wake
 
Ungeweza kujenga hoja yako bila kuita watu majina na kutanguliza hisia.

Nina mashaka kama unalimudu vyema jukwaa hili

Kauli zake ndani na nje ya chama ndizo zinadhihirisha ubaguzi wake wa dini na kabila, kwanini Mtei asitajwe kwa jina lake au ujumbe utamfikiaje Edwin Mtei?.Huyu mzee ni wa hovyo kabisa na ndio maana Nyerere alimtambua mapema kuwa ni kirusi akamtimua kazi katika utawala wake leo tunaona rangi yake halisi.
 
Hili ndio tatizo la watu wanafiki.Kutetea kanuni na katiba inapotumika dhidi ya mwingine inamaanisha kwamba haiwezi kutumika dhidi yangu?

Mbona una mawazo primitive kiasi hiki?

Huyu nae eti amejenga hoja hapo juu.
Ndugu,
Kama hiyo ndiyo hoja yako na unafahamu hivyo, kwa nini ulitaka kwenda mahakamani baada ya kanuni na katiba hiyo hiyo kutumika juu yako.

Kwa mantiki hii, nani mnafiki hapa kati yangu na wewe.
 
Hakika unaipenda chadema sana unaonaje tukikupa nafasi ya uenezi? Kwenye majukwaa lazima ndio ajenda yako kwenye vikao na mitandao ya kijamii ndio ajenda yako kuitangaza cdm hongera sana na karibu cdm.
Ndugu,
Wewe mwenyewe umepewa hiyo nafasi na wenye chama, utatoa wapi nguvu na uwezo wa kunipatia nafasi?

Kwanza ukionekana unaongea na mimi utaonekana na wenye chama kama msaliti ambapo adhabu yake ni kufukuzwa uanachama!
 
Ndugu,
Kama hiyo ndiyo hoja yako na unafahamu hivyo, kwa nini ulitaka kwenda mahakamani baada ya kanuni na katiba hiyo hiyo kutumika juu yako.

Kwa mantiki hii, nani mnafiki hapa kati yangu na wewe.

Mkuu MwanaDiwani swali zuri sana kwa huyo msaka tonge.Waka i Chadema inakataza wanachama wake kwenda mahakamani kutafuta haki wakati huo huo ni chama kinachoongoza kuwa na mawakili wengi wanaokitetea chama kwa kulipwa fedha za chama.Sasa sijui ni woga au kutojiamini kwa viongozi kunakopelekea kupinga wanachama wake kwenda mahakamani wakati hata Dr Slaa akiongopa ukitaka kufahamu uhalali/ ukweli kwa alichokisema utasikia akisema "NENDA MAHAKAMANI"
 
Last edited by a moderator:
Tatizo sio kuwasiliana bali uwasiliana kwa sababu zipi?Kumuwekea mtu sumu?Kutoa siri za vikao?

Punguza upotoshaji na unafiki

Kuwa mkweli japo utakugharimu sio kwakua wamesema maboss wako nawewe ufuate wewe unaamini hiyo sinema yakuwawa dr au nikiki tu kua mkweli japo utaitwa msaliti
 
Naona mnavyopapatikia uzi wa boss wenu, nasikia huwa anawapigia kabla ya ku-post!
Maboss wako CHADEMA kiasi kwamba, wanapata mpaka ulinzi wa kujifananisha kama Rais wa Tanzania!.

Ndani ya CCM hakuna boss bali kuna ndugu.
 
Cdm kisha kufa tyr wngi wao akili mgando,akili ndogo kuongoza akili kubwa tatizo ndo lilipoanzia hapo
 
tunavyosema usalama wa taifa sio lazima watoke ccm hata CHADEMA inausalama wa taifa tena wako makini kuliko hao wa ccm Ben sanane hebu waeleze hao magamba
 
Back
Top Bottom