Uaskofu unazidi Ukardinali

MdogoWenu

JF-Expert Member
Dec 23, 2009
555
915
HIVI karibuni, gazeti la Daily News (ISSN 0856-3812, No. 11,152) katika ukurasa wake wa mbele liliandika hivi, (.."in D'Salaam, the Head of Roman Catholic Church in Tanzania, Polycarp Cardinal Pengo, trumped wisdom for personal gratification and welfare of the nation at large"..).

Jioni Machi 14, 2014, nilimsikiliza Januari Makamba akitoa mchango wake wa maoni kwenye Bunge la Katiba. Wakati anahitimisha, alituasa tuheshimu maoni ya viongozi wa dini waliopendekeza Serikali mbili, akiwemo Polycarp Kardinali Pengo.

Hii ilikuwa wiki moja baada Samuel Sitta kuwatembelea Polycarp Kardinali Pengo pamoja na Mufti wa Tanzania, Issa Shaaban Simba.

Kwa asiyeujua muundo wa Kanisa Katoliki, ikitangazwa kwamba Samuel Sitta katoka kwa Mufti kisha amekwenda kwa Polycarp Kardinali Pengo, ni rahisi kudhani ilikuwa ni ziara ya kuwatembelea viongozi wa dini wa ngazi ya kitaifa.

Hata mimi utotoni nilikumbatia dhana kwamba, Laurean Kardinali Rugambwa ndiye aliyekuwa Mkuu wa Kanisa Katoliki nchini, kwani aliwapa daraja maaskofu 26, wakati Polycarp Kardinali Pengo amekwishawapa maaskofu 24.

Nilipokumbatia dhana ya pili kwamba Mkuu Kanisa nchini ni Rais wa Baraza la Maaskofu, nikajiona nimetumia hoja ya kisomi zaidi!

Nilipoanza kusoma nyaraka rasmi za kanisa, hasa Sheria za Kanisa ziitwazo "Code of Canon Laws", ndipo nikagundua sikuwa na ukweli wowote katika zile dhana mbili.

Hizi "Canon Laws" ibara zake hutajwa hivi, Can. 381, zinatosha kumwelewesha yeyote muundo wa Kanisa Katoliki. Zinataja mamlaka ya askofu, askofu-mkuu, kardinali, rais wa baraza la maaskofu na zaidi.

Hakuna ibara inayoonyesha kwamba kuna "mkuu wa kanisa", au "msemaji wa kanisa" katika nchi yoyote.

Kinyume chake, sheria ya kanisa, Can. 381(1) na Can. 391(1), zinasema kwamba askofu jimboni, ndiye mkuu na mwenye madaraka jimboni.

Ibara hii inatokana agizo la mkutano wa maaskofu uitwao Vatican II, uliotoa hati iitwayo "Lumen Gentium" ibara ya 27, isemayo kwamba, askofu jimboni ni mwakilishi wa Yesu na si mwakilishi wa Papa au chombo chochote.

Vilevile, hakuna andiko la kanisa linalotaja maneno "makao makuu". Badala yake jengo la kanisa liitwalo "Cathedral" ndilo lenye mamlaka ya uaskofu.

Kwa wale wanaopenda neno "makao makuu", basi afadhali waseme "Cathedral" ndiyo "makao makuu" ya kanisa jimboni.

Pale Roma, "Cathedral" ni kanisa liitwalo "St. Lateran's archbasilica". Kumbe, makao "makuu ya Kanisa Katoliki duniani", siyo anakoishi Papa yaani kule Castle Gandolfo au pale Vatican, bali ni hapo "St. Lateran archbasilica".

Hata kanisa maarufu lililopo Vatican, yaani "St. Peter's basilica", lina hadhi ndogo iitwayo "basilica", wakati hili la "makao makuu" linaitwa "arch-basilica", hadhi kubwa kuliko makanisa yote Katoliki duniani.

Ibara ya 390 na 436(3) ya sheria za kanisa, zinamkataza askofu (bishop) pamoja na askofu-mkuu (arch-bishop) wasiendeshe misa kwenye "Cathedral" bila ruhusa ya askofu mwenye jimbo.

Hivyo, Polycarp Kardinali Pengo au askofu Tarcicius Ngalalekumtwa, hawawezi kuendesha misa kwenye "Cathedral" ya Ifakara, bila kwanza kuruhusiwa na askofu Salutaris Libena.

Pia, kwa kutumia sheria, Can. 763, askofu wa jimbo, mfano pale Ifakara, amepewa mamlaka na Papa kumpiga marufuku askofu yeyote duniani asihutubie lolote jimboni Ifakara ikihitajika kufanya hivyo.

Mwaka 2004, Joachim Kardinali Meisner, alitumia ibara hii kumkataza askofu Jacques Gaillot asiingie jimboni Cologne, kwani alikwishachokwa kuigawa nchi kwa kauli zake alizoziita "ni maoni yake binafsi".

Nimechagua ibara hizi chache kuonyesha mamlaka ya askofu, uone kwamba, hakuna askofu hata mmoja nchini aliye juu ya mwingine.

Sasa tuone ukardinali ni nini?

Mkatoliki akitaka utumishi wake utambulike rasmi kikanisa, lazima atasajiliwa au kusimikwa kwenye kundi linalotambulika. Mara nyingi huwa ni jimboni au kwenye jumuiya ziitwazo "religious".

Zamani kila aliyesimikwa hivyo aliitwa "kardinali". Lakini kuanzia karne ya tisa, neno "kardinali" lilibaki kutumika tu kwa walioitwa na Papa wakahamia na kusimikwa upya Roma.

Padri aliyehamishiwa Roma, huko alisimikwa kwenye kanisa lililoitwa "titular church". Hiyo ikawa aina ya kwanza ya makardinali, wakijulikana kama "cardinal-Priest".

Baadaye mashemasi nao wakawa wanahamishiwa Roma, huko wakapewa vituo vilivyoitwa "deaconia". Ikawa aina ya pili ya makardinali waitwao "Cardinal-Deacon".

Kazi za Papa zilipoongezeka, akahitaji msaada wa maaskofu kutoka majimbo jirani yaliyoitwa "Suburbicarian Diocese". Hali ya maaskofu hawa kuwa karibu na kuhitajiwa Roma, kukawafanya waitwe "Cardinal-Bishop".

Hizi ndizo aina tatu za makardinali. Zipo hadi leo, yaani "Cardinal-Deacon", "Cardinal-Priest" na "Cardinal-Bishop".

Kuanzia mwaka 1150, Papa alianza kuwaita makardinali kwenye vikao vya kumshauri, ambavyo hadi leo vinaitwa "Consistory".

Mwaka 1179, haki ya kumchagua Papa mpya, ikaacha kuwa ya wanajimbo wengine wa Roma, bali ikabaki kwa "makardinali" tu kwenye mkutano unaoitwa "Conclave". Mwaka 1975, Papa Paul VI alifupisha umri wa kardinali kuhudhuria "Conclave", yaani chini ya miaka 80.

Tumeona kwamba, kitendo cha kupewa ukardinali na Papa, ni uhamisho wa kwenda Roma. Uhamisho huo unamfanya awe mwanajimbo wa Roma, ambaye kama haishi Roma, basi kokote aliko duniani anafanya umisionari.

Ile aina ya "Cardinal-Bishops" bado hupewa lile kanisa liitwalo "Suburbicarian Diocese". Siku hizi "Cardinal-Deacons" hupewa hata yale makanisa, "titular church".

Ile aina ya "Cardinal-Priest", wengi hawaishi Roma kwa sababu ya umisionari wao mbali na Roma. Mmojawapo ni Polycarp Kardinali Pengo, anayeongoza Jimbo la Dar es Salaam, lililo kilomita 6043 kutoka Roma.

Je, mtu anapewa ukardinali baada ya kufikia ngazi ipi ya utumishi? Teodolfo Kardinali Mertel, alipewa ukardinali Machi 15, 1858 akiwa hajapata hata ushemasi. Machi 20, 1556 Reginald Kardinali Pole alikuwa ameshakuwa kardinali kwa miaka 20 na ameshashiriki "Conclave" tatu akiwa hajawa padri.

Kuanzia Februari 2, mwaka 1983, Papa John Paul II aliwapa ukardinali mapadri saba, waliobaki na upadri wao bila kuwa maaskofu.

Watano kati yao wameshafariki ambao ni Henri Kardinali de Lubac, Avery Kardinali Dulles, Aloys Kardinali Grillmeier, Joseph Kardinali Congar, Leo Kardinali Scheffczyk. Wawili kati yao wako hai, yaani Roberto Kardinali Tucci na Albert Kardinali Vanhoye.

Papa Benedict XVI, naye ana mapadri wanne aliowapa ukardinali bila kuwa maaskofu. Watatu wamekwishafariki, ambao ni Domenico Kardinali Bartolucci, Urbano Kardinali Navarrete, Umberto Kardinali Bett. Aliye hai ni Josef Kardinali Becker.

"Roman Curia" ni jopo linalomsaidia Papa kuendesha kanisa lote duniani. Karibu timu yote "Roman Curia" huripoti shughuli zake kwa "Secretariet of State".

Hivyo, "Secretariet of State" ana majukumu mazito ndani na nje ya Kanisa, kwani Papa anaweza kusifiwa au kulaumiwa ndani na nje ya kanisa kwa sababu tu ya utendaji wa huyu "Secretariet of State".

Nafasi hii ya "Secretariet of State" sasa inashikwa na Pietro Kardinali Parolin, aliyeachiwa na Tarcisio Kardinali Bertone.

Wote Kardinali Bertone na huyu Parolin ni maaskofu. Lakini mwaka 1848, nafasi hii ilisimamiwa vizuri na Giacomo Kardinali Antonelli, ambaye alikuwa shemasi tu hadi kifo chake Novemba 06, 1876.

Papa anaweza kumpa mtu ukardinali kwa siri, yaani "Cardinal in pectore". Serikali ya China ilipomfunga askofu Ignatius Kung Pin-mei wa Shanghai, haigundua kwamba akiwa humo gerezani alipewa ukardinali kwa siri mnamo Juni 30, 1979.

Kardinali yeyote, kama alivyo Polycarp Pengo, siyo mwakilishi wa nchi kama Tanzania, kwani, hakuna jimbo wala parokia inayoitwa Tanzania.

Tumeona kwamba ukardinali ni kuwa mwanajimbo wa Roma au jirani na Roma (suburbcarian). Hivyo, hata inavyoelekeza sheria ya kanisa, Can. 357(1), kardinali ni mwakilishi wa parokia yake pale Roma yaani "titular chuch", ambayo ya Polycarp Pengo pale inaitwa Nostra Signora de La Salette.

Lakini ibara hiyo 357(1), bado inamdhibiti kardinali kwamba, hata hiyo parokia yake pale Roma, haruhusiwi kuiingilia kiutawala, kiuendeshaji au kinidhamu.

Hivyo, eneo pekee duniani ambako Polycarp Pengo ana mamlaka ya uchungaji, utawala, uendeshaji au nidhamu, ni ndani ya mipaka ya Dar es Salaam tu (rejea, Can. 381(1).

Wakati mabaraza ya maaskofu yanashamiri duniani, baadhi ya maaskofu waliitaadharisha Vatican kwamba, ama baraza zima au rais wa baraza hilo, ataweza kujikuta anaingilia ukuu wao jimboni na kugeuka kuwa mkuu nchini.

Hivyo, Papa aliiweka ibara ya 455(4) makusudi kulinda huo ukuu wa askofu wa jimboni, ili asiingiliwe kwa namna yoyote na baraza zima au rais wa baraza la maaskofu.

Hivyo, ibara hii inatosha kukuthibitishia kwamba, rais wa baraza la maaskofu, si kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini, wala si mkuu wa maaskofu nchini.

Hivyo, Rais wa TEC, Askofu Tarcicius Ngalalekumtwa, naye eneo pekee la ukuu wake, ni mipaka ya Jimbo la Iringa tu.

Mkutano wa makardinali wote duniani na Papa yaani "consistory", hauna mamlaka ya kutoa tamko kisha liitwe kuwa ni la Kanisa Katoliki duniani. Huo ni mkutano wa askofu wa Roma na wanajimbo wake.

Wakati mkutano wa maaskofu wote duniani na Papa, ndicho chombo kikuu kupita vyote kiitwacho "magisterium", chenye mamlaka ya kuamua lolote ndani ya Kanisa Katoliki.

Ibara ya 1121 ya Katekism ya Kanisa Katoliki inasema, askofu haachi kuwa askofu hadi kifo chake, hata akijiuzulu madaraka.

Lakini ukardinali ni tofauti. Padri Louis Billot alikuwa kardinali kwa miaka 16 ,alipojiuzulu ukardinali Septemba 21, 1927, akaacha kuwa kardinali.

Hivyo, uaskofu ni nafasi ya juu zaidi na nyeti zaidi ndani ya Kanisa Katoliki, kuuzidi ukardinali.

Lakini, siku hizi, msemaji akishamtambulisha kardinali, anafuata askofu-mkuu, kisha askofu, baadaye mapadri na kuendelea, halafu mwishoni anasema "itifaki imezingatiwa"!

Tumeona kwamba "Secretariet of State" wa "Roman Curia", yaani Kardinali Antonelli, hata upadri hakuufikia. Tumeona, kwamba hata leo, wapo hai na wametajwa humu makardinali watatu ambao hata uaskofu hawajaufikia.

Pia, mifano mitatu ifuatayo nchini Albania, Switzerland na Italy, inakufahamisha kwamba Papa John Paul II, amewahi kufanya jimbo liwe na padri ambaye ni kardinali, wakati askofu wa jimbo hilo si kardinali.

Jimbo la Chur (Switzerland), halijawahi kuongozwa na askofu ambaye ni kardinali. Lakini padri Hans Urs von Balthasar wa humo, alitangazwa kwenye orodha ya makardinali Juni 28, 1988.

Mei 25, 1985, hayati askofu Antonio Mistrorigo wa Treviso (Italy), alishuhudia padri wake Pietro Pavan akipewa ukardinali wakati mwenyewe hakuwahi kuwa kardinali.

Novemba 26, 1994, hayati askofu Franco Illia wa Shkodre (Albania), alishuhudia padri wa jimbo lake yaani Mikel Koliqi akipewa ukardinali wakati yeye mwenyewe hakuwahi kuwa kardinali.

Kumbe, yaliyotokea Albania kwa Kardinali Koliqi, yanaweza kabisa kujirudia Tanzania, yaani padri wa jimbo moja tu nchini anakuwa kardinali, wakati hakuna askofu hata mmoja nchini aliye kardinali.

Hivi, ikitokea hivi, halafu huyo padri ambaye ni kardinali, akusanyike na maaskofu wote nchini ambao si makardinali, je, wapenzi wa ile "itifaki", wataizingatia vipi ile itifaki yao?

Ukitaka kuvijua "vyeo" ndani ya Kanisa Katoliki, sharti utulie na kuvisoma.Vinginevyo, unaweza kuhutubia tuheshimu mawazo ya mwenye "cheo" fulani, ukidhani ndiye mkuu hapa nchini, kumbe sivyo.


Chanzo;Raia Mwema
 
Kwanini anasisitiza tuheshimu waliosema serikali mbili pekee?

Waraka ws TEC umesema maoni ya wananchi yaheshimiwe ambayo yapo kwenye rasimu ya tume. Maoni ya wananchi waliosema tuyaheshimu yaliyo kwenye rasimu, yaani serikali 3.

Katika waraka huo Pengo ameungana na Maaskofu wenzake 31 na wameupitisha.
 
Kwanini heading ya mada yako umanza na neno "kumbe"? That's the reality, kama ulikuwa unaenenda katika ujinga ukweli ndio huo. Ukadinali anaweza kupewa hata asiyekuwa mchungaji/padre. Nashangaa unashangaa juu ya hilo kwani mkristo yeyote anajua wazi kabisa cheo cha ukadinali hakitajwi popote katika Biblia Takatifu bali uaskofu pamoja na vingine kama uinjilisti, ualimu, uchungaji, n.k. Kibiblia, mwalimu ni mkuu kuliko kadinali.

Mwandishi wala hajakosea, Muadhama Polycarp Kadinali Pengo mamlaka yake yanaishia ndani ya mipaka ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam pekee kama ilivyo kwa maaskofu wengine ambao kiutendaji wanabanwa na mipaka ya majimbo yao. Jambo lolote ambalo Pengo atatakiwa kulifanya nje ya jimbo lake ni lazima apate ruhusa ya askofu husika.

Hivyo kimsingi, Pengo alivyodakia haraka haraka kwamba kauli ambayo aliwahi kuitoa kuhusu kuunga kwake mkono serikali mbili ni "kauli yake binafsi" alikuwa anafahamu fika utaratibu wa Kanisa na angeweza kuingia matatani endapo angelisemea Kanisa Katoliki Tanzania kwani hana mamlaka hayo asilani. Lakini kwa wale wasioelewa au kwa sababu zao binafsi baadhi ya waandishi walihanikiza eti ni kauli ya Kanisa!

Hata yule "chizi" aliyewahi kusema ni "chaguo la Mungu" ilikuwa ni kauli yake binafsi ingawa watu wa aina hii wasipodhibitiwa wanaweza kuleta matatizo makubwa ndani ya jamii kwa kauli zao "binafsi".
 
Kwa maana hiyo mkuu wa Kanisa katoliki Tz ni nani hasa?

Hivi aliyekuambia Kanisa Katoliki Tanzania (au nchi nyingine yoyote) lina mkuu wake ni nani? Kwa haraka haraka (mimi sio mtaalamu wa mambo ya Kanisa Katoliki anyway) utawala wa Kanisa unaanzia kwa Pope (Mrithi wa Kiti cha Mtume Petro) => Jimbo (Askofu) => Parokia => Vigango => Jumuiya => Familia (Mwanaume na Mwanamke wenye ndoa takatifu Katoliki) => Mtu Binafsi (anayekiri imani Katoliki).

Hakuna kitu kinachoitwa "Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania".
 
Asante mdogo wetu kwa ufafanuzi mzuri. Mkatoliki mimi sikuyajua haya.
 
Hivi aliyekuambia Kanisa Katoliki Tanzania (au nchi nyingine yoyote) lina mkuu wake ni nani? Kwa haraka haraka (mimi sio mtaalamu wa mambo ya Kanisa Katoliki anyway) utawala wa Kanisa unaanzia kwa Pope (Mrithi wa Kiti cha Mtume Petro) => Jimbo (Askofu) => Parokia => Vigango => Jumuiya => Familia (Mwanaume na Mwanamke wenye ndoa takatifu Katoliki) => Mtu Binafsi (anayekiri imani Katoliki).

Hakuna kitu kinachoitwa "Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania".

well said
 
Hivi aliyekuambia Kanisa Katoliki Tanzania (au nchi nyingine yoyote) lina mkuu wake ni nani? Kwa haraka haraka (mimi sio mtaalamu wa mambo ya Kanisa Katoliki anyway) utawala wa Kanisa unaanzia kwa Pope (Mrithi wa Kiti cha Mtume Petro) => Jimbo (Askofu) => Parokia => Vigango => Jumuiya => Familia (Mwanaume na Mwanamke wenye ndoa takatifu Katoliki) => Mtu Binafsi (anayekiri imani Katoliki).

Hakuna kitu kinachoitwa "Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania".

Umefafanua vizuri mpaka basi, hapo roho swaaaaafi!
 
Kaka umezama duu...kwa maana hiyo hata pengo anatuchanganyi HAWI muwazi ktk mipaka ya uongozi wake Watanzania wengi tunajua yeye ni boss kanisa katoriki tz...big up kwa sana
 
Thread ina mengi ya kujifunza na kuelewa. Sasa ngoja aje jini kahtaan na majini wenzake waichafue
 
Last edited by a moderator:
Thread ina mengi ya kujifunza na kuelewa. Sasa ngoja aje jini kahtaan na majini wenzake waichafue

Teh teh teh!

Kuna jamaa hapo juu ameandika kuwa kulawitiwa kunazidi kubakwa!
Kwa hio sidhani km kuna cha ajabu hapa!
 
Last edited by a moderator:
Wakatoliki ni wabaya sana!
Wanawabagua wakristo wote wasii wakatoliki!
Mkuu Ntuzu hawa wabudu masanamu unawaongeleaje?
Manake mi nawaona kila mara wanavyo wabagua nyie.

Na nnadhani yule mchungwaji mpenda makalio Eiyer pia ni mkatoliki! Lkn hujifanya sio ili ale ile michango ya paroko tu!
 
Last edited by a moderator:
We need separation of church/ religion and state, in practice.

Not this lip service bullshit we see.
 
Tanganyika Waisilamu ndio wengi zaidi kuliko Wakristo lakini serikali ina Wakristo wengi kuliko Waisilamu.

Kwa hiyo ukiitizama Tanganyika kwa jicho la woga utajidanganya na kuhisi Wakristo ndio wengi kumbe ni kinyume chake. 🚲
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom