Ubabaishaji wa bodi ya mikopo

vonmadiwa

Member
Apr 20, 2015
89
11
Wanachuo wote wanaonufaika na Mkopo kutoka bodi ya Mikopo HESLB kisheria wana mkataba Wa kudumu na bodi hiyo wa kupewa Mkopo kwa wakati.

Cha kushangaza sana bodi ya Mikopo bila sababu zozote za msingi hawatoi Mkopo huo kwa wakati, kisheria ni kosa kubwa sana kwani bodi ya Mikopo wanakiuka mkataba waliosaini na wanafunzi.

Kwa mfano kwa sasa hivi kuna zaidi ya College's 50 hawajapata pesa ya mafunzo kwa vitendo na tafiti,baadhi yao wameshafanya tafiti kwa taabu kubwa na wameshamaliza Chuo.

Hawa wanaofanya mafunzo kwa vitendo wanaendelea kudhalilika huko waliko kwani hawana fedha za kuratibu zoezi hilo, bodi ya Mikopo ndio inawajibika kudai pesa hazina sio wana Chuo.

Bodi wanakuwaga na majibu ya kawaida sana ,ukiwauliza wanasema hazina hawajatupa pesa, kwa mfano, wanachuo wa Smmuco wameenda field tangu jumatatu bila pesa ,wanahangaika sana hata mahala pa kujihifadhi hawana.

Yaani kwa kifupi wanafanya field katika mazingira magumu sana, bodi ya Mikopo ichukue hatua madhubuti kumaliza tatizo hili haraka maana mnajitia aibu sana.
 
Back
Top Bottom