Wanajamii taarifa ya ndani kabisa kutoka jikoni inasema kuwa NEC haitaweza kuorganize kura ya maoni ya katiba pendekezwa hapa April 30,2015.Mpaka leo tume ina mashine 250 tu ya BVR out of 15000.Katikati ya mwezi huu tutapata machine zingine 3000 tu.Sasa kwa hali hiyo ni hesabu ndogo ambaye hata madenge na kipepe wanakujibu vizuri tu kuwa "kura ya maoni ya katiba mpya April 30,2015 haiwezekani."
Issue hapa ni kuwa kwanini serikali imeshindwa kuwapatia NEC yetu vifaa hivyo vya BVR.Jibu ni kuwa mifuko ya serikali imetoboka baada ya kutokuwa na nidhamu ya fedha.Hawaweki akiba,hawana vipaumbele,fedha nyingi inatumika nje ya taratibu ya fedha za umma.
Tunashukuru MUNGU kwa kufanya hayo yashindwe maana suala la katiba italipasua ardhi hii ya babu yangu vipande vipande.
Nimetosha kuwa MBUNGE WA RORYA - ukawa.