Ndugu Kwanza naomba nikusahihishe. Msemo "mpaka kieleweke" sio kauli mbiu ya chadema. ni msemo wa kiswahili uliotumika miaka mingi kabla hata chadema hawajaanza harakati, na umekuwa ukitumiwa na watu ambao hawataki kukatishwa tamaa katika jambo wanalolifanya au wasiokubali kushindwa kwa dhuluma. Mifano ipo mingi Wanafunzi wa vyuo wanapodai maslahi yao, makonda na madereva wasipofikisha hesabu utawasikia wakisema mpaka kieleweke, wanaapolo wakitafuta mawe bila mafanikio utasikia mpaka kieleweke nk.
Mtu yeyote anayetumia lugha ya kiswahili aweza kutumia msemo huu kwa maana anayofikiri yeye itamtia moyo na kufikisha ujumbe kwa wahusika kuwa hawezi kukatishwa tamaa kirahisi.
Post yako imekosa mantiki kwa sababu unajaribu kuhusianisha makundi mawili ambayo hayana uhusiano huo kwa kuwa eti wametumia misemo ya kiswahili inayofanana. Hakuna hoja yeyote ya msingi umetoa ya kushawishi kuwa chadema wana jambo wanashirikiana na hawa wana uamsho. hata kama kuna maeneo ambayo sera zinaonekana kushabihiana lakini hili haliwafanyi kuwa na ushirikiano hata kidogo.
Naamini CHADEMA watafika zanzibar kuelimisha, lakini wataenda kama chama cha siasa km vile walivyo vyama vingine na si kwa gia ya uamsho.
-Kwanza ukumbuke Motive ya CDM ni kuelimisha watu haki zao, hawa uamsho ukisikiliza hotuba zao ni kujenga chuki dhidi ya watu fulani kwa kisingizio cha kuonewa
-Pili Chadema wanapingana na Ufisadi, Uamsho wanapingana na ukristo
-Tatu Chadema wanapigania katiba mpya ya nchi nzima, uamsho wanataka tu kuvunja muungano
Hawa huwezi kuwaweka meza moja hata siku moja