Uanaharakati umefeli Tanzania

DaudiAiko

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
302
274
Wanabodi,

Wengi wana uelewa kwamba katika nchi inayo minya haki, katika serikali inayo didimiza uhuru wa kujieleza, katika serikali inayo ingilia vyombo vya habari, uanaharakati ni njia muhimu katika kuhakikisha kwamba serikali inawajibika kwa maamuzi yote yanayofanywa. Katika kipindi hiki, nimeshuhudia njia mbali mbali zinazo tumiwa na wanaharakati kama njia ya kufikisha ujumbe kwa walengwa. Inawezekana kabisa kwamba asilimia kubwa ya walio hapa wanafahamu umuhimu wa "movement" nyingi duniani kama "Black lives matter" katika kutatua migogoro iliyopo kwenye jamii.

Kama ninavyo eleza kuhusu uanaharakati, ni vyema kufahamu kwamba lazima wapo wanaharakati ambao kazi zao zimeleta manufaa na ambao hawaja fanikiwa kushawishi walengwa kwa njia moja au nyingine. Vilevile ni muhimu kufahamu kwamba katika uanaharakati wa aina yoyote, lazima kuna masuala ambayo sio nyeti sana na ambayo yanayoweza kusababisha maafa makubwa kama siasa.

Katika jitihada zote za kuikosoa serikali, inavutia kuwa na hoja nzito au maoni ambayo kiukweli yanaweza kuleta mabadiliko chanya. inawezekana kwamba serikali huchukua muda sana kutafakari chochote kwa ufanisi kabla ya kufanya maamuzi yoyote na kwasababu hiyo mtazamo wakwao unaweza kuwa: "Serikali haikosei" au "Huwezi kuwa na maoni ambayo serikali haijawahi kuwa nayo".

Mpaka hapa, ni vyema kama ungekubaliana na mimi kwa kusema kwamba, "Mwanaharakati lazima awe na uelewa mpana kuhusu masuala mengi", " Mwanaharakati lazima awe na uwezo wa kuchambua suala lolote bila upendeleo", "Mwanaharakati lazima ajikite zaidi katika kutatua changamoto mbalimbali badala ya kukosoa tu". Mwisho kabisa, kama tunavyo fuatilia kesi ya Freeman Mbowe, mwanaharakati lazima awe tayari kwa lolote.
 
Mimi ni mwanaharakati huru, na nawaomba wote nilowakweza tusameheane, sisi ni Watanzania na tuwe na umoja.
Sina hela. Narudia sina hela.
 
Back
Top Bottom