Uandishi gani huu wa kibaguzi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uandishi gani huu wa kibaguzi?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 8, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 8, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Na Ramadhan Semtawa (Mwananchi)


  ZAIDI ya asilimia 90 ya uchumi wa Tanzania unaendelea kumilikiwa watu wenye
  asili ya Asia na Ulaya, takwimu zinaonyesha.  Takwimu hizo zimetolewa huku kukiwa na kilio kikubwa cha Watanzania
  wazawa, kutaka wajengewe mazingira mazuri ya uwezeshaji ili kumiliki uchumi wa nchi kupitia migodi mikubwa ya madini na maeneo nyeti ya kiuchumi.  Lakini wakati kilio hicho kikiwa hakijapata ufumbuzi, Taarifa ya Utendaji ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji
  Wananchi Kiuchumi, iliyowasilishwa katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi jana, ilisema watu wenye asili ya mabara ya nje wanaomiliki uchumi wa Tanzania ni sawa na asilimia moja ya Watanzania.  Takwimu hizo zilifafanua kwamba, asilimia hiyo 90 ya uchumi wa nchi umeshikwa na watu w
  enye asili ya Asia na Ulaya, wakati asilimia 99 ya Watanzania wazawa, hawana kitu.  Kwa mujibu wa takwimu hizo zilizowasilishwa katika kikao hicho kilichohudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Omar Yusuph Mzee, tatizo la
  Watanzania weupe kumiliki uchumi, lilianza tangu wakati wa ukoloni.  "Wakati wa enzi za ukoloni na hata baada ya uhuru Watanzania wengi hawakuwa wakishiriki kikamilifu katika kumiliki uchumi wa nchi yao. Uchumi wa nchi umeendelea kutawaliwa na wageni wakishirikiana na Watanzania wachache," inasema sehemu ya ripoti hiyo.
  Ripoti hiyo inasema "asilimia 99 ya wananchi ni
  Watanzania weusi na asilimia 1 iliyobaki inajumuisha Waasia na Wazungu ambao wana miliki zaidi ya asilimia 90 ya uchumi wa nchi hii (Msambichaka, 2008).  "Hii ina maana asilimia 99 ya
  Watanzania halisi wanamiliki asilimia 10 tu ya uchumi wa taifa lao," inasisitiza ripoti.  Kwa mujibu wa ripoti hiyo, serikali imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali za kurekebisha kasoro zilizoko, ikiwa ni pamoja na kuanzisha (lililokuwa) Azimio la Arusha, Vijiji vya Ujamaa, Elimu ya Kujitegemea, Serikali za Mitaa, Vyama vya Ushirika, Sera ya Uwekezaji na Sera ya Ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma.
  Inasema hata hivyo,juhudi hizo hazijazaa matunda yaliyotarajiwa na kwamba na kwamba kushindikana kwa juhudi za kuwawezesha Watanzania kushiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa nchi yao, ndilo chimbuko la kubuniwa kwa mkakati wa kuwawezesha wananchi kiuchumi, katika ilani ya CCM ya mwaka 2000."  My Take:

  Kuna mtu katuroga tate nane!!!
   
 2. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #2
  Apr 8, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ni uandishi wa kibaguzi au ndio ukweli wenyewe?
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Apr 8, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Ndio ni wa kibaguzi.. kwa sababu hao asilimia moja walipoweza kushika uchumi kwa asilimia 90 hao asilimia 99 walikuwa wameshikiliwa bunduki kwenye vichwa vyao.. na ni nani aliyesema utanzania unahusiana na rangi au asili ya kijiografia?
   
 4. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #4
  Apr 8, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tupende tusipende utaifa unahusiana na asili ya kijiografia na rangi. Ndio maana afrika kusini, marekani na kwingineko kuna misuguano kwa sababu hiyo. Na ndio maana hata wayahudi walirudi kwao kutoka Misri. Hatuishi kwenye duni "perfect", tusijidanganye ati nitahamia Mongolia halafu hatimaye wajukuu wangu watachukuliwa kama wamongolia tu baadae, waapi?
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Apr 8, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,547
  Likes Received: 18,210
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji, facts are sturbon things!.
  Huo sio ubaguzi, bali ni bitter facts, tena hajaongeza kuwa magerezani kote tuko wenyewe, wenye rangi zao wakikutwa na hatia wanapigwa fine, mtashuhudia kwenye kiini macho cha kesi za Epa.

  Alichofanya Semtawa ni kuaplify that bitter reality.

  Kulihitajika affimative action maalum ya kuwa empower kina yakhe. Hili ndilo lilikuwa lengo la awali la ubinafsishaji, kuwa fedha za kuuza zile rasilimali zetu, zingewekwa mfuko maalum kuzitawanya kwa wazawa wanunue hisa na kuwa wamiliki. Sijua hata hizo fedha zilikwenda wapi maana huo mfuko, sikubahatika hata kuusikia.

  Wenzetu kwa Mandela wamefanya na wanaendelea kufanya hiyo affimative action kwa weusi. Hata huko mliko, USA, wana Black Empowerment, niliisoma enzi zile za Ebony zilipokuwa deal bongo, kuna tatizo gani tukiwaempower wazawa?.

  Tunakoelekea, ni wenye nacho kuzidi kuongezewa na wasio nacho kunyang'anywa hata kile kidogo walichonacho, Hii itapelekea kwa watoto wetu na watoto wa watoto wao kuishia kuwa wapangaji kwenye nchi yao kwa maisha yao yote, ila pia watafika mahali watasema basi! na hapo ndipo!.
   
 6. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #6
  Apr 9, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Pasco

  Hakuna nchi yoyote duniani iliyoendelea kwa kuwabagua raia wake kwa misingi ya rangi ya ngozi zao.

  Kwa sababu hoja inakubalijka kisiasa, haina maana ni sahihi na kwamba haitakuwa na madhara huko mbeleni. Sera za SA za kuwangeza idadi ya waafrika kwenye kumiliki uchumi zitakuja kuback fire iwapo hawatazingatia vigezo vingine muhimu kama elimu, uzoefu na uwezo.

  Kinachotakiwa ni kuwapatia raia wote huduma muhimu kwa haki na sheria zinazozingatia umoja; elimu, matibabu, maji n.k. Haya mambo ya nani anamiliki duka au kiwanda gani yatakuja kujirekebisha yenyewe huko mbeleni baada ya wato kuelimika.
   
Loading...