UAMSHO wanawatumia waislam kutimiza malengo yao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UAMSHO wanawatumia waislam kutimiza malengo yao

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mngony, Oct 20, 2012.

 1. mngony

  mngony JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2012
  Joined: Jul 27, 2012
  Messages: 2,780
  Likes Received: 1,596
  Trophy Points: 280
  mimi ni muislamu lakini nimeshtukia hichi kikundi cha UAMSHO kuwa ni kikundi cha kisiasa kinachowatumia waislamu bila wenyewe kujijua! Uamsho wanataka kujitenga na bara wakisingizia huku ni makafiri, je huku hakuna waislamu? Kwa nini wamuue askari ambaye ni Muislamu mwenzao? Katika uislam si haramu kumwaga damu ya muislamu mwenzako? hawa waislamu gani? kwa nini watoe taarifa za kuwa kiongozi wao ametekwa na hali ilikua haijulikani yuko wapi na kama ametekwa au la!? dereva anasema alishuka akapanda gari lingine na alikua akiwasiliana na watu, huko ndo kutekwa tena bila hata purukushani tena gari limekuja taratibu! na hilo gari lake mwanzo alikua akiendesha mwenyewe kwa nini alimua kumpisha dereva wake?Huo si uongo ambao ni haramu katika uislamu! Kwa nini zichomwe ofisi za CCM peke yake, mbona CUF nayo ni serikali pia? je CCM huko zanzibar viongozi wao makafiri? je hao CUF waumini? kama ni hivyo kwa nini unamuacha huyu CUF kwa sbb anaonekana mnafiki anashirikiana na makafiri CCM! Hawa ni wanasiasa wa mda mrefu ambao wamekua wakitaka Zanzibar ijitenge lakini wakashindwa katika hoja za kisiasa,ndo kipindi kile ikabidi rais achaguliwe ambaye sio mhafidhina akawekwa sheina agombee, na Rais kikwete akaahidi kusimimia muungano pamoja na shein hadi ikaundwa kamati ya kushughulikia kero ya muungano! kwa vile walishindwa wameamua kutumia mwamvuli wa dini! ni hatari sana, ni kama kipindi kile CUF ilivokuwa ikijinasibisha na uislam! Na kila mwenye akili atakubali kuwa hichi kikundi Kina mkono mkubwa kutoka mataifa ya nje, taifa fulani ambalo siku hizi limekua mstari wa mbele kusimamia mataifa kujitenga maadam wana maslahi ya kiuchumi pindi tu taifa hilo likishajitenga.
   
 2. D

  Dr.Who Senior Member

  #2
  Oct 20, 2012
  Joined: Jun 23, 2012
  Messages: 172
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siamini kabisa wewe ni muislam, naamini kabisa wewe nikikojozi kama vikojozi wenzako, hujawai fika kwenye mihadhara ya muamsho na kuwasikiliza zaidi unachoongea nikilekile wanachoongea vikojozi wenzio

   
 3. mngony

  mngony JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2012
  Joined: Jul 27, 2012
  Messages: 2,780
  Likes Received: 1,596
  Trophy Points: 280
  kaka mimi ni mwislamu. kama unahoja toa tusitukanane wala mimi sitokutukana. kumbuka shujaa sio yule mwenye nguvu nyingi ila ni yule anaeweza kudhibiti ghadhabu zake.
   
 4. A

  Amani kwa wote Member

  #4
  Oct 20, 2012
  Joined: Sep 22, 2012
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hata enzi za mtume wapo watu walijitokeza wakasema na wao ni waislamu kumbe ni wanafki wakubwa
   
 5. D

  Dr.Who Senior Member

  #5
  Oct 20, 2012
  Joined: Jun 23, 2012
  Messages: 172
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Asante, Mkuu, kama nimuislam jaribu kufika kwenye mihadhara au sikiliza kasseti zao ili uelewe policy zao badala ya kuleta mada dhidi ya policy za uamsho, madai kama haya tunayasikia kwa vikojozi, kwahiyo ni vizuri uwasikilize mwenyewe uelewe ukweli

  Respect
   
 6. B

  Bob G JF Bronze Member

  #6
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hawa watu nikawaida yao kutumika ccm imekuwa pia ikiwatumia sana wakati wa kupiga kura, na Cuf nayo inawatumia sana na sasa UAMSHO mara Ponda, na bei yao ni ndogo sana yaani pilau, kofia, kanga, kitenge, Tshirt na ccm haifanyi juhudi ya kuwapa maarifa ya kufikiri ili ifikie malengo yake.
   
 7. kbm

  kbm JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 4,964
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  mkuu mbona una itikadi kali na maneno yasiyokuwa na tija? Toa hoja sio kutukana.
   
 8. S

  Sadagada Member

  #8
  Oct 20, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 76
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  Tatizo moja hawa wa2 sidhani kama wakiambiwa vitu na viongozi wao huwa wanafikiria kwa kina kabla ya kuchukua hatua. Mfano ishu ya mbagala nilitegemea hata yule mtoto wa kislam achukuliwe hatua na waislam. Hivi kwa mfano ukiwa umetoka kazini mara unakuta TV yako ya chumbani imevunjika. unamuuliza mwanao, anakwambia kuwa ameivunja mtoto wa jirani alipokuwa anajaribu kuibeba na kukimbia nayo. kwa kuwa nilimwambia hana nguvu za kuibeba hiyo TV. sasa yeye ndio akaidondosha. Hivi wewe kwa akili zako utaenda kugombana na mzazi wa mtoto wa jirani kweli?. je hautamchukulia mwanao hatua aliyetoa tv ndani?.
   
 9. D

  Dr.Who Senior Member

  #9
  Oct 20, 2012
  Joined: Jun 23, 2012
  Messages: 172
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama Mzazi wa mtoto anakawaida ya uchokozi, na mtoto wake anapokosea kutakuwa na vitu viwili;

  1-Kafundishwa tabia mbaya na wazazi wake
  2-Katumwa (kukojoa) au kuvunja tv kwa makusudi

  Hii inategemea uhusiano wako na mzazi, hivi karibuni mzazi huyuhuyu, alimzika mtoto wake Bagamoyo kwenye makaburi ya waislam na kuweka misalaba, na pia alichoma qura'n kwa makusudi nk...nk..nk... Bila kuomba msamaha, je kutakuwa na uhusiano mzuri?


   
 10. S

  Sadagada Member

  #10
  Oct 20, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 76
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  kwa hiyo huyo mzazi kama anaishi nyumba ya jirani na ukute amepangisha. utachukua uamuzi wa kwenda kuharibu na kuchoma nyumba nzima pamoja na wapangaji wengine ikiwemo hata ya baba mwenye nyumba?. kisa una bifu na m2 mmoja?
   
 11. mngony

  mngony JF-Expert Member

  #11
  Oct 20, 2012
  Joined: Jul 27, 2012
  Messages: 2,780
  Likes Received: 1,596
  Trophy Points: 280
  sorry sijazungumzia la Ponda,nazungumzia UAMSHO,yanaweza kuwa yanafanana kidogo kwa kuwa yanahusu kiongozi wa kiislamu lakini nazungumzia dhana nzima ya UAMSHO na harakati zao za kujitenga na Tanzania bara! na pia sio vizuri kutukejeli kuwa sio ndo tunapewa hizo kanga na kofia na CCM, kumbuka hawagawi misikitini au makanisani. tusiharibu mjadala tutoe hoja
   
 12. mngony

  mngony JF-Expert Member

  #12
  Oct 20, 2012
  Joined: Jul 27, 2012
  Messages: 2,780
  Likes Received: 1,596
  Trophy Points: 280
  naomba waislamu tuchangie! kwa wakristo siwakatazi ila najua wengi wenu mkichangia mtaleta kejeli au maneno makali mtawaamisha waislamu hawataweza kunijibu mimi watakua wanajibu kejeli na maneno yenu makali badala ya kujibu hoja zangu. otherwise mchangie vizuri na msitoke nje ya mada hope mumenielewa
   
 13. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #13
  Oct 20, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Muislam anayemuua muislam mwenzake hugeuka kafiri rightaway. Sitashangaa kusikia watu wakiwakana uamsho kwa vile hawajafuata sharia ya Mwenyezi Mungu. Wanataka kujitenga na muungano ingawa wanatumia njia chafu na yenye madhara kwao kwani wataumizana wakati serikali ya muungano iko Dar ikitanua na bosi wake akijirusha ughaibuni na jamaa zake. Tumieni akili jamani mtamalizana na mnachotafuta hamtakipata kwa vile mtawapa jamaa sababu ya kuwavunja vunja viungo.
   
 14. mngony

  mngony JF-Expert Member

  #14
  Oct 20, 2012
  Joined: Jul 27, 2012
  Messages: 2,780
  Likes Received: 1,596
  Trophy Points: 280
  really it is! Sasa sijiskia labda kusema askari kauwa bahati mbaya! hapana kapigwa mapanga kabisa alaf tunakuja kudai tunapigania haki za waislamu wakati tunawauwa wenzetu wenyewe! mwislamu anaefikiria hapa tu panatosha kujiuliza! UAMSHO NI SIASA KABISA WALA SIO ABOUT RELIGION
   
 15. D

  Dr.Who Senior Member

  #15
  Oct 20, 2012
  Joined: Jun 23, 2012
  Messages: 172
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kama Judicial System inampendelea jirani kuliko wewe, upouwezakano mkubwa kwa binadamu yoyote kuchukua sheria
  mkonono n haya ndiyo yaliyotokea wakati jirani anachoma Qur'an, filamu ya matusi kwa Mtume (S.A.W), kuzika mkiristo makaburi ya waislam na kuweka misalaba hawakuchukuliwa hatua yoyote na hata kikojozi hasingechukuliwa hatuwa ya kisheria kama shinikizo la waislam lisingefanyika
   
 16. D

  Dr.Who Senior Member

  #16
  Oct 20, 2012
  Joined: Jun 23, 2012
  Messages: 172
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama askari alikuwa upande wa maadui nae ni adui hata kama ni raia wa nchi moja au dini yako, yeye amesha kusaliti nae nisawa na adui
   
 17. mngony

  mngony JF-Expert Member

  #17
  Oct 20, 2012
  Joined: Jul 27, 2012
  Messages: 2,780
  Likes Received: 1,596
  Trophy Points: 280
  mtume hakuwajua wanafki? aliwauwa? sasa we hukmu ya kumuua mwislamu mwenzako inatoka wapi? alaf nenda kapitie kwenye vitabu vya dini hukmu ya kumuua mwislamu mwenzko kwa maksudi ni straight motoni! hiyo kwa bahati mbaya unaambiwa ufunge miezi miwili! uaskari wake ndo uadui kwa uislamu? ile si kazi tu. kwa hakika kila mmoja wetu atakuja kuulizwa yeye kama yeye kwani kila mtu amepewa akili na uwezo mkubwa wa kufikiria
   
 18. D

  Dr.Who Senior Member

  #18
  Oct 20, 2012
  Joined: Jun 23, 2012
  Messages: 172
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kama wewe kweli ni Muislam sio kibaraka, kasome Qur'an 66;9. nimefunga mchezo nakusubiri......
   
 19. mngony

  mngony JF-Expert Member

  #19
  Oct 20, 2012
  Joined: Jul 27, 2012
  Messages: 2,780
  Likes Received: 1,596
  Trophy Points: 280
  nimeisoma, je huyo mwislamu mwenzetu mliyemuua mmejua yukoje au sababu yeye tu ni askari? Unakumbuka mkataba wa hudaybia ulisainiwa kati ya nani na nani? Tunaacha kufuata kiigizo chema kutoka kwa mtume tunakurupuka na matokeo yake ni vurugu! mtume angekua hvo huo uislam ungetufikia? we unajua kuwa kuna mtu kipindi cha mtume alikua akivizia nyumbani kwa mtume then akawa anajisaidia mlangoni then anaondoka, mtu alimjua na wala hakukurupuka kumhukumu kupigwa wala kuuwawa bali kila anapochafua anasafisha, je waislamu leo tunaiga mwenendo wa mtume! alaf hata mtume aliambiwa msiwapige wala kuwatoa watu katika majumba yao mpka watakapoanza wao kuwapiga,na ndo maana mtume aliweza kuishi na makafari kupitia mkataba wa hudaybia! na ikitokea kosa kafanya mmoja na sio makafiri kwa pamoja hakukurupuka na kuwahukumu makafiri wote! Aliyemlea mtume baada ya kufarika mama na babu yake alikua mwislamu? mbona waliishi bila tatizo wala mtume hakumhukum mpka anakufa anabaki kumkumbusha atamke shahada? hiyo aya ya 66:9 haikushuka? kwa nini mtume hakumhukumu mjomba wake huyo? ni kwa sbb hakuanzisha vita aliishi nae vizuri.
   
 20. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #20
  Oct 20, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,002
  Trophy Points: 280
  Mimi nijuavyo waislam hawahongwi kofia ama pilau
  Ila najua kuna wagalatia wanahongwa gongo ulezi chibiku tu na kutoa kura zao kwa wagalatia mafisadi
  Ama kuhusu malengo ya Uamsho hili darasa pana
  Walianza na harakati nyingi za kijamii lakini sasa kuna hili Zanzibar kuondokana na ukoloni wa Tanganyika
  Kwani ukoloni ? Kwa sababu nia ya Muungano haikua nzuri watanganyika walikua na nia ya kuimeza zenj
  Wewe fikiria kitu kimoja tu kuna sababu gani za kufanya suala la mafuta kuingizwa kitapeli ndani ya mambo ya muungano?
  Na wakati huo zanzibar hawafaidiki na gas ya songo songo ?
  Hawafaidiki na madini ya dhahabu
  Kwa nin tanganyika wasiwaachie zenji kuchimba mafuta yao ?
  Jee inawezekana tuhamishe makao makuu ya serikali ya muungano yawepo zenji?
  Mambi ni mengi na kazi ya uamsho ni hii kuwafahamisha waislam kuwa muungano sio
  Mila na utamaduni wa nchi hizi ni tofauti
  Mfumo wa maisha wa nchi hizi ni tofauti
  Tabia za watu wake pia ni tofauti
  Marafiki wa tanganyika pia ni tofauti na wale zenj
  Hivyo muungano ulikua ni kasa la kulazimishwa kihistoria
  UAMSHO WANAAMSHA. Na support yao ni kubwa kuliko unavodhani wapo wabunge police mawaziri majaji wakulima wafanyakazi bila ya kujali itikadi zao wote wanasema Zanzibar kwanza

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
Loading...