Uanzishaji wa kiwanda cha Tomato Source

Uanzishaji wa kiwanda cha Tomato Source

MrIsidori

Senior Member
Joined
Apr 3, 2014
Posts
191
Reaction score
83
Naomba anayejua jinsi ya kutengeneza tomato sorce na utaratibu wa kuanzisha kiwanda chake, gharama za uanzishaji. utengenezaji na uendeshaji, nyanya nitaanzisha shamba la greenhouse, aksanteni.
 
Point of correction. Ni Tomato Sauce not sorce
 
check alibaba utapata machine kibao kubwa na ndogo kadri ya uwezo wao
 
Pritty hata mimi natamani kuanzisha hicho kiwanda kidogo cha Tomato sauce cause tayari nina greenhouse ila soko bovu sana una hakika na mashine hiyo ya kusagia nyanya huko SIDO au unao mwanga kidogo wa bei yake ebu niondolee tongotongo basi
 
Hebu fungua hicho kiwanda uokoe jahazi maana nyanya ni nyingi na soko hakuna...

Ova
 
Tafiti zaidi,maana Usidhani Nyanya zipo nyingi Hapa nchini,Kiwanda cha Dabaga wanalazimika kuimport Tomato paste miezi 6 kwa Mwaka,kipindi cha uhaba wa Nyanya.Hizi unazosikia Dodoma na Kwingineko hazijawa nyingi za Kutosha Kiwanda.Pili vema ukachagua Kazi moja,ili uwe efficient,aidha ulime au Uchakate (Specialisation ni Mhimu kwa Ufanisi)
 
Ni nyema unawa na subira kidogo, ukatafiti unahitaji mzigo kiasi gani (raw materils) wa aina gani (ubora), kabla hujafungua hicho kiwanda. Unaweza ona nyanya ni nyingi lakini kiwanda kitakapoanza ukashangaa huna mzigo. Nyanya kwa kawaidia huwa nyingi kuanzia June Mwishoni hadi September mwanzoni hapo ndio bei huporomoka sana, baada ya hapo huanza kuwa adimu mpaka mwezi march. Kuna watu wanaitwa Darsh Industrial wamejenga kiwanda kikubwa sana iringa hapo km kama 5 hivi kutoka stend ipogolo kama unakuja mbeya mkono wa kushoto just after Ebeneza SEC, waliambiwa nyanya ni nyingi sana Iringa tatizo ni soko. Wamemaliza ujenzi nyanya hakuna, sasa hivi wanaplan kuwa na mashamba yao kama eka 200 hivi wapende nyanya zao wenyewe maana wasipokuwa makini kuna kipindi watakuwa wanafunga kiwana kwa kukosa mzigo. Chukua muda kutafiti usikimbilie tu kila unaloambiwa.
 
mkuu,
Naomba anayejua jinsi ya kutengeneza tomato sorce na utaratibu wa kuanzisha kiwanda chake, gharama za uanzishaji. utengenezaji na uendeshaji, nyanya nitaanzisha shamba la greenhouse, aksanteni.
ulifanikiwa??
 
Back
Top Bottom