Uandikishaji wa BVR Njombe kumalizika Aprili

Uandikishaji wa BVR Njombe kumalizika Aprili

dubu

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2011
Posts
3,502
Reaction score
3,487
Dar es Salaam. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema mchakato wa uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura mkoani Njombe utakamilika Aprili 12.

Kwa mujibu wa taarifa ya NEC kwa vyombo vya habari, mashine za kielektroniki za Biometric Voters Registration (BVR), zinazotumika katika uandikishaji huo zina uwezo wa kuandikisha wapigakura kati ya 80 na 160 kwa siku.

Wakati uandikishaji huo ulioanza Februari 23 mwaka huu ukikamilika, kitendawili kinabaki kwa Nec kama itakamilisha uandikishaji kwa wakati kabla ya Aprili 30 mwaka huu ili kutoa fursa kwa Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa kufanyika.


Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva amekuwa akikaririwa mara kadhaa akisema ili kura ya maoni iweze kufanyika ni lazima watu wote wenye sifa wawe wameandikishwa.

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema jana kuwa: "Kura ya maoni kufanyika Aprili 30 ni kitendawili kwani muda uliobaki, kwa Tume haiwezi kumaliza kuandikisha nchi nzima."
Taarifa kwa umma iliyotolewa na Nec ilisema, baada ya kukamilika kwa uandikishaji itatoa ratiba ya mikoa mingine kuanza mchakato huo.

Kwa mjibu wa ratiba hiyo inaonyesha kuwa, Machi 3 uandikishaji ulianza Kata ya Kitandililo na utamalizika Machi 9. Kata ya Mahongole na Utengule utaanza Machi 11 hadi Machi 17. Machi 16 hadi Aprili 12 uandikishaji huo utaendelea Wilaya za Njombe, Makete, Ludewa na Wanging'ombe.

"Uandikishaji katika Kata tisa za Halmashauri ya Mji wa Makambako ulifanyika kwa ufanisi na mafanikio makubwa kutokana na kuvuka malengo kwa kuandikisha wapigakura 46,709 tofauti na tulivyopanga kuandikisha watu 32,370."

"Tunawaomba viongozi wa vyama vya siasa, asasi za kiraia na vyombo vya habari kuhamasisha wananchi wote wenye sifa za kujiandikisha katika Wilaya za Njombe, Makete, Ludewa na Wanging'ombe kujitokeza kwa wingi kujiandikisha," ilisema taarifa hiyo ya tume.

Iliongeza: "Tangu uandikishaji uanze katika Halmashauri ya Mji wa Makambako na kumalizika, wananchi wameonyesha mwamko mkubwa wa kujiandikisha."
Taarifa ya tume ilisema, mashine nyingi za kielektroniki za Biometric Voters Registration (BVR) zilifanya kazi kwa ufanisi mkubwa kutokana na kuandikisha wapigakura kati ya 80 na 160 kwa siku.

Chanzo: Mwananchi
 
Dubu bwana sasa mbona unamsahihisha Rais wako? Kwa maana hiyo watakaoweza kuipigia KURA katiba ni Wilaya ya Njombe tu? Maana come April 30 2015 ndiyo zoezi la kuipigia kura Katiba ya Chenge.Mbona sielewi? Maana hizi shule za kata ni shidaaaaaaaaaaa!
 
Timing ya kupiga kura ya referendum April 30 inaonekana ni mbinu ya kuhalalisha ulaji wa fedha uliofanyika kwenye BMK kiharamu.
Tume ya taifa ya uchaguzi haitaweza kuandikisha watu nchi nzima kwa ajili ya referendum.
Kama uandikishaji mkoani Njombe unaenda mpaka mwezi April,je,mikoa mingine tena yenye watu wengi utachukua muda gani?
Kirahisi ni kwamba haiwezekani kwa watanzania kupigia kura katiba pendekezwa mwezi ujao.Hilo haliwezekani.
Sasa hii timing ya uandikishaji kuanza,matumizi ya BVR na tarehe ya kupiga kura imetokea kwa bahati mbaya au makusudi.
Kwangu mimi naona ni makusudi.Katiba pendekezwa ilishanajisiwa kwa namna mbalimbali.Japokuwa maccm wenyewe ni najisi,hawawezi kuleta katiba ambayo itazidi kuwanajisi kama wao walivyoinajisi rasimu ya Warioba.
Kwa hiyo kujiandaa kutumia kushindwa kwa NEC kuandikisha kama mwavuli haikubaliki.
Tunataka maccm kwa ujasiri uleule wapige kura tar 30April.
Wasipopiga,watuambie ni kwanini walikula hela zetu bila kufanya tathmini ya uwezekano wa kupiga kura!
Kwa njia zilezile haramu mlizotumia kwenye BMK,zitumieni mpigie kura katiba yenu ya vijisenti.
Kama mliweza kuwapigisha kura marehemu,hatutarajii mtakosa mbinu hata sasa!
 
Una hasira kaka.Mbona hata uhakika wa uchaguzi mkuu haupo? Imagine hapo ni njombe tu mwezi mzima, hesabu tuana mikoa mingapi na mashine ndiyo hizo 250 na wale wanaotugawia KODI ZA Wananchi wao wamegoma kuzitoa niambie kama uchaguzi upo.Na mwaka huu Prof atatawala mpaka 2018 mpo? Hawajamaliza kujilimbikizia mali si unajua tena ukoo mkubwa ule.
 
mbowe aliwambia wakamuona mjinga haya sasa mmeona wenyewe tuone kama hiyo kura ya maoni ya tarehe 30 itafanyika ikiwa mkoa mmoja tu umeanza tarehe 3 march hadi tarehe 12 april
 
Chama Cha Mapinduzi wanaelekea kuingiza nchi katika sintofahamu kuhusiana na masuala ya KATIBA, UANDIKISHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA, KUPIGA KURA KATIBA INAYOLAZIMISHWA na UCHAGUZI MKUU.

Ni dhairi mkaidi hafaidi hata siku ya idi, na faida ya mjinga kuumia. kama ilivyokuwa katika mchakato wa katiba ndivyo itakavyokuwa katika hatua za kuhitimisha mchakato. maCCM hayana uzalendo, ari wala kujali maslahi ya nchi.
Mazingira ya nchi yetu sasa ni dhairi amani na utulivu tunavyojivunia ni matokeo kundi linalonyanyasa kuwa na moyo wa uvumilivu na subra.

Lukuvi, Wassira, Nape hawana busara ya kuhakikisha amani na ustawi wa taifa letu
 
mbowe aliwambia wakamuona mjinga haya sasa mmeona wenyewe tuone kama hiyo kura ya maoni ya tarehe 30 itafanyika ikiwa mkoa mmoja tu umeanza tarehe 3 march hadi tarehe 12 april
Tena mkoa wenye idadi ndogo ya watu. Lakini si vifaa vingine vinakuja ili mikoa yote ifanyike kwa pamoja? Pengine bado yawezekana, tuvute subira ingawa inatupa taabu kupanga mipango yetu
 
Mbona hamueleweki? mara mnataka mara amtaki!
 
Dubu bwana sasa mbona unamsahihisha Rais wako? Kwa maana hiyo watakaoweza kuipigia KURA katiba ni Wilaya ya Njombe tu? Maana come April 30 2015 ndiyo zoezi la kuipigia kura Katiba ya Chenge.Mbona sielewi? Maana hizi shule za kata ni shidaaaaaaaaaaa!
yes Wapige wow tu watuwakilishe.
 
yes Wapige wow tu watuwakilishe.

Baada ya hapo utawapeleka kwa Hakimu aliyepokea ESCROW ACCOUNT.Sijui kitakachoendelea.Na baada ya Bunge la Bajeti hakuna bunge lingine yaani bunge linavunjwa rasmi.Jamani mie na shule za kata zangu hizi.Hebu nikauze Icecream zangu mie....
 
Kwani kazi ya bunge maalumu la katiba ni kupiga kura?
 
Jana nilimuona yule dr. Wa mifumo ya kielectronic kutoka tume ya uchaguzi, alikuwa katika kipima joto cha itv jana. Alibanwa mbavu mno na marcus albanie, na mzee masako kuhusu je watakamilisha hili zoezi kabla ya april 30 nchi nzima?? Akaaaanza ahaa, unajua, so.. Kuna charter plane italeta labda kiti 250, mara italeta labda 400 hivi, tutaround mikoa 20 at once, ahaaa unajua hizo mashine zina lithium sasa lithium hairuhusiwi kusafirishwa na abiria... Bla blaaaah......watu wakamuuliza je unauhakika hizo mashine zilizobaki huko zaidi ya 7850 ambzao hazijaja zimeshalipiwa?? Anatoa toa macho kama mjusi..nikajua tu hapa tayari tumeliwa.. Jk anaendesha nchi kisanii sana mamlaka ya kutangza tarehe ya uchaguzi ni ya tume, sasa yeye kaipangia tume muda matokeo yake vifaa hakuna, wataalamu wa kuandikisha shida tupu.. Inafikia hatua mashine zinabuma inabidi wawapigie wazungu wenyewe waliozitengeza, yes, no , okay okay kibao.... Tumeliwa hili suala la katiba ya chenge na sitta, tukicheza hata uchaguzi utaahirishwa, yaani sherehe za muungano fedha zipo, sherehe za 9 dec pesa zipo, nyerere day pesa zipo, ila suala la kuleta bvr kit halikuandaliwa bajeti huku wakijua mwaka 2015 tuna uchaguzi.. Jk maliza uondoke zako; umetulet down sana watanzania, ndio maana nyerere alikwambia bado u mdogo, zamu yako bado.. Kumbe alikuwa na maana pana sana zaidi ya hiyo.
 
Hatutaki kupiga kupigia kura kitu najisi.
Tunachotaka ni kuona manajisi yakikamilisha unajisi wao kwenye chema walichokinajisi.
Tumieni mbinu zozote mlizonazo mpige kura.
Mbona hamueleweki? mara mnataka mara amtaki!
 
Jana nilimuona yule dr. Wa mifumo ya kielectronic kutoka tume ya uchaguzi, alikuwa katika kipima joto cha itv jana. Alibanwa mbavu mno na marcus albanie, na mzee masako kuhusu je watakamilisha hili zoezi kabla ya april 30 nchi nzima?? Akaaaanza ahaa, unajua, so.. Kuna charter plane italeta labda kiti 250, mara italeta labda 400 hivi, tutaround mikoa 20 at once, ahaaa unajua hizo mashine zina lithium sasa lithium hairuhusiwi kusafirishwa na abiria... Bla blaaaah......watu wakamuuliza je unauhakika hizo mashine zilizobaki huko zaidi ya 7850 ambzao hazijaja zimeshalipiwa?? Anatoa toa macho kama mjusi..nikajua tu hapa tayari tumeliwa.. Jk anaendesha nchi kisanii sana mamlaka ya kutangza tarehe ya uchaguzi ni ya tume, sasa yeye kaipangia tume muda matokeo yake vifaa hakuna, wataalamu wa kuandikisha shida tupu.. Inafikia hatua mashine zinabuma inabidi wawapigie wazungu wenyewe waliozitengeza, yes, no , okay okay kibao.... Tumeliwa hili suala la katiba ya chenge na sitta, tukicheza hata uchaguzi utaahirishwa, yaani sherehe za muungano fedha zipo, sherehe za 9 dec pesa zipo, nyerere day pesa zipo, ila suala la kuleta bvr kit halikuandaliwa bajeti huku wakijua mwaka 2015 tuna uchaguzi.. Jk maliza uondoke zako; umetulet down sana watanzania, ndio maana nyerere alikwambia bado u mdogo, zamu yako bado.. Kumbe alikuwa na maana pana sana zaidi ya hiyo.
Umenchekesha sana mdau,jamaa umemnukuu usanii wake,nao huwa hawana Hoja ila wanaogopa kupoteza UGALI
 
Kama Mkoa mmoja ni zaidi ya mwezi na Tanzania inamikoa zaidi yaishirini na Tano.

Kuna hatari hadi uchaguzi mkuu daftari lisikamilike.!
 
umenchekesha sana mdau,jamaa umemnukuu usanii wake,nao huwa hawana hoja ila wanaogopa kupoteza ugali
yaani mkuu acha kabisa sikuamini kama yule jamaaa ni dr (degree 3), nina mashaka sana na hilo... Kwa sababu nilitegemea awe muwazi kabisa, sijui ni nini huwa kinatokea yaani hata mtu awe msomi mzuri vipi, muadilifu mcha mungu namana gani akiishachaguliwa tu na ccm katika nyazifa fulani baasi.,.. Anaanza kuwa muongo, 1 pulus 1 atasema 11, yaani ilimradi tu aonekane anaisaidia serikali kumbe watz wa leo wanaelewa sana, wakimuanglia kiongozi machoni tu wameshamjua hili bomu au laaa.. Hili zoezi limebuma serikali haina pesa, na hizo kit hazipo za kutosha na wataalalmu bado kabisa sasa mkoa kama njombe ambao hauna hata watu milioni 3 leo wanakaaa takribani mwezi hapo.. Je dar wataaa miezi mingapi??.. Kuna kura ya maoni hapoo??... Na tayari jana kuna mpiga simu mmoja alisema ccm wamepeleka wapuuzi wao kutoka kinondoni kwenda kuwalisha sumu watu wa tume ya uchaguzi jinsi ya kukataa kuandikisha watu hasa wa upinzani meneo ambayo ccm ilipoteza kura nyingi 2010, na uchaguzi wa serikali za mitaaa, sasa hapo kuna amani tena??
 
Jana nilimuona yule dr. Wa mifumo ya kielectronic kutoka tume ya uchaguzi, alikuwa katika kipima joto cha itv jana. Alibanwa mbavu mno na marcus albanie, na mzee masako kuhusu je watakamilisha hili zoezi kabla ya april 30 nchi nzima?? Akaaaanza ahaa, unajua, so.. Kuna charter plane italeta labda kiti 250, mara italeta labda 400 hivi, tutaround mikoa 20 at once, ahaaa unajua hizo mashine zina lithium sasa lithium hairuhusiwi kusafirishwa na abiria... Bla blaaaah......watu wakamuuliza je unauhakika hizo mashine zilizobaki huko zaidi ya 7850 ambzao hazijaja zimeshalipiwa?? Anatoa toa macho kama mjusi..nikajua tu hapa tayari tumeliwa.. Jk anaendesha nchi kisanii sana mamlaka ya kutangza tarehe ya uchaguzi ni ya tume, sasa yeye kaipangia tume muda matokeo yake vifaa hakuna, wataalamu wa kuandikisha shida tupu.. Inafikia hatua mashine zinabuma inabidi wawapigie wazungu wenyewe waliozitengeza, yes, no , okay okay kibao.... Tumeliwa hili suala la katiba ya chenge na sitta, tukicheza hata uchaguzi utaahirishwa, yaani sherehe za muungano fedha zipo, sherehe za 9 dec pesa zipo, nyerere day pesa zipo, ila suala la kuleta bvr kit halikuandaliwa bajeti huku wakijua mwaka 2015 tuna uchaguzi.. Jk maliza uondoke zako; umetulet down sana watanzania, ndio maana nyerere alikwambia bado u mdogo, zamu yako bado.. Kumbe alikuwa na maana pana sana zaidi ya hiyo.

You are right, nilikaona kale kamdada kababaishaji tu, hakawezi kuwa Expert kale! kalipandikizwa kuzuga kipindi, hawana pa kutokea mwaka huu, janja zao zote ziko ukingoni. Freedom is coming tomorrow, Let freedom reign, Aluta Continua.
 
kumbukeni pia Njombe ilimegwa kutoka Iringa,ingekua bado ni mkoa mmoja wangemaliza july.
 
Back
Top Bottom