Ubabaishaji wa katiba si jambo geni tz,kinachofuata!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubabaishaji wa katiba si jambo geni tz,kinachofuata!!!!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by CHIGANDA, Mar 3, 2012.

 1. C

  CHIGANDA New Member

  #1
  Mar 3, 2012
  Joined: Mar 3, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Niwafahamishe watanzania ya kuwa,Jamhuri ya muungano wa Tanzania ni nchi kubwa sana. Mfumo wa utawala wa nchi ikiwa ni pamoja na ukubwa wake unatoa mwanya kwa 'wafalme wa mwitu' kuwa na kila sifa ya kuhidhinisha ufisadi nchini. Niliwahi kusema katika kongamano la katiba lililofanyika ubungo plaza mwaka jana nikiitaarifu serikali kipofu inayolazimisha kuwaongoza wanaoona.

  Niwape pongezi serikali kwa kutoa kipaumbele ktk elimu kwa kujitahidi kujenga shule nyingi na taasisi lukuki zinazotoa kada mbalimbali za elimu. Lakini niwasikitie kwa kutojua ni athari gani watapata kwa kutoa elimu hii.Nadhani wameshau kuwa wanajitahidi kuleta kizazi elevu ambacho ni chachu ya kupinga maovu ya vipofu hawa. Ikiwa watashikilia msimamo wao wa kifisadi,wawe tayari kushuhudia mataifa zaidi ya ishirini yakidai uhuru ndani ya BARA LA TANZANIA.

  Tuko tayari kupambana ili kila mkoa uwe na sauti binafsi kwa maslahi ya watu wa mkoa huo,na kwa jinsi hii tutakuwa tumepunguza madaraka ya raisi mjaza mifuko ya mafisadi. NiwafamiShe pia yakuwa, nina hasira sana kwa kuwaona wanachi wa mkoa wa mara hususani wilaya ya bunda inayoongoza kwa umaskini ktk wilaya zote tanzania 'kwa mujibu wa takwimu za serikali kipofu isiyo na aibu' pamoja na ukweli kwamba mbunge wa jimbo hilo ni miongoni mwa vigogo maarufu wanaoongoza kwa ufisadi na rushwa bwana STEVEN WASIRA.

  Napenda kumpa taarifa ya kwamba ninafahamu kuwa yeye siyo mbunge halali wa jimbo hilo kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi uliopita kwani kaingia madarakani kwa kutoa rushwa ya pesa ambayo ni mali ya walipa kodi wa wilaya hiyo.2015 ni uchaguzi unaochagizwa na mabadiliko ya katiba,salaam FISADI WASIRA,usithubutu hata kuonekana kwenye kampeni kwani nitakuwa karibu kabisa na wananchi wa Bunda nikianika maovu yako kwa ushahidi,na wala usithubutu kumsimamisha fisadi yeyote kutoka CHAMA CHA MAFISADI(CCM).

  Huna jipya zaidi ya kuligeuza bunge kuwa MASTER BED ROOM.
   
 2. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Bila shaka wewe ni mwanaharakati.
   
Loading...