Uamuzi wangu

Uamuzi wangu

mudy92

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2014
Posts
671
Reaction score
535
Wasalaaam,

Ni kijana wa umri wa miaka 23 sasa, nategemea kumaliza elimu yangu ya juu tarehe 16 June mwaka huu.Kifamilia mimi ni mtoto wa kwanza kati ya watatu, mmoja ni marehemu (wakiume) ko tumebaki wawili mimi na dada yangu mdogo, baba pia ni marehemu ila mama yupo.

Uamuzi wangu kuwa nataka kuoa sasa niendeleze familia/ukoo maana katika ukoo mimi pekee ndio mjukuu wa kiume naeweza uendeleza wote ni wakike. Nimepata binti wa Kisukuma umri miaka 19, hajaenda skuli, mweusi, mwembamba mrefu, adabu anayo, nataka kumfanya mama watoto.

Kaka/dada/baba/mama/ zangu nipeni ushauri juu ya uamuzi wangu natakamama yangu acheze na wajukuu wake maana ni mpweke sana alifiwa mume(baba yangu) na mtoto(mdogo wangu) ndani ya mwezi mmoja.
 
Course work una ngapi had sasa?
 
Kama unakazi oa tafuta watoto, Mie mtoto wa kwanza nilipata na 20 yrs tena nilikua sina kitu,, sasa hivi dogo yupo form one mungu akinipa uhai soon wajukuu nitawaona
 
mudy92

Subir kidogo mdogo wangu! Tafuta maisha kwanza! Age yako bado inaruhusu na hata huyo binti bado!

Kama wako ni wako tu! Familia ni zaid ya watoto! Unaweza fikir utampa mama furaha kumbe ikawa vise versa
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: Kig
Subir kidogo mdogo wangu! Tafuta maisha kwanza! Age yako bado inaruhusu na hata huyo binti bado!

Kama wako ni wako tu! Familia ni zaid ya watoto! Unaweza fikir utampa mama furaha kumbe ikawa vise versa

Atafute maisha kwani kayapoteza?maisha anayo sema atafute hela.
 
Furaha ya mama yako inaweza kuletwa na nyie wawili..ww na dada ako sio lazima wajukuu..ndoa ni jambo jema na ina hadhi yake..ila sababu zako za kuitaka hiyo ndoa nahisi ni dhaifu mkuu.
 
Usikurupuke kuoa, utajuta, mwanamke siyo ndugu yako tena hao wasiosoma utaishia kulia.
 
Jipe muda tena uweze kujipanga mikikimikiki ya kuanzisha familia. Furaha hupatikana kwa namna tofauti zaidi yahiyo uifikiriayo.
 
Kuoa ni jambo jema ila jipange kwanza.Hitimu masomo kwanza.Kisha tafuta ajira ndio uoe.
 
Back
Top Bottom