The big problem na hili zoezi la uboreshaji wa daftari la wapiga kura kwa mfumo mpya wa BVR ni upungufu wa mashine...........eti 250 tu kwa nch nzima!!
Tunaambiwa zinazojitajika kwa mujibu wa tume ni 15,000 ili zoezi lifanyike kwa ufanisi nchi nzima, lakini serikali chini ya CCM ilikataa ikakubali kuwapatia 8000 lakini mpaka sasa ndo hizo 250 tu zipo na wanajiamini na kutuambia......everything is alright, going as planned!!
Hivi hizi BVR zingine 7750 zilizosalia ziko wapi? Mmeshazinunua na kuzilipia nyie CCM?? Mbona tunaambiwa pia eti ishu ni ndege ya kuzileta hakuna na wakati huohuo MR FASTJET yuko angani kila baada ya siku kadhaa na bakuli lake la kuombea?
Laiti kama mashine hizi zote zingekuwa zipo na kila mkoa unaendelea na zoezi, mjadala ungekuwa na uelekeo mwingine tu!!
Lakini kwa sura hii, mimi naamini kabisa hawa wapuuzi hawana pesa kwanza za kulipia hizo mashine, pili za tume yenyewe kuendeshea zoezi zima nchi yote!! Tafadhali serikali kuweni wakweli kwa wananchi wenu na daima ukweli utawaweka huru!!